Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Naandika kwa ushahidi wa kutosha na kwa kuishi maeneo hayo na kwa hapa Dar kuna kundi kubwa sana la wadada wa kizaramo,wakwere na wadengereko wanao OKOKA na kuolewa na vijana wa kikristo

Nimehudhuria harusi kama 14 ndani ya mwaka huu ambapo mabinti wa kiislam wanabadili dini na kuwa wakristo ili kuoleka

Leo ukienda kwenye Makanisa mengi hasa haya ya kinabii,utakuta kuna Wamama wengi sana wa kiislam wameokoka
Hivi unajielewa kweli?

Hapa unajadili nini sasa? naona unaendeleaza zile zile za kusema Nahisi

Umeielewa mada lakini?
 
Nimeona tangazo la Dr. Zakir Naik anayetafutwa kufikishwa mahakamani na mamlaka za nchi yake ya India tangu mwaka 2016 kwa makosa ya ugaidi, utakatishaji fedha na kauli za chuki kuwa nchini wiki ijayo kwa shughuli za kidini.

Hili jambo tumepima kama halitatuleta shida zinazoepukika na utata usio wa lazima na India ambao ni marafiki zetu wakubwa na washirika muhimu wa kibiashara na maendeleo?

View attachment 3187483
Keshatua Bongo, atafanya kazi yake ataondoka na nyie bakini na mikelele yenu ila HAMNA CHA KUMFANYA ZAIDI YA KUUMIA ROHO ZENU TU
 
Asante kwa matusi. Hebu kanusha kuwa Boko Haram (waislam) hawachinji WAKRISTO na kubaka wanawake Nigeria na kwingineko. Nihakikishie mimi mkristo naweza kupata kibali Uarabuni kumhuburi Mohamed vibaya na kumuinua Yesu. Nihakikishie kama naweza kufungua Kanisa Somalia sawa na wewe unavyoweza kuanzisha msikiti hapa. Hapo kati yetu nani ana chuki ?
Wewe jamaa ni mjinga sana,

Kwanza unaweza kuyaonyesha hayo matusi?

Jikite kwenye mada,jadili mada,hatujadili Nigeria hapa,fungua uzi wako kuhusu hayo,tutakuja kujadili,jikite kwenye mada,acha kutafuta pakutokea,usihamishe magoli.
 
Asante kwa matusi. Hebu kanusha kuwa Boko Haram (waislam) hawachinji WAKRISTO na kubaka wanawake Nigeria na kwingineko. Nihakikishie mimi mkristo naweza kupata kibali Uarabuni kumhuburi Mohamed vibaya na kumuinua Yesu. Nihakikishie kama naweza kufungua Kanisa Somalia sawa na wewe unavyoweza kuanzisha msikiti hapa. Hapo kati yetu nani ana chuki ?
Kwani tanzania nchi ya kikristo?..hivi nyie vichwani huwa mna ubongo au kamasi?.. Somalia hakuna wakristu?.. arabuni hakuna wakristu?..antibalaka siyo wakristu?.. angola hawakubomoa misikiti?..ufaransa hawapigi marufuku hijab?
 
Nioneshe neno lolote linalo onesha huyu muhubili akihamasisha vurugu dhidi ya dini nyingine.
20241229_103337.jpg
 
Members wa hili jukwaa sio Wakristo na Waislamu tu, kuna Atheists na waumini wa dini za kienyeji pia.
Umewahi kulijua hili??
Waanzisha mijadala ya kashifa na kejeli dhidi ya waisilam humu, huwa wanaanzisha mijadala kwa misingi ya kilinganisha kati ya uisilam na ukristo.
 
Waanzisha mijadala ya kashifa na kejeli dhidi ya waisilam humu, huwa wanaanzisha mijadala kwa misingi ya kilinganisha kati ya uisilam na ukristo.
Kwani atheist hawezi kufanya hivyo??
Hujawahi kuona watu wasio na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi wanaichagua CCM au CHADEMA??
 
Waislam wakifanya mkutano wakapata majanga wenyewe au WAKRISTO wakifanya mikutano wakafa huko sioni walivyoingilia Imani ya mwingine. Shida ni pale mkristo atakapoandaa mkutano mahususi kuwasema waislam je, anaweza kufanya hivyo Uarabuni ? Kama NJ I tatizo au haiwezekani mkristo kufanya mikutano huru kwa uislam mbona iwe ruhusa na rahisi kwa muislam kuandaa mkutano wa kukashifu ukristo na kulindwa na serikali ? Huko Nigeria hamjasikia chuki iliyopondwa na Boko Haram wanavyochinja WAKRISTO kama kuku na kuteka wanawake na kuwabaka kama mateka wa ngono ?
Anaye enda kujadiliwa ni yesu na sio wakristo , wakristo hawana hati miliki ya yesu mpaka useme kuwa waisilam hawana ruhusa ya kujadili yesu.
Yesu ana tambulika kama nabii ndani ya uisilam
 
Asante kwa matusi. Hebu kanusha kuwa Boko Haram (waislam) hawachinji WAKRISTO na kubaka wanawake Nigeria na kwingineko. Nihakikishie mimi mkristo naweza kupata kibali Uarabuni kumhuburi Mohamed vibaya na kumuinua Yesu. Nihakikishie kama naweza kufungua Kanisa Somalia sawa na wewe unavyoweza kuanzisha msikit hapa. Hapo kati yetu nani ana chuki ?
Waathirika wakubwa wa matendo ya boko haramu ni waisilam hata wale wanafunzi wa choboko waliotekwa %70 ya wanafunzi hao walikuwa waisilam.
 
Anaye enda kujadiliwa ni yesu na sio wakristo , wakristo hawana hati miliki ya yesu mpaka useme kuwa waisilam hawana ruhusa ya kujadili yesu.
Yesu ana tambulika kama nabii ndani ya uisilam
Kama Yesu ni WA wote na Mohamed ni mtume wa wote msikasirike au kukereka akihubiriwa na kuchambuliwa msiamzishe jazba na vurugu. Quran iko wazi na tunayo.
 
Nikubalieni na mimi niandae mafundisho dhidi ya dini zingine/uislam uwanja wa Mkapa.
Yeye hatukanini dini nyingine. Waislamu pia wanaomwamini Yesu ni mtumishi wa Mungu/mtume wa Mungu. Hivyo si shida kumuweka hapa. Tatizo wengi wetu tunaogopa uislamu na kuuwazia mabaya. Dini hiyo ni ibrahamic religion. Ni mpango wa Mungu kama ilivyo kwa uyahudi na ukristo. Hakuna awezaye kuifuta au kuipunguza. Usipambane na kitu ambacho utakufa na utakircha kikiendelea kustawi. Uislrmu hsuhubiri chuki, achilia mbali waislamu wachache wakihubiri chuki, ni wao na siyo imani nzima.
 
Sasa walimletaje wakat wanaijua background yake
 
Mi nadhani, na kwa maoni yangu... Huyu muhubiri kuja ni sawa na haki kabisa, maana kila dini inahitaji kulishwa zaidi neno inaloliamini. Na Tanzania dini kuu ni mbili, so uislam na waislam wana haki ya kumsikiliza mfuasi wao anasema nini... Changamoto kubwa na mzozo ulipo ni aina ya mada anazotarajiwa kuzitoa (soma bango) ikiwemo hiyo ya JESUS (pbuh) na MUHAMMED (saw). Hiyo ni kutengeneza chuki ya wazi au kuchochea mabishano na mgogoro wa kiimani na kidini (kama unaoendelea hapa) usiokua wa lazima. Nadhani kama angeandika tu heading kwamba mada kuu ni kuhusu Mtume MUHAMMAD (saw), let say na maisha yake duniani, sidhani kama kungekua na tension ya namna hii.

Na mamlaka kuruhusu "heading" ya namna hii ni mapungufu makubwa, nikiamini mamlaka inajua madhara ya midahalo au mahubiri ya mtu wa Imani moja kuzungumzia imani nyingine. Ni wazi haitakua kwa kusifia bali kuponda. Refer kipindi cha kina Sheikh Mponda na mihadhara ya pale Kinondoni biafra (nadhani) enzi hizo, na pale msikiti wa mtambani. So yale matatizo ndio yanaanza kujijenga taratibu taratibu. Mbaya zaidi mwakani tunaingia kwenye uchaguzi, tusipozuia haya mapema, basi yamkini determinant ya uchaguzi ikawa mambo haya ya udini.


So tuwaombee busara viongozi wetu walione hili kwa jicho la karibu na wafanye maamuzi sahihi kwa faida na mustakabali wa taifa letu.

Ni hayo tu!
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom