Serikali ikiondoa unafiki na chuki bado Kagera inaweza kuchomoza, Chalamila unatakiwa kujua haya

Serikali ikiondoa unafiki na chuki bado Kagera inaweza kuchomoza, Chalamila unatakiwa kujua haya

Tatizo lenu ni ego ! Yaani kila kitu unalaumu serikali.

Kilimanjaro imehujumiwa sana kuliko Kagera, iko mpakani kama Kagera, wana Kahawa kama Kagera tena Kagera wana Ardhi nzuri na kubwa zaidi, wasomi kama Kagera. Sasa tofauti iko wapi ? Ni utamaduni pamoja na kwamba kuna wasomi wengi Kilimanjaro wananchi wa Kilimanjaro wana wathamini zaidi wafanyabiashara kuliko wasomi. Pili Kilimanjaro kuna utamaduni wa harambee za shule, makanisa, na hata barabara za mitaani. Tatu watu wa Kilimanjaro wana wekeza nyumbani kwao na ku lobby ili wapate pesa za maendeleo. Nne Kilimanjaro wamewawezesha wanawake kwenye maendeleo kuanzia biashara hadi kilimo.

Hakuna hujuma mpaka makatibu wa CCM walitoka huko🤔 badala ya kulalamika jiangalieni wenyewe
Ego na ubishi wa kuamini tunajua kila kitu. Unamchukua mtoto wa mjomba au shangazi yako kutoka nyumbani kabisa, akifika Dar anakuwa wa kwanza kukuhujumu hapo nyumbani.

Ndio hulka zetu watu wa Kagera, RC Chalamila sio wa kuchukiwa, ametupa changamoto nzuri.
 
Ukiona mtu anazungumzia Umalaya,mashoga, na uvivu kwamba ni sifa ya mkoa flan ndani ya tz, jua
1.akili yake kaifungia kwenye sanduku, alipo anatembea yeye tu,.
Hakuna mkoa haya Mambo hayapo
Huwezi kujiona mpaka uambiwe ndiyo maana tulifuta uchifuu
 
We ni mpuuzi sio kawaida yangu jibiza na wapuuzi,unamtisha nani umekaa Mikoa mingi na kuja na matusi hapa mwanaharam mkubwa, Kama ni laana zako za ukoo kaa nazo huko,binfsi sio mtu wa matusi
Kaliwe mbele hamna unachojua mpumbavu kabisa

Kasome hyo report hujui kitu unajua umaskini nenda longido ukaone umaskin usidanganywe na magorofa investment za watu wa juu kabisa wachache
 

Attachments

  • Screenshot_20220904-142845.png
    Screenshot_20220904-142845.png
    94 KB · Views: 7
We unahitaji kwenda kusoma kwa vile mshamba sana wa magorofa kaangalie kilimanjaro magofu kibao ila wananchi wake Wana kipato kizuri na ni WA pili kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja..

Umaskini upi? Life la Tanga lipo chini ambayo watu wanaaffoid ndo maana wanaita Tanga raha kwa mshahara wa laki na nusu unaishi.. unachoshindwa kuelewa hujitambui nn unaongea unasema bodaboda na baiskeli ndo uwezo wao huo ulifikia kaangalie na mkoa Kuna watu hWana hata chakula kabisa

Kule chakula sio shida nenda handeni ukaone mahindi ,vitu Bei chee umekariri kupiga picha kweny magorofa punguza ushamba umaskini haupimwi kiivyo nenda Kilimanjaro hakuna magorofa kaangalie standard ya Maisha ya watu ipo juu kwa mmoja mmoja

Huwezi nidanganya Tanga hata Ukitaja mikoa 20 maskini haipo! Kwa takwimu nnilizo nazo huwezi kuacha shinyanyaz lindi, kagera, mara,mtwara,katavi,singida,tabora,manyara,singida, mwanza,simiyu eti uje kutaja Tanga kuwa na akili timam

Kaliwe mbele hamna unachojua mpumbavu kabisa

Kasome hyo report hujui kitu unajua umaskini nenda longido ukaone umaskin usidanganywe na magorofa investment za watu wa juu kabisa wachache
Wewe jamaa Shamba Sana alikwambia Kama mtu mmoja kipato chake sh 300 KWA siku na mwingine 500 KWA siku basi Hawa wote sio maskini ni nani,? Mnakuja na vipeperushi vya kuokoteza hapa ,
Hiyo ni Mikoa kiwango Cha umaskini akiwezi lingana ila Mikoa maskini ,
Alafu jitu linakuja na matusi alafu eti nimekaa Mikoa kibao,
Sasa nakuonya binafsi sio mtu wa matusi ,Sasa hutaki endelea na matusi upate haki yako live pitia hapa jf , wenda ipo laana ya ukoo inakutafuna , ni swala la kuiongezea
 
kama kuna mikoa imeminywa na serikali ni mikoa ya nyanda za juu kusini, mbeya, iringa, rukwa , songwe, lakini tofauti yenu na mikoa ya huko ni nyinyi kuzidisha ujuaji kuliko kazi, nimekaa na wahaya na nimefika hadi kagera umaskini ni mkubwa sana aisee, ni watu wanaomini sana maisha yanapatikana kupitia shule tu na tatizo linanzia hapo, miaka hii aliyesoma na asiye soma ujanja ni kuwa na akili ya utafutaji nje ya mfumo, hangikieni masoko y bizaa zenu ,
 
Wewe jamaa Shamba Sana alikwambia Kama mtu mmoja kipato chake sh 300 KWA siku na mwingine 500 KWA siku basi Hawa wote sio maskini ni nani,? Mnakuja na vipeperushi vya kuokoteza hapa ,
Hiyo ni Mikoa kiwango Cha umaskini akiwezi lingana ila Mikoa maskini ,
Alafu jitu linakuja na matusi alafu eti nimekaa Mikoa kibao,
Sasa nakuonya binafsi sio mtu wa matusi ,Sasa hutaki endelea na matusi upate haki yako live pitia hapa jf , wenda ipo laana ya ukoo inakutafuna , ni swala la kuiongezea
🤣🤣🤣Acha mkwara tafuta wajinga wenzio ndo uwadanganye sio mbele yangu...kama hujielewi lazima ukumbushwe sio unaropoka Kuna watu kibao tafuta wenzio kuwadangany watuw anafanya research Kuna sehemu watu wanaoga mpaka mkojo wa ng'ombe ndo maisha yao unaongea ebu tembea uone uache kukariri
 
Kwa hiyo nyie wananchi wa Kagera mnajadili miaka Sita wapi mjenge soko na stand?
Mko very serious aisee
Kazi ya kwanza ya Serikali& viongozi wake ni kuwaletea wananchi Maendeleo . Na Hilo ndo Huwa wanaliombea kura! Huo ndio MKATABA WA SERIKALI NA WATU WAKE, SIO MKATABA WA WASOMI NA WATU. WASOMI wanaweza kushirikiana na Serikali ila HAWAWIWI kwa mjibu wa uongozi. Wanasiasa watata sana. Wanafanya agenda ya wasomi kumbe sio. SERIKALI itimize wajibu wake kwa wananchi wake na KUWAOMBA WASOMI kusaidia kwa Kisomo Chao.
 
Tatizo lenu ni ego ! Yaani kila kitu unalaumu serikali.

Kilimanjaro imehujumiwa sana kuliko Kagera, iko mpakani kama Kagera, wana Kahawa kama Kagera tena Kagera wana Ardhi nzuri na kubwa zaidi, wasomi kama Kagera. Sasa tofauti iko wapi ? Ni utamaduni pamoja na kwamba kuna wasomi wengi Kilimanjaro wananchi wa Kilimanjaro wana wathamini zaidi wafanyabiashara kuliko wasomi. Pili Kilimanjaro kuna utamaduni wa harambee za shule, makanisa, na hata barabara za mitaani. Tatu watu wa Kilimanjaro wana wekeza nyumbani kwao na ku lobby ili wapate pesa za maendeleo. Nne Kilimanjaro wamewawezesha wanawake kwenye maendeleo kuanzia biashara hadi kilimo.

Hakuna hujuma mpaka makatibu wa CCM walitoka huko🤔 badala ya kulalamika jiangalieni wenyewe
Yote uliyoandika, la maana ni hilo hasa ambalo hao wa kagera hawana
 
Wahaya wanapenda sifa za kijinga sana. Sifa zao za kijinga ndizo chanzo cha umaskini wao wa kutupwa. Ovyo kabisa nshomile.
 
Ni imani yangu Mikoa mingi inapata viongozi ambao wao ubunifu, burasa katika kutatua kero nyepesi upo chini,
Siku moja nikashangaa katika Mapato eti Dodoma jiji ikawa juu ya Mwanza,!!
Leo Kagera, Ruvuma, Tanga , Tabora, kigoma ,KWA nini ziwe maskini? alafu unalaam Elim za watu,
Chalamila wakati anafundisha moja ya chuo hapo IRINGA, alikua anafundisha kwa KIBENA? maana vingereza hataki, na ni kwanini watoto wake awapeleke kwenye shule za kulipa, lengo siwajue vingereza

Kagera Kama ilivyo Mikoa mingine, vipo vyanzo vingi vya kuongeza mzunguko na Mkoa ukapaa ni swala la kuwa na viongozi wabunifu,
Basi endeleeni na vingereza vyenu na sifa za kijinga. Chalamila kawashauri mfanye kazi, nyie mnatokwa na povu!
 
Fainal hata mfanyeje serikali ndo Ina uwezo kufanya mkoa fulani uwe juuu kwa vile kibongo hatuna matajiri wakubwa wakasimama kuwezesha mikoa, mfano kanda ya ziwa mwanza iwezeshwa kaskazini Arusha na pwani ni dar ,hyo ni plan ya serikali na sasa wanawezesha Dodoma ambapo mnadai wakazi wake ni omba omba ila mtakuja kuona maendeleo mpaka mshangae ..

Ujinga unabaki vichwani kwamba kagera hawaendelei ila wahaya Wana manyumba ya kifaharu sio kosa lao ni mpango wa serikali ... wajinga wengi mmekariri eti uchapa kazi sijui wengin wavivu maendeleo sio kiivyo ndo maana mnakufa maskini eti uchapakazii !!Hkuna sehemu iliyoendelea bila ya sapot ya serikali kama unabisha niambie ukitaka kujua maendeleo y watu binafsi angalia ubora wa makazi na per Capital income kama Kilimanjaro hapo ndo utajua kwamba wanafight hata kagera pia, ila kwa image ya mji mzima na mkoa ni juu ya serikali.

Katika wote naunga mkono hoja. Miji yote watu wanaojigamba kuwa imeendelea(kwa kibongo bongo) imefanywa na Serikali. Bila serikali ni zero. Leo hii Serikali ikiamua Singida kwa mfano liwe jiji itakua na itachangamka. Mfano wa Dodoma,bila msukumo wa Serikali Dodoma haina ubavu wowote kuizid mikoa ya kimkakati kama Iringa tu kwa mfano.
 
Kinachosikitisha ni kwamba kila anayepanda jukwaa kuelezea kinachoitwa umaskini wa Mkoa wa Kagera anakuja na ngonjera za wingi wa maprofesa na ma-PhD holders kutoka mkoani mwetu. Lawama zote zinarundikwa kwa watu hao na Wanakagera kwa jumla.

Huo ndio ukasuku na unafiki wa watawala wetu ambao tumezoea kwa miaka mingi sasa. Watawala wanajifanya kama hawajui chanzo halisi cha kile wanachokiita umasikini uliokithiri mkoani humo. Bila tafakuri yoyote ya "tafiti" zinazodaiwa kufanywa na Serikali, wanakuja tu na porojo za jumlajumla kuhusu "umasikini" huo. Tafiti hizo za kimangumashi hazielezei chanzo cha tatizo la mkoa wa Kagera.

Haziangalii matokeo ya vita vya Kagera na uharibifu wa usalama na miundombinu uliosababishwa na ugomvi wa Serikali na Iddi Amin. Kwamba shughuli za uzalishaji na kiuchumi zilikufa kabisa kutokana na vita hiyo.

Hawaoni kwamba serikali ilikosea (kwa makusudi) kutotangazwa kwa hali ya hatari mkoani humo, kwa maana ya kujenga miundombinu upya na kuwasaidia wanakagera kurudia maisha yao ya kabla ya vita. Hawasemi Serikali ilifunga mpaka na Uganda, hivyo kusitisha shughuli zote za kiuchumi, ambapo soko kuu la mkoa wa Kagera lilikuwa Uganda. Baada ya vita Ukimwi uliotokea Uganda ulimaliza nguvukazi kubwa ya mkoa huo kwa kupuputisha maisha ya maelfu ya nguvukazi wa Kagera.

Wanajifanya hawajui kwamba MV. Bukoba ilizama na kuua mamia ya watu, wengi wao wakiwa Wanakagera. Hapohapo, MV. Victoria "iliharibika" na kufanya Wanakagera kukosa kabisa usafiri wa kuwaunganisha na nchi yao, huku mazao yao ya kiuchumi yakishindwa kusafirishwa kwenda kwenye masoko makubwa ya kibiashara ya hapa nchini kama Mwanza na Dar es Salaam. Serikali haikuona umuhimu wa kuwapa Wanakagera vyombo vingine vya usafiri ili wajimudu kiuchumi.

Ndipo pia ulipoingia "Ugonjwa wa Mnyauko" wa migomba uliopigilia msumari wa mateso na umasikini wa wanakagera. Yapata sasa zaidi ya miaka 15. Je, Serikali ilichukua hatua gani kuwasaidia wakulima wa kilimo cha migomba mkoani Kagera? Hakuna! Wakati huohuo Wanakagera walikatazwa kuuza kahawa yao nchini Uganda ambako walikuwa wanapata bei nzuri kulingana na gharama za uzalishaji. Waliopatikana na uvushaji wa zao hilo waliadhibiwa, ikiwemo vifungo au kufilisiwa, huko kahawa ikilimbikiziwa "tozo" lukuki bila kutilia maanani gharama za wakulima za uzalishaji.

Hiyo ni mifano michache tu ya hujuma ya serikali dhidi ya mkoa wa Kagera kwa miongo mingi sasa. Matokeo yake ni nini, Wananchi wa mkoa wa wa Kagera waliona serikali ilikuwa haiwataki, haiwapendi. Wakasema isiwe taabu, wakaamua kuhamia mikoa nyingine nchini na kuwekeza huko. Je, serikali inajifanya haioni uwekezaji wao mkubwa na uliotukuka katika mikoa mingine nchini, ikiwemo Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha na kwingineko?

Serikali imekuwa ikipiga kelele nyingi eti wahaya wameshindwa kujenga soko na kituo cha mabasi mjini Bukoba, ikijifanya haijui kwamba jukumu hilo ni lake na vyombo vyake, ikiwemo TAMISEMI. Kwani vituo vya mabasi na masoko ya Dodoma, Morogoro, Dar Es Salaam, Mwanza na kwingineko vimejengwa na nani kama sio Serikali? Nimalizie kwa kuishauri Serikali kwamba iwekeze mkoani Kagera kama ambavyo imekuwa ikiwekeza sehemu nyingine nchini.

Ikiwekeza Kagera, kama ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kufanya kwa kujenga kitengo cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), mkoani humo, basi itarajie kwamba maprofesa na PhD holders kutoka mkoani Kagera watarudi nyumbani kufaidi fursa za uwekezaji wa serikali. Ni matumaini ya wengi mkoani Kagera kwamba Mkuu mpya wa mkoa wa Kagera, Mhe. Chalamila ataelewa chanzo cha "umasikini wa mkoa wa Kagera."
Changamoto zifuatazo, zinafanya Kagera tuwe nyuma. Tuache visingizio.

1. Ardhi ni ndogo
Kupata mkulima mwenye acre 2 au zaidi ni shida. Maeneo mengi yaliyotumika na jamii kwa kuchungia, kulima nafaka kama karanga n.k. yalichukuliwa na watu wachache wakapanda miti ya mbao, na kuacha watu wengi wakabaki wanahangaika.

2. Utamaduni wa kilimo cha migomba.
Migomba ni utamaduni wa Mhaya. Migomba hii haizalishi tena kwa wingi. Mashamba mengi ni yamechoja. Siyo rahisi kuwashauri watu kung'oa na kupanda mazao yenye tija. Hii ni crop rotation ambayo ingesaidia kurudisha rutuba na kutokomeza mnyauko.

3. Matumizi ya mbolea
Watu wengi wanaamini kwamba, mbolea inaharibu ardhi. Kwa hiyo, mapinduzi ya kilimo kwa kutumia ardhi iliyochoka ni ngumu.

4. Kaitu kaila
Acceptance ya aina mpya ya mazao ni ngumu. Tukubaliane, Mhaya anapenda sana migomba.

Pia, Takwimu zinaonyesha Kagera unaoongoza uzalishaji wa maharage kitaifa. Tatizo kubwa ni kwamba hawalengi soko. Maharage yanalimwa kwa wingi, lakini ni local na mchanganyiko. Yaani kila variety kidogo kidogo kiasi kwamba ukiyachambua na kukusanya, kiasi kinachopatikana hakikidhi soko individually.

5. Vijana na akina baba kutoshiriki kilimo
Mathalani, vijana wengi wilaya ya Missenyi hasa Kiziba na Kibumbilo, wamejikita sana kwenye kunywa karadarugo ambayo ni starehe ya vijana wengi. Hii inua nguvukazi.

Fursa za masoko

Masoko siyo shida. Kuna kipindi nimeshuhudia mihogo inatoka Lindi na Kigoma kupita Mutukula kwenda South Sudan. Vivyo hivyo, maharage na mahindi kutoka Rukwa na Mbeya. Halafu, wakati wa vita ya Rwanda, Kulikuwa na soko kubwa la WFP. Waliofaidi ni watu wa mbali.

Kuna mashule ya bweni pamoja na majeshini. Maharage yanayotumika huko ni ROZIKOKO. Soko siyo shida.

Kwa hiyo, swala la Stendi au Soko Kuu, havitaongeza chochote kwenye mfuko wa mwananchi. Vitabadili mandhari tu na kuongeza mapato ya serikali. Ni sawa na kuvaa suti huku una njaa.

Ili kubadili wananchi, inatakiwa nguvu kiasi, hasa ya kisiasa. RC ameanza vizuri japo tunataka zaidi action.

Nashauri kampeni kubwa iwe ni kubadili mindset za watu. Mfano, badala ya radio nyingi(Kasibante, Fadeco n.k) kushinda wanajadili mpira na miiziki, wajikite kutoa elimu ya kilimo na uchumi muda mwingi.

Ianzishwe TV station ya Kagera. Hii itakuwa na muda mwingi wa kutoa elimu kwa vitendo. Mpaka sasa kuna watu hawajui hata namna ya kupanda mahindi na maharage kitaalamu!. Watu hawajui kama kuna aina mpya za migomba na kahawa inayogawiwa bure.

Nashauri vikundi vya kilimo, vilivyo na uwezo wa kuunganisha wakulima pamoja, kama kule Kenyana Kilimilile, vipewe elimu na misaada ili kuleta chachu kwa wakulima wengine.

Nashauri pia, Maafisa ugani wapewe mafunzo ambayo ni 'tailor made' kwa ajili ya kupeleka elimu sahihi kwa wakulima.

Inawezekana. Hapo chini ni shamba la maharage katika kijiji cha Kenyana, 2021
FB_IMG_1662286507841.jpg
 
Haya Sasa. Huyo ni kiongozi na kaonyesha wazi chuki dhidi ya wahaya. Pia naona michango mingi unakuja against wahaya. Sasa wahaya tafuteni jinsi ya kubadilisha majina yenu. Msitegemee kupata ajira na kushinda interview kama watu wenyewe ndo hao. Kazi kwenu akina Mutashobya, Mwijage, Karugendo nk
 
Mkuu tatizo mnadanganywa na tafiti za Twaweza, wenda mnazungumzia tu kipi kinapatikana kule katika changia kwenye mfuko wa serikali kuu, kisa hivyo viwanda vichache vinavyofanya kazi

Maana vingi ni maghofu,

Pili utazungumzia labda kilimo Cha mkonge ambacho nacho kinasuasua, mashamba yale yaliyokua yakiajili watu wengi mengi yamebaki Kama sanam,ila wachache pitia hatimiliki walishachukulia mamikopo wanakula KWA urefu wa kamba zao,

Utazungumzia kilimo Cha machungwa, ambapo wengi wenye mashamba pale sio wazawa ni Wakinga, wazawa walisha uza

Bandari pia utaizungumzia lakin je imeajiri watu wanagapi?

Pale katika uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja ni wakimaskini wa kutupa,ndo maana linaitwa jiji ila bodaboda za baiskeli ni Kama zote,

Sasa niambie nyie kipimo Cha umaskini katika mkoa mnaangalia kile mkoa inachangia katika mfuko wa serikali kuu au pato kwa mwananchi mmojammoja

Hoja ya Wazawa kwa maana ya kuwekeza haina mashiko. Kila mkoa upambane kuleta ushawishi wa wawekezaji haijalishi ni wwzawa au Mtanzania yeyote. Dar kwani ni wazaeama
 
Back
Top Bottom