DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
He is mentally sick
Soon atapata tukio la aibu kwa staili hyo
Mkuu, Hilo Ni la Uhakika kama hatabadilika na kukubaliana na matokeo. Ajue na Atambue kwamba Amestaafu i.e. Hayuko Ofisini tena na pia Yeye sio IGP tena bali ni Raia sawa na raia wengine. Huko kumiliki gari na bastola na vitu vingine kama anavyo ajue kwamba hata raia wengine wanavyo vitu hivyo pengine hata kumzidi.
Hivi inakuwaje kwa huyo mwamba - anakwama wapi? haangalii hata Rais mstaafu Mh. J. Kikwete anavyoishi na Jamii ? CDF mtaafu anavyoishi na Jamii??? anadhani hivyo vitu (gari na bastola)anavyotamba navyo wao hawana? Mbona wametulia?
 
T

Tujaribu kuwa wakweli mwembechai mtu anakuja na panga au shoka yupo mbio anakuja kukudhuru..wewe una gun..utafanyaje...??
unarusiwa kujiham ila sheria yavsirah inakataz kua kitisho wa jamii kidgo umeonyesha kidgo umetoa umeona kwa malalamiko tu uyo mshua angekua raia wa kawaid washamnyang'anya ktambo sema tu vle alikua na wadhifa then sheria ya kujiham ipo pia sio uue tu kisa mtu kakutolea panga unakaa jela km kawaid shelia ya kujiham ni kupga juu mweny panga awez skia risas asitupe panga aje akmbie aje akudhur tu na kiwang cha mwish kabs kupga miguu sio kuua na ukimpga nyuma ni kosa yan kuna sheria kal km unavoona trafk wanapma ajal na sirah ivo ivo kuna wachunguz pk waon umetumia sirah kmakosa au laa
 
Huyu jamaa bado anadhani bado ni IGP.hata wakati yupo madarakani alikuwa na tabia ya hovyo sana na hakupaswa kumilikishwa silaha.hii nchi ya hovyo sana ni kama vile hatuna serikali na wakati jpm alikuwa mpole sana ila sasa wanachezea sana mama
 
Kwa nchi zetu hizi za kujuana sana.

Kufunga lock gari ya IGP mstaafu ni kujitafutia matatizo tu. Huyo mfunga lock ni mpumbavu pia.

IGP mstafu huwezi kwenda kumshitaki popote ukamshinda.
Kama hakuijua mkuu inakuwaje? Japo una point, kwanza kituo utachoenda kushitaki wanaweza kukugeuka umemdharau afande.
 
Kwani yeye yuko juu ya sheria au!
 
Tatizo ni kwa Serikali inaweza kupewa Dokezo kama hili, halafu ikakaa kimya halafu likitokea la kutokea ndo Wanaamka - lakini maji yanakuwa yameshamwagika.
 
Inaonekana kijana aliwaaminisha wenzake ngoja kwa niifunge gari ya mahita ... Nyie sini mnamuogopa.😁 Arafu kijana mwenyewe ni huyu huyu muanzisha mada hii..

Halafu makosa mengi kama hayo ya kufunga gari unakuta hata vile vibango vya Katazo havipo au kukiwepo kimeanzishwa makusudi ili usikione au kimewekwa mazingira ambayo si rahisi kukiona

Sababu wanajua kabisa watakosa hela..


Labda kwa taarifa kijana ambazo hazijui Omar mahita ni mtu hatari sana na aina ya wafu wenye misimamo mikali sana enzi zake za utumishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…