Serikali ichukue hatua hizi haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la upungufu wa fedha za kigeni

Ziara za viongozi wote ni zile zile na zina uzito uleule wa kiitifaki lakini tofauti zinaweza kuonekana kutokana na ukubwa wa Taifa husika. Kwa hiyo unataka Rais wa Tanzania afanye ziara yenye malengo Yale Yale na Rais wa Marekani? Unapozungumzia tija kwenye ziara ya Rais wa Tz usiangalie tija inayopatikana na Rais wa Marekani. Ziara zina tija kubwa sana na faida ni nyingi, kwanza nchi inafunguka na bidhaa za Tanzania zinatambuliwa kimataifa. Kwa mfano Rais anapoenda kwenye maonesho makubwa ya kimataifa, anaenda na watu ambao watatangaza utamaduni wetu na hivyo kufanya hata vinyago vya mmakonde kupata soko la kimataifa.

Ndio maana katika sifa za mgombea Urais wa CCM mojawapo anatakiwa kuwa na uzoefu wa masuala ya kimataifa. Ikiwa na maana kubwa kwamba kiongozi mwenye sifa hii atatusaidia kwenye masuala mengi ya kimataifa na mojawapo ni ziara za nje na kuizungumzia nchi kimataifa.

Acha nikuambie tu ukweli, unaposikia kipande Cha SGR Dar-Kimekamilika Kwa 99 au JNHPP imefikia 90 mpaka sasa ni misaada na mikopo ndio imetusaida. Kukopa Kwa lengo la kufanya uwekezaji wenye faida kiuchumi sio hasara maana gharama za mkopo zitafidiwa na mradi husika. Kama tusinge kopa na tukajenga Kwa pesa zetu ni lazima Kodi zingepanda sana ili kugharamia mradi huu na katika hoja zako sijaona uliposema serikali iongeze Kodi kugharamia pengo la kutokukopa. Tungesema tuwatumie wawekezaji wa ndani kwenye miradi mikubwa maana yake ni hii mradi kama SGR au JNHPP ungejengwa kwa miaka 20 wakati wakezaji WA nje au mkopo unaweza kujengwa Kwa miaka 5 ,kipi Bora?
 
Naongezea
1.BOT inunue madini Kwa wafanyabiashara au makampuni alafu iuze Kwa Dora
 
Naongezea
1.BOT inunue madini Kwa wafanyabiashara au makampuni alafu iuze Kwa Dora
Ni kweli, hususani wachimbaji / wafanyabishara wadogo na wakati. Itaweza kununua kwa shilingi na kuuza kwa Dollar.

Kwa bahati mbaya yale makampuni makubwa tulikubaliana wakati wa JPM kuwa wauze madini kwenye soko la ndani lakini sidhani kama yale makubaliano yanatekelezwa baada ya JPM kututoka.
 
Ccm wanaficha hela na kuiba ili 2024&2025 wazitumie kuiba uchaguzi kwa kuhonga wapiga kura na wasimamizi
Ni hatari sana pale serikali inapokuwa inawaza namna ya kuiba uchaguzi ujao muda wote badala ya maendeleo.
 
Hii nchi ina wezi waliokubuhi ,,,na wana mbinu za kuiba wamebobea. Hebu tafakali mtu Kama tutuba ( Gavanna BOT ana uwezo mkubwa sana lakini anawatazama tuuu .Nan kama mama
 
Hii nchi ina wezi waliokubuhi ,,,na wana mbinu za kuiba wamebobea. Hebu tafakali mtu Kama tutuba ( Gavanna BOT ana uwezo mkubwa sana lakini anawatazama tuuu .Nan kama mama
Naam, ukiwagusa tu unaondolewa kwenye nafasi yako. Kuna watu hiyo ndio shughuli yao, wanafanya juu chini wawepo serikali ili waibe kwa manufaa yao na vizazi vyao.

Maana yake ni kwamba ili Tanzania ikomeshe wizi ni aidha tuwe na rais mzalendo ambaye hatowalinda wezi au tufanye mabadiliko ya katiba na kumwondolea baadhi ya mamlaka rais wa nchi.
 
1.Umewahi kumuona Rais alifanya safari za anasa?

2.Swala la kusitisha kukopa Kwa Sasa ni hadithi za kufikiria maana hukopo Leo ukalipa kesho na Kwa situation ya Sasa mikopo ya Nje ndio inatakiwa Ili kuongeza reserves.

Hapa Serikali itafute zaidi mikopo nafuu

3.Hakuna kampuni ya kigeni itakubali kulipwa Kwa pesa ya madafu

4.Wizara ya Fedha na Mipango kuwa chini ya Ofisi ya VP ndio itaongeza reserves? Umeandika ujinga.

5.Tanzania haiwezi kuingia kwenye huo mgogoro kamwe,kama ilishindikana wakati wa uviko 19 ndio iwe saizi? Hakuna kitu kama hicho.

Mwisho naunga mkono utaratibu ambao BoT unaendelea nao wa rationing ya Dola ingawa Kuna Baadhi ya bidhaa tuzuie kabisa ku import hasa furnitures na Baadhi ya urembo na bidhaa zinazofanana na hizo.
 
Ni mpuuzi huyo jamaa
 
Kwamba tatizo la Dola ni Kwa sababu Wataalamu hawajatumika au? Mbuzi ni.wengi.sana Nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…