Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!

Mkuu kuna watu wanalipwa kutetea dhuluma, Na wengine bila kujua wanaingizwa mkenge kutetea mhalifu
 
Chukulia wewe una eneo lako Halafu aje mvamizi ajenge au anuuzie mtu mwingine wewe utajisikiaje?
Huyo mmiliki AsiΔ™ halali ajenge akibomolewa utasema kaonewa?
Hapana tuache unafiki.
Tujenge misingi ya jamii bora yenye kuheshimu haki na sheria .
Usiseme hivo boss, haitafit narrative zao, wao wanataka waziri aonekane mwenye kosa,
Wanamtuhumu bila hata kuwa na uhakika ile amri kuvunja kaitoa waziri au mahakama?
 
Mkuu chankende ya Biharamulo amaπŸ˜….
Umeongea fact,ila ndo siasa za ccm mkuu.
Madalali ndo wanachangia migogoro ya ardhi na nyumba Kwa 90%.

Japo Mahakama nazo zinatuhumiwa kuwasikiliza wenye nazo.

Kiufupi huwezi kutatua migogoro Kwa staili kama ile,ni ujinga kiwango Cha PhD.

Acha yawapate,maana wote wale ni wanachama wao🀣🀣🀣🀣.
Hatuna,Bunge bali tuna Jengo.Hatuna viongozi bali tuna wapenda sifa.
Siku hizi,mtu kuitwa wazuri hana matiki Wala heshma kama awamu 3zilizopita.

Wazuri wa Sasa,hana tofauti na wazuri katika Serikali ya wanafunzi vyuoni.
 
Mbona kama muanzisha uzi anamtetea mhalifu, au mleta uzi ndiye aliebomolewa au ana undugu na aliebomolewa kwa kujenga eneo alilovamia, amini amini nawaambia hakuna sekta imejaa dhuluma kama ardhi, wacha waziri afanye kazi yake Wananchi wanyonge wapate haki zao, Mh. Waziri sisi Wananchi tupo na wewe chapa kazi ondoa hao madhulumati na waporaji wa ardhi za watu, yeyote anayemtetea mvamizi kuna namna ana maslahi naye hivyo hatushangai kuona watakaokupinga ila yaliotukuta tunajua muhimu wa kazi yako, Mungu akupe nguvu Mh. Waziri Mungu akubariki
 
Niliposoma eti yeye ndio Hakimu nikayakumbuka maneno ya Katibu mwenezi wake aliesema msiende Mahakamani

Naona na yeye kashikilia pale pale kama kiongozi wake alivyosema
Ila watajuana maana kila mmoja ana sheria zake kama serikali nyumba zao
 
Chukulia wewe una eneo lako Halafu aje mvamizi ajenge au anuuzie mtu mwingine wewe utajisikiaje?
Huyo mmiliki AsiΔ™ halali ajenge akibomolewa utasema kaonewa?
Hapana tuache unafiki.
Tujenge misingi ya jamii bora yenye kuheshimu haki na sheria .
Mtu anapojenga anakua tayari ana building permit ili BT lazima uwe na hati, Sasa mpaka watu wa Halmashauri wanatoa kibali Cha ujenzi ni kosa la nani
 
Kwa maeneo yaliyopimwa haizidi laki 3 kaka, hati tayari
 
Yaan huyu jamaa hiyo Wizara haimfai kabisa, sijui kwann walimtoa Mabula ila kwangu mimi aliitendea haki sana
Mabula alikuwa ni mbwa asiye na meno.
Labda kwa kujiuliza kama unavyojiuliza, ungeliuliza: 'kwanini walimtoa Lukuvi'?
 
Anajitahidi kutenda kwa haki.

Vibaya kumuonea mtu lakini tabia ya kuvamia maeneo ya watu na janja janja kisha kujenga Halafu utake huruma wakati umedhurumu haki ya mtu mwingine haikubaliki.
Baada ya kusikia vzuri story... Na mimi nimeona amefanya sawa mwenye kiwanja ilipaswa ndo azungumze na yule mama kabla ya kupata kilichompata
 
Vizuri umeweka huu ushahidi, sasa Waziri ana weza waomba Takukuru, wakafanya kazi yao, wakamfungulia kesi ya uvamizi wa eneo na ya rushwa pia
 
Kaka tunawatu wajinga sana kwa kutetea upuuuz
Uwepo wa watu kama Mahululu ni matokeo ya mfumo mbovu wa idara ya ardhi na maofisa wake na kukosekana kwa uwajibikaji
Takukuru ingebidi wawe wamehusika hapa
Na haki ya hawa raia ipatikane maofisa ardhi ni kiungo muhimu kwa Mahululu kufika hapo alipo
Lakini namna ambavyo Slaa anadeal na haya mambo ni lini atamaliza mamia ya maelfu ya migogoro na uonevu uliopo kwa wananchi kwenye eneo la ardhi
Ni wazi kwamba hawezi kumaliza na anachofanya ni kwamba inawezekana kabisa kuna uhusiano fulani wa karibu na hao victims ambao ameamua kuwapambania
Kwa sababu kwa njia anayotumia hawezi kufika popote katika kutatua migogoro ya ardhi iliyopo nchini, jambo analofanya lingemfaa afisa ardhi wa kata lakini siyo kwa waziri ambaye inabidi pia aende kigoma,Rukwa na mikoa mingine unayoweza kuitaja akafanye the same ya kile anachofanya sasa hivi ni jambo ambalo haliwezekani
 
Ndugu yangu, hizo mahakama zenu za kina, kibatara, na madereke na mahakimu na majaji wao zimekuwa za kitapeli, uongo, rushwa. Haki za, watu zimepotea, sana. Nampongeza sana wazir Slaa kusimamia haki. Nina kiwanja changu toka mwaka 1970. Nina hati zangu. Mnaenda kwa maafisa wa, ardhi, mnawaonga. Mnabadilisha hati. Mnawadhulumu watu, kwa kupitia hizo mahakama zenu feki. Na ww unakuja hapa kuongea, uongo. Nafikiri ili tuishi kwa amani, hiz sheria, mahakimu na majaji wapitiwe upya, ili haki ipatikane. IPO siku haki itapatikana kwa njia ya, siraha.
 
Hapana kama alivamia kiwanja ni sahihi kubomolewa kabisa. Na nikuambie tu uvamizi wa kiwanja usikie tu na usikupate Ndugu yangu
 
Ni waziri wa ardhi.
Alichofanya ni sahihi.
Mkuu najua wewe ni mtu wa details. Hebu tupe snapshot ya kilichotokea. Kwangu mimi waziri kama kiongozi mkubwa wa serikaki ni muhimu kufuata sheria. Inawezekana mahakama zetu zina mapungufu mengi. Lakini ndo chombo tulichonacho.
Tukiamua kuignore maamuzi ya mahakama, it will be anarchy.
 
Halafu hizi taratibu za kuvunja, si ustaarabu na ni kinyume cha ubinadamu. Pakiwa na mgogoro, thamani ya uwekezaji/uendelezaji haionekani bali pande la ardhi tu! Na kitendo cha Waziri kusimamia zoezi, kimeshusha kiwango chake cha uwajibikaji..!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…