Serikali ichukue hatua hizi haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la upungufu wa fedha za kigeni

Serikali ichukue hatua hizi haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la upungufu wa fedha za kigeni

Mkiambiwa nyie ni wajinga mtabisha? Bilioni 550 ndio expenditures ya mwaka mzima ya serikali kuhudumia magari mapya,mafuta na vipuri Sasa hayo magari ya bil.500 ndio magari gani? Ni mitambo ya jeshi?
Wewe ndio hauna akili. Na kubishana na wewe ni kupoteza muda tu. Chawa ni chawa, atatetea chochote kibaya au kizuri.
 
1. Hakuna safari ya kikazi ya Rais ya nje isiyo na tija, kama hufuatilii ni uvivu wako lakini mara kwa mara zinatolewa press conference na DPC Zuhuru kuhusu ziara hizo na faida zake. Dunia ya Sasa inahitaji mazungumzo lakini anapokwenda nje kuzungumza ina tija zaidi kuliko kuwakilishwa bila hivyo tusingesikua Rais wa Marekana anazuru katika nchi za Afrika.

2. Hoja ya pili ni mpaka pale nchi itakapokuwa na wawekezaji wengi na wenye uwezo wa ndani wa kuwekeza kwenye miradi mikubwa. Kwa mfano uwekezaji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee unagharimi Zaidi ya Dola za kimarekani billion 7 ambazo ni sawa na Trillion 16 za kitanzania. Kwa wawekezaji waliopo ni nani ambaye ana hiko kiwango Cha pesa kutukamilishia ujenzi huo? Hata matajiri 10 wakubwa wakawekeza Kila kitu Chao Bado hawawezi kufanya mradi kama huo. Ingefaa kweli miradi ijengwe na wazawa ili malipo yafanyike Kwa shilingi lakini tuseme kweli tutachelewa Zaidi.

Hoja ya Tatu, Serikali inakopa ili kuharakisha maendeleo na zaidi mikopo hiyo ni Ile yenye riba nafuu sana au isiyo na riba kabisa. Pia, tunakopa ili tuwe na akiba kubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi ya nje, bidhaa na Teknolojia. Ingefaa utupe na ufafanuzi, Serikali itumie njia Gani kugharamia Kwa haraka miradi mikubwa kama Tukiachana na mikopo.

Hoja ya nne, umemtaja Makamu wa Rais Dkt.Mpango kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia wizara ya fedha na wizara ya mipango na uwekezaji Kwa uwezo wake wa kitaaluma kwenye masuala ya uchumi na fedha na ndio maana ukataka wizara hizo ziwe chini yake lakini umesahau jambo Moja kubwa ambalo litahitaji majibu baadaye, je asipokuwepo Dkt Mpango katika ofisi ya Makamu wa Rais na akawepo mtaalamu wa Sanaa ofisi ya Makamu wa Rais, je Bado itahitajika wizara hizo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais?

Hoja ya Tano, siamini kama unaendesha asasi yoyote ya kufanya tathmini ya uchumi mpaka uje na hoja ya kwamba tunakwenda kutumbukia kwenye mdororo wa kiuchumi. Ni vema hoja yako hii ingejikitika kwenye takwimu halisi Zaidi ya blabla Kwa sababu uchumi ni namba na namba hazidanganyi.
Haya mambo unaandika ukiwa umekula nini?.

Waachie wataalam wajibu hizi hija, wewe bado mdogo.
 
Haya mambo unaandika ukiwa umekula nini?.

Waachie wataalam wajibu hizi hija, wewe bado mdogo.
Hizi ndio hoja msizopenda kuzisikia, mnataka Mbowe akisema nchi itauzwa au uchumi umedorora wote tushangilie utafikiri tumelewa. In short bwana mdogo hajatoa hoja hata Moja ya maana au yenye uzito wa kujadilika,vyote ni vitimbwi vilivyozoeleka.
 
1. Hakuna safari ya kikazi ya Rais ya nje isiyo na tija, kama hufuatilii ni uvivu wako lakini mara kwa mara zinatolewa press conference na DPC Zuhuru kuhusu ziara hizo na faida zake. Dunia ya Sasa inahitaji mazungumzo lakini anapokwenda nje kuzungumza ina tija zaidi kuliko kuwakilishwa bila hivyo tusingesikua Rais wa Marekana anazuru katika nchi za Afrika.

2. Hoja ya pili ni mpaka pale nchi itakapokuwa na wawekezaji wengi na wenye uwezo wa ndani wa kuwekeza kwenye miradi mikubwa. Kwa mfano uwekezaji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee unagharimi Zaidi ya Dola za kimarekani billion 7 ambazo ni sawa na Trillion 16 za kitanzania. Kwa wawekezaji waliopo ni nani ambaye ana hiko kiwango Cha pesa kutukamilishia ujenzi huo? Hata matajiri 10 wakubwa wakawekeza Kila kitu Chao Bado hawawezi kufanya mradi kama huo. Ingefaa kweli miradi ijengwe na wazawa ili malipo yafanyike Kwa shilingi lakini tuseme kweli tutachelewa Zaidi.

Hoja ya Tatu, Serikali inakopa ili kuharakisha maendeleo na zaidi mikopo hiyo ni Ile yenye riba nafuu sana au isiyo na riba kabisa. Pia, tunakopa ili tuwe na akiba kubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi ya nje, bidhaa na Teknolojia. Ingefaa utupe na ufafanuzi, Serikali itumie njia Gani kugharamia Kwa haraka miradi mikubwa kama Tukiachana na mikopo.

Hoja ya nne, umemtaja Makamu wa Rais Dkt.Mpango kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia wizara ya fedha na wizara ya mipango na uwekezaji Kwa uwezo wake wa kitaaluma kwenye masuala ya uchumi na fedha na ndio maana ukataka wizara hizo ziwe chini yake lakini umesahau jambo Moja kubwa ambalo litahitaji majibu baadaye, je asipokuwepo Dkt Mpango katika ofisi ya Makamu wa Rais na akawepo mtaalamu wa Sanaa ofisi ya Makamu wa Rais, je Bado itahitajika wizara hizo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais?

Hoja ya Tano, siamini kama unaendesha asasi yoyote ya kufanya tathmini ya uchumi mpaka uje na hoja ya kwamba tunakwenda kutumbukia kwenye mdororo wa kiuchumi. Ni vema hoja yako hii ingejikitika kwenye takwimu halisi Zaidi ya blabla Kwa sababu uchumi ni namba na namba hazidanganyi.
Safari gani ya Rais Ina tija. Ile ya kwenda kumuona baba yake na Rihanna au?. Safari za Rais zingekuwa na tija Kama Dolla isingeadimika. Ina maana hata utalii haulipi.
 
Wameshaomba msaada kwenye benki ya dunia. Subiri maokoto yanakuja soon
 
Kuna nchi moja huko kuna viongozi wa mchongo, hawana uchungu na maisha ya raia pamoja na rasilimali zao.

Kiufupi ni kikundi cha wahuni tu, hawapo kusaidia raia bali kuwaibia tu, wapo kama vibaka.
Ukiona mtu anafanya jambo lolote hata kuua ikibidi ili aishinde Uchaguzi haya ndio matokeo yake.

Sisi tulijua tangu mwanzo 2020
 
Safari gani ya Rais Ina tija. Ile ya kwenda kumuona baba yake na Rihanna au?. Safari za Rais zingekuwa na tija Kama Dolla isingeadimika. Ina maana hata utalii haulipi.
Acha kujiita mchumi kujiita hivyo ni kuwadhalilisha wachumi. Tatizo lako ni kusikiliza ambao hata hawahusika ili wakupatie Takwimu za kiuchumi, kumsikiliza Lissu au Mbowe na kuacha kumsikiza Dkt.Mwigulu haya ndio matatizo yake.

Dkt.Mwigulu amebainisha wazi kwamba Dola zimepungua Kwa sababu tunalipa sana madeni ili tusiingie kwenye hatari ya kutokukopesheka tena. Kama wewe ni mchumi nichambulie hii scenario kiuchumi, Nchi ambayo bajeti yake Kwa Zaidi ya 50% inategemea mikopo na misaada na huku ikiwa low taxable capacity ,je itumie njia ipi kufinance budget deficit ikiwa imeamua kuachana na mikopo ?

Je, kufidia hiyo gap ya 50% ifidiwe Kwa kuongeza Kodi au kukopa mikopo nafuu yenye riba nafuu?

Je, ni kipi Bora kiuchumi kati ya kuongeza Kodi ili kuwaumiza wananchi au kukopa concessional loan ya miaka ishiri kama ule mkopo wa WB wa kukabiliana na UVIKO 19?
 
Hii nchi ina wezi waliokubuhi ,,,na wana mbinu za kuiba wamebobea. Hebu tafakali mtu Kama tutuba ( Gavanna BOT ana uwezo mkubwa sana lakini anawatazama tuuu .Nan kama mama
Tatizo hao wezi wamejipanga kwa safu na wameunda Cartel yao wakiongozwa na raia namba moja. So kila wizi unaofanyika una baraka zake zote na ndio maana huwezi sikia wala kuona Wakurugenzi wakiwajibishwa. Nchi inayojitambua Lameki asingekuwepo ofisini hadi leo
 
1.Narudia kukwambia Rais hajawahi na haitakuja kutokea akafanya safari za hasara.
Swala la sijui kununua magari ya Viongozi huna hata ushahidi zaidi ya kuropoka tuu.Kwa taarifa Yako tuu Rais amenunua magari mengi ya vitendea kazi Kwa taasisi kuanzia Wizara ya Kilimo hadi Halmashauri Sasa sijui hiyo ni anasa ya wapi.

2.Aliyekwambia ni lazima Dola itaendelea kushuka Kila mwaka ni nani? Harafu Dola inalipwa Kwa Dola Kwa hiyo thamani ya Shilingi ya Tanzania vs Dola haihusiki na kulipa Madeni,Ili kutunza thamani ya wakopeshaji ndio maana wanaweza riba.

3.Wazo ni zuri ila Hao wakandarasi wa ndani wenye uwezo wa utaalamu, Fedha na teknolojia wako wapi ili wapewe kazi? Bora hata ungesema kwenye Suala la sheria ya local content kwenye kazi za ukandarasi pale inapolazimu wa Nje kupewa walau 40% ya kazi afanye Sub iwe kisheria.

4.Umeandika ujinga,hata Kwenye vyeti tuu Mwigulu ana vyeti Vikali kuliko Mpango ndio maana nakwambia wewe ni mjinga , upungufu wa Dola haujasababishwa na utendaji wa Wizara ya Fedha au Mwigulu

5.Wakati wa Magu tuliwahi kuwa na uhaba wa mafuta ni Aisha unajitoa ufahamu au unadhani wote ni wajinga kama.wewe.Na haikuishia mafuta tuu hadi sukari,saruji,chanjo za Watoto Hadi condoms.Na yote hayo yalitokea wakati uchumi wa Dunia uko.poa na hauna Changamoto zozote.

Mwisho pamoja na Changamoto ya uhaba wa Dola na mafuta Bado uchumi wa Sasa ni mzuri na private sector inakua Kwa Kasi sana kuliko wakati wowote.Unaweza soma monetary statement ya BoT mwezi wa 8.
Uhaba wa mafuta halafu yakauzwa 1500 kwa litre?
 
Uhaba wa mafuta halafu yakauzwa 1500 kwa litre?
Kwani huo uhaba ulikuwa all over? Ulikuwa locally na kama kawaida habayzilipigwa pini na kama ni bei yanaweza kuuza hata buku Cha maana ni bei ya soko Duniani ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom