KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mama anaupiga mwingi na hakuna kitu mtafanya.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hii serikali katili sana. Wanachukua hela kuwahonga akina Msigwa.
Mkuu, amekwenda mwenyewe baada ya kushindwa Uwenyekiti wa jimbo la Nyasa, hii ni aibu sana, angekuwa anaunga mkono maboresho na ufanisi ya kiutendaji ndani ya Serikali basi angejiunga kitambo sana na sio baada ya kukosa uwenyekiti.
 
Kwa sasa makato ya kodi unaponunua LUKU yameongezeka kutoka TZS 1,000 mpaka TZS 2,000.

Tunaomba maelezo kwanini gharama hizi zineongezeka? Kuna sababu gani ya kuendelea kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu ili hali mabwawa ya umeme yaliyotumia matrilioni ya kodi za wananchi yameshafunguliwa?

Je, kodi wanazotozwa wananchi bado hazitoshi? Je, mmeshindwa kutumia rasilimali zilizopo nchini, kuna madini, maliasili na vivutio mbalimbali vya utalii n.k pamoja na vyanzo hivi vya mapato, serikali imeshindwa kuwa bunifu na kutegemea tozo na kuendelea kunyonya na kufanya maisha ya watanzania yazidi kuwa magumu?

Hali hii itaendelea mpaka lini?

View attachment 3030797
Julai 1 hii Bwashee, check pengine unadaiwa mwezi uliopita wa Juni
 
Wakuu habarini za jioni,
Naomba kuuliza mnieleweshe ni kwamba ile kodi ya pango inayotozwa kwenye umeme imeongezeka au nini kimetokea

Nimezoea nikinunua umeme mwanzo wa mwezi nakatwa 1500 nashangaa leo nimekatwa 2000

Je kuna mtu amekutana na hii leo au ni mimi tu au ndo tushaongezewa tozo tayari kimya kimya

IMG_2708.jpeg
 
🤣🤣🤣🤣
Uzi huu tayari dada..
 
Back
Top Bottom