Mi nadhani, na kwa maoni yangu... Huyu muhubiri kuja ni sawa na haki kabisa, maana kila dini inahitaji kulishwa zaidi neno inaloliamini. Na Tanzania dini kuu ni mbili, so uislam na waislam wana haki ya kumsikiliza mfuasi wao anasema nini... Changamoto kubwa na mzozo ulipo ni aina ya mada anazotarajiwa kuzitoa (soma bango) ikiwemo hiyo ya JESUS (pbuh) na MUHAMMED (saw). Hiyo ni kutengeneza chuki ya wazi au kuchochea mabishano na mgogoro wa kiimani na kidini (kama unaoendelea hapa) usiokua wa lazima. Nadhani kama angeandika tu heading kwamba mada kuu ni kuhusu Mtume MUHAMMAD (saw), let say na maisha yake duniani, sidhani kama kungekua na tension ya namna hii.
Na mamlaka kuruhusu "heading" ya namna hii ni mapungufu makubwa, nikiamini mamlaka inajua madhara ya midahalo au mahubiri ya mtu wa Imani moja kuzungumzia imani nyingine. Ni wazi haitakua kwa kusifia bali kuponda. Refer kipindi cha kina Sheikh Mponda na mihadhara ya pale Kinondoni biafra (nadhani) enzi hizo, na pale msikiti wa mtambani. So yale matatizo ndio yanaanza kujijenga taratibu taratibu. Mbaya zaidi mwakani tunaingia kwenye uchaguzi, tusipozuia haya mapema, basi yamkini determinant ya uchaguzi ikawa mambo haya ya udini.
So tuwaombee busara viongozi wetu walione hili kwa jicho la karibu na wafanye maamuzi sahihi kwa faida na mustakabali wa taifa letu.
Ni hayo tu!