Serikali imeanza kuingiza udini katika sera zake? Suala la masomo ya kiislamu na Divinity yanatoka wapi?

Mbona mnaweweseka na kubwata bila kutoa maelezo kamili? Weka hapa syllabus ya hilo somo au toa maelezo zaidi.

Kama suala ni Islamic finance, hili ni somo la kimataifa sasa pengi duniani kwenye nchi zisizo za kiislamu linatolewa.
 
Mkenda mpuuzi sana. Halafu wakishasoma hayo masomo wanaenda kuwa nani huko mitaani????
 
Sasa kama soko la iko kinachofundishwa lipo kunashida gan
Hizo taasisi za kidini si zina shule zake zina vyuo vyake humo hao wanaoitaka hiyo michepuo waende wakaisome huko siyo kuichanganya kwenye government.

Kingine hata kama soko lipo ni kujidanganya kwamba wa upande ule atawekwa humu wa upande huu atawekwa kule.
 
Siyo kweli, mayai ya MKIRU(Mkuranga, Kibiti, Rufiji) yalitagwa wakati wake.
Mwendazake ndiye aliyasafisha.
Watu tunasahau haraka.
Hii thread inaenda kuwagawa watu hapa jukwaani sasa hivi !!
Hivi huwa mnaanzisha makusudi ili kuhamisha magoli ??!
😂😂😂 kwakweli muko wajanja bandugu ! 😅😅😅
Duh 🙄 !
 
Safari ni ndefu kweli. Kwamba elimu ya nchi haimhusu kila mtu????
umelazimishwa kusom hayo masomo? au shobo

Tahsusi kibao kasome , nyingine hazikuhusu laiti kama ungekuwa na akili ungetaka tahsusi fulani iongezwe .
 
Habari Mkuu!
Nakubaliana na wewe kwamba Divinity na Islamic Religion zimekuwa zikisomwa Kwa muda mrefu sana katika Secondary na hata Advance..

Serkali haikuwahi kujihusisha na Elimu Hizo hapo kabla!

Sijui kama Unafahamu hilo?

Hakukuwahi kuwepo kwa Walimu Wa Dini waliokuwa wanalipwa na Serikali!.
Masomo hayo yalikuwa yakifanyika kama masomo ya Ziada tu..

Kitendo cha Kuanzisha Tahsusi Za masomo hayo Kinailazimisha Serkali iajiri waalimu wa Masomo hayo kitu ambacho ni kinyume Cha katiba ya Nchi ibara ya 19..

Ambayo imeitaka serkali kutohusika na Uenezwaji au shughuli za Kidini Nchini..

Sijui kama umenielewa?
 
Watanzania wapo kwa ajiri ya kupiga kura tena ya Ccm, baada ya hapo hkn anayepoteza muda kuwafikiria
 
Niseme tu kuwa,aliyeko juu na anayesema hiki kibinafsishwe na kile kiwe hivi ndo TATIZO la msingi katika nchi hii.

CCM haina mawazo,hawezi kuongoza,kila kiongozi amebaki kuwa mlalamishi; hawawezi kuchukua hatua yoyote kwa lolote zaidi tu wanaloweza kukomba fedha,wizi na kutesa watu.

Imagine,wanashindwa kuiendesha hadi mradi wa mwendo kasi uliopo Dar tu. Hiyo elimu ya nchi nzima wataiendeshaje?

TATIZO NI NGOME YA jengo jeupe...hakuna kitu.
 
umelazimishwa kusom hayo masomo? au shobo

Tahsusi kibao kasome , nyingine hazikuhusu laiti kama ungekuwa na akili ungetaka tahsusi fulani iongezwe .
Una watoto? Ndugu jamaa na marafiki?
 
Asante mkuu kwa kuliweka wazi.
Mara utasikia ....Takbir!!!! .......na unapata maandamano ya waalimu masheikh wanaotaka kuongezewa mishahara.
Wenzetu hawakawii kuwa na munkari.
Tupunguze au kuepuka direct conflict kati ya dini na serikali
 
Tena itapendeza sana, islamic na lugha adhiim ya kiarabu ziwemo, na ukizingatia idadi kubwa ya waislamu nchini. Ni hayo tu
 
Kwa kuona mbali, kutaanza kuwa na ajira za kidini dini kutokana na masomo ya kidini.
Tunaanza kutaga mayai ya machafuko huko mbele ya safari.

Hili lipingwe kwa nguvu zote.
Machafuko yanakuja dini moja kujiona wanamiliki kila kitu na wengine hawana nafasi. Chemistry uliosoma form umetengeneza acid gani? Si umejibia mtihani tu?
 
Tatizo limeanza kwa mtoa masa mwenyewe;

kiislam vs Divinity...............kuna maana kubwa hapo ya kiubaguzi (kwa mwenye akili)
 
Swala linaloongelewa ni kuchanganya Serkali na Imani za kidini mkuu inapswa Vingine Uvielewe..
Hupaswi kukaza Shingo..

Serkali haipaswi Kuongeza nguvu katika Kueneza Dini kwa Njia yoyote ile Ni kinyume cha Katiba..
View attachment 2940739

Mtaendelea kuupiga vita sana uislamu, ila kila kukicha watu wanatoka kwenye kiza na kuifuata nuru. Kuweni wapole tu

Aleyommba gekke bhabhaa, kuweni wapole! Nimemaliza
 
Tatizo limeanza kwa mtoa masa mwenyewe;

kiislam vs Divinity...............kuna maana kubwa hapo ya kiubaguzi (kwa mwenye akili)
Elewa mada, ni Kiislamu AND Divinity, havina nafasi kwenye sera rasmi za elimu kiserikali.
Hizo wanaachiwa wenyewe wenye dini zao.
 
Vita labda muanzishe ninyi kama kawaida yenu, ila Uislamu haujatufundisha hivyo
Umejuaje kama nipo upande wa Uislamu au Ukristo?
Hakuna mahali nimeusema Vbaya uislmu...

Na kwa maelezo yangu umegundua kama mimi ni muislamu au mkristo??

Punguza mihemko Na munkari haisaidiii..
Nilichokionyesha ni Katika Hoja inayotokana na Katiba ya Taifa..
 
Elewa mada, ni Kiislamu AND Divinity, havina nafasi kwenye sera rasmi za elimu kiserikali.
Hizo wanaachiwa wenyewe wenye dini zao.
Pia mkumbushe kwamba Elimu ya Dini ya kiislamu (Islamic knowledge) ni soma na wala sio Ubaguzi..

VIvyo hivyo Elimu ya Dini ya Kikristo Huitwa (Divinity) ni somo sio ubaguzi..

Mbona sioni Wakristo wakilalamika kuhusu Hili Au ni kwamba Waislamu Wenyewe ni watoto special kuliko wengine??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…