Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Lakini asilimia 99 ya waliokufa ni watu waliokuwa na magonjwa mengi na ni tishio zaidi kwa wazee.
Hawa ndio waliostahili kuwekwa sehemu maalum, kwa uangalizi wa karibu zaidi, wakiwa wametengwa wasigusane na jamii nyingine, wakati shughuli za kuudhibiti ugonjwa zikiendelea.

Ngoja niweke siasa kidogo:
Hizo picha mwanzo zilinitisha mkuu 'Cannabis' nilipoziona kwa mara ya kwanza kabla ya kusoma andiko lako.

Jambo la kwanza nililofikiri ni maandalizi ya uchaguzi wetu mkuu mwaka huu!
 
Kwa hiyo basi tuamue kwamba hawa ndio wanaohitaji 'isolation'; badala ya hao wenye kinga zao za miili? Au unasemaje?

Wazee wote wenye afya dhaifu dhaifu watengwe majumbani mwao, wasitembelewe na hawa watu wengine wanaoweza kuwaambukiza ugonjwa huo.

Na hapo hapo juhudi nyingine za kusitisha maambukiza hata katika kundi hilo la wenye nguvu zikiendelea kusisitizwa!

Corona sio hatari sana.

Hatari ni upashanaji habari unaosambaa haraka.

Hatari ni 'corona' hakujulikana, ndio kwanza anajitokeza, hana chanjo wala kinga yoyote zidi yake.

Lakini corona, katika 'virulence' yake hana tofauti yoyote na hawa wengine tunaowajua kwa siku nyingi, kama 'influenza' n.k.

Tutamzoea tu na kumdharau siku sio nyingi.
Nenda Italia leo waambie Corona siyo hatari sana.
 
Hawa waathirika wa Corona ambao ni takribani 6 waliotangazwa hadi sasa, na wote wametokea nje ya mipaka ya Tanzania. Walifanyiwa vipimo uwanja wa ndege walipowasili au ni baada kuingia mtaani ndio wakagundulika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunafanya utani na uhai wa wananchiwetu. Hata tukifanya maombi kwa huu utani unaoendelea tutakuwa tunamkufuru Mungu tu.
 
1584631943918.png
 
Hawa waathirika wa Corona ambao ni takribani 6 waliotangazwa had sasa, na wote wametokea nje ya mipaka ya Tanzania, Walifanyiwa vipimo uwanja wa ndege walipowasilia au ni baada kuingia mtaani ndio wakagundulika?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuache ushamba jamani. Mipakani na airport hawapimi corunavirus kuona kama msafiri ameambukizwa. Wanachofanya ni kupima tu joto la mwili kuona kama liko juu (ambayo ni moja ya dalili za mtu anayeugua ugonjwa wa corona. Zaidi wanakupa form unajaza kuelezea sehemu ulizotembelea kabla hujasafiri au kama umeshaishi sehemu yenye mlipuko. Kama joto liko sawa unaruhusiwa kuingia lakini unapewa angalizo la kuwa makini kwa kujitenga kwa wiki mbili ili kama uliambukizwa usisambaze kwa watu wengine. Nichi zote ndivyo wanavyofanya. Hata wakati ule wa mafua ya ndege walikuwa wanafanya hivi hivi. Wangekuwa wanapima corona virus yenyewe kusingekalika kwani vipimo bado ni vichache na wasafiri ni wengi. Imagine vuiwanja vyenye wasafiri wengi kama Hearthrow waanze kupima kila msafiri kama ana virus.... itachukuwa muda mrefu sana.
 
Hv wote ambao wamekutw na corona n kutoka nje y nchi..kwa nini mipaka y kuvuka nje ya nchi isizuiwe ??
 
Back
Top Bottom