DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Walishawahi kufunga gari(ya kazini) nikamwambia dereva piga jeki toa hiyo tairi funga spear tukasepa wakatutafuta kwa kuomba misamaha kibao tuwape kidude chao
 
Ukute dingi aliona hii ndio nafasi ya kukumbushia kurenga😂 hapo funzo ni serikali iwakumbuke maigp kwenye vijisafari vya nje huko wakarelax
Nasikia hakusoma pia
Lakini kwa nini usubiri eti Serikali wakukumbuke kwenye vijisafari vya nje ilhali mstaafu hupokea malipo makubwa mwanzoni si angelitumia kwenda kujirusha huko nje? au bado anaHang over ya posho za kiserikali?
 
Mzee wa Ngunguri
 
Attachments

  • images (15).jpeg
    images (15).jpeg
    27.6 KB · Views: 3
Lakini kwa nini usubiri eti Serikali wakukumbuke kwenye vijisafari vya nje ilhali mstaafu hupokea malipo makubwa mwanzoni si angelitumia kwenda kujirusha huko nje? au bado anaHang over ya posho za kiserikali?
😂Itakuwa Hang over. Nilisikia Kuna kipindi TRA walimkalia vibaya
 
Baada ya kustaafu, mzee huyu kwasasa anaishi mkoani Morogoro. Moja ya madoido yake katika uzee wake ni kuchomoa hadharani silaha yake ya moto (bastola) kila anapokerwa na mtu.

Miongoni mwa matukio ya ajabu aliyofanya ni kupiga risasi lock iliyowekwa kwenye gari yake baada ya kupaki sehemu isiyo sahihi.

Mzee alipaki gari yake binafsi, akaingia sehemu, alivyotoka akakuta gari imepigwa lock, akauliza ni nani kaifunga? Kwa mamlaka gani? Inamaana hajui gari yangu? Akachomoa bastola akaitandika ile lock ikafunguka bila kuathiri tairi, akaitupa huko, akaondoka!

Mwamba aliyeifunga aliogopa hata kusogea eneo la tukio.

Nikweli mzee ulikuwa nafasi ya juu sana, ila hilo lisifanye uishi kibabe mzee, mbona ma CDF wastaafu tunaishi nao fresh tu na wana unyenyekevu mkubwa?

Badilika.
Muee ya ngunguri!
 
A
Kusema kweli una lock gari ya IGP mstaafu...Watanzania wenzangu kulala na kuamka salama sio jambo dogo...kuna watu hawalali ili sisi tulale na tuamke vyema...yupo sahihi sana imagine amepiga chuma bila kuathiri tairi la gari mlitazame hili..yupo makini kiasi gani...hongera mahita
Aisee!
Pole yako.
 
Ana tumia gari gani kwanz aisije kua ni subaru yenye turbo na sport rims [emoji81] .afu tuna ongea humu kutoa kufunga gari lake
 
Sasa wewe uishi chuo cha sokoine, Kuna umuhimu gani kumfahamu mahita. Gari ya shabiby wala abood hujawahi iona. Ila maisha yakiwa ya mjini utafahamu tu, haswa kwa hao watu wa parking.
Mm nimemjua mahita kabla sijafika mzumbe, na nikiwa mzumbe 3 years sikuwahi kuona gari yake. Ila nimeishi mjini, nimefanyakazi, na nilikua na duka, na nimemuona tena mahita tena zaidi ya mara moja.
Manispaa ya Morogoro ni kubwa kuliko mahita.Na hao watu wa parking Kuna wanaostaafu na wengine ni waajiriwa wapya ambao huchukua muda kadhaa kuyazoea magari na wamiliki wake.Mimi kwamfano nimeishi Tanga mjini miaka Tisa bila kutoka ila Kuna watu maarufu sana kama matajiri maarufu, na viongozi wastaafu kama wabunge , mawaziri na wanajeshi wastaafu ambao sikuwahi kuona magari yao. Halafu kwa watu wenye pesa ndefu hawakai na gari moja muda mrefu. Hupenda kubadilisha na kununua magari ya kisasa zaidi kwa sababu Hela inaruhusu. Kwa mfano wakati mahita anastaafu kuna magari ya kisasa yalikuwa hayajatoka ambayo bila shaka atahitaji kuwa nayo ili kwenda na wakati . Kwa hiyo Bado kusema kwamba wakazi wa Morogoro wote wanalijua gari la mahita sio kweli.
 
Nanukuu: "Mtu yyte lazma uijue gari ya huyu bwana, else wise ni dharau. Na hiyo ndio kazi ya bastola."
Mkuu, Hiyo gari yake ina utambulisho(Identity) gani wa kipekee kiasi kwamba mtu yeyote ni lazma aijue? Mbona ss huku umasaini ndani ndani huku hatuijui au sisi sio watu?
Je, kazi ya bastola ni kufungua lock za magari? Tafakari.
Huyo mwamba mstaafu inabidi ajitambue(Kama bado akili iko vizuri) kwamba ni muda wake sasa wa kupumzika na kuyafurahia mema ya nchi na sio kuendeleza ubabe. Wahenga walitanabahisha "Dunia huwatiisha watu".
1. Hiyo gari yaweza kutofanya kazi muda wowote e.g. kuharibika au vinginevyo;
2. Hiyo bastola sio mali yake - amedhaminiwa tuu i.e. anaweza kutakiwa kisheria airudishe kwa waliompa.
3. Kadri umri wake unavyosogea, anaweza kufikia umri ambapo asiweze tena kuvitumia hivyo vitu hata kama bado atakuwa navyo.
Ushauri: IGP (Inspector General Police) Mstaafu, kwa heshima alokuwa nayo (kabla na baada ya kustaafu) ndani ya Jamii ingependeza zaidi akawa ni mfano wa kuigwa na sio kuwa ni mtu wa vitisho na kuonesha umwamba.
IGP mstaafu sio askofu mstaafu msichanganye mambo.

Watu wamelika akili zimechoka kwa ajili ya usalam wa nchi miaka kibao,anakuja mtu ambaye hata hajui gharama za hayo anasababishia mzee huyu usumbufu,
Haikuwa kazi ya mfunga lock kujua gari ni ya nani,ila nina imani sasa anaifahamu na atafahamisha wengine.

USA wana salamu kwa wanajeshi"thank you for you're service"kuonyesha wanakubali mchango wao.haighalimu chochote kukubali mchango wa mtu wa aina yake,kwa kumpa favour sehemu yoyote ukimkuta,sio unyonge ni ukomavu wa fikra.unaona kijana alipotea kabisa sababu alijua kabisa bila kujua kafanya jambo la hovyo.
 
Manispaa ya Morogoro ni kubwa kuliko mahita.Na hao watu wa parking Kuna wanaostaafu na wengine ni waajiriwa wapya ambao huchukua muda kadhaa kuyazoea magari na wamiliki wake.Mimi kwamfano nimeishi Tanga mjini miaka Tisa bila kutoka ila Kuna watu maarufu sana kama matajiri maarufu, na viongozi wastaafu kama wabunge , mawaziri na wanajeshi wastaafu ambao sikuwahi kuona magari yao. Halafu kwa watu wenye pesa ndefu hawakai na gari moja muda mrefu. Hupenda kubadilisha na kununua magari ya kisasa zaidi kwa sababu Hela inaruhusu. Kwa mfano wakati mahita anastaafu kuna magari ya kisasa yalikuwa hayajatoka ambayo bila shaka atahitaji kuwa nayo ili kwenda na wakati . Kwa hiyo Bado kusema kwamba wakazi wa Morogoro wote wanalijua gari la mahita sio kweli.
Sawa
 
Back
Top Bottom