Mimi nilikuwa pale muhimbili hospital, nikiwa natoa gari bahati mbaya nikagusa gari lingine kwa nyuma, wale walinzi suma jkt wakaizingira gari yangu. Hapo nilipoigusa hiyo gari mwenyewe hata ukimuonesha hawez kupaona. Wakasema hii gari ni ya generali wa jeshi huwezi kutoka mpaka afike hapa uelewane nae, kipindi tunaendelea na mjadala ghafla nashtukia gari ishatiwa lock na mlinzi mwingine.
Nikiwaambia nionesheni huyo jenerali alipoelekea nikaongee nae, wanasema hawawezi kufanya hivyo mie nisubiri mpaka atoke. Mara naambiwa huyo jenerali ni daktari pia kitengo cha wagonjwa wa dharura.
Hapo nipo na mzee wangu ambae nilimleta hospital akitokea kigoma. Namcheki mzee anatetemeka kusikia jenerali, nadhani alikuwa anawaza vita ya kagera na iddi amini😀😀😀
Dakika chache akaja MP wa jeshi akauliza kuna nini hapo na mbona mmezingira gari ya mzee (akimaanisha hiyo gari ya mkuu wake) nikashuka nikamsalimia salamu ya kawaida tu, habari yako kiongozi, imetokea bahati mbaya wakati natoka nimeigusa gari ya mkuu kidogo sana hapa (huku namuonesha sehemu nyingine) jamaa akasema mbona padogo saana, hata mzee hawez kupaona, mimi mwenyewe sijaona shida iliyopo..
Jamaa akaagiza lock zifunguliwe then niruhusiwe niondoke, suma wakafanya hivyo naondoka ety wakanizuia tena kuona yule MP kaondoka, ety ooh mzee akija akigundua atatumaindi sie, tuachie chochote tumpange mzee akitoka. Nikacheka saaaanaaaaaaaaa 😀😀😀😀😀😀
Mlipaswa muongee hivyo mapema kabla yule MP hajairuhusu gari yangu na nyie kukubali. Nitaenda kumwambie yule bwana mnaniomba rushwa...daah jamaa waligeuka nyuma bila kuuliza kitu.