DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Duh! Kwa jinsi ya majibu hayo; Unaweza na unafaa kuwa chawa wa IGP mstaafu. Hongera sana.
Ndio watanzania mnapoishia akili zenu, unaelezwa unaleta story za uchawa. Njoo na opinions zako, Unaongelea uchawa.
Very low minded aisee
 
Mleta mada tusimulie vizuri hili tukio😂 baada ya kufyatua risasi hakuipuliza bastola pale mbele kama kwenye movie kweli ?

Dingi limekaa kijambazi sana 😂 Huwa napenda kusoma stories zake
 
Mimi nilikuwa pale muhimbili hospital, nikiwa natoa gari bahati mbaya nikagusa gari lingine kwa nyuma, wale walinzi suma jkt wakaizingira gari yangu. Hapo nilipoigusa hiyo gari mwenyewe hata ukimuonesha hawez kupaona. Wakasema hii gari ni ya generali wa jeshi huwezi kutoka mpaka afike hapa uelewane nae, kipindi tunaendelea na mjadala ghafla nashtukia gari ishatiwa lock na mlinzi mwingine.

Nikiwaambia nionesheni huyo jenerali alipoelekea nikaongee nae, wanasema hawawezi kufanya hivyo mie nisubiri mpaka atoke. Mara naambiwa huyo jenerali ni daktari pia kitengo cha wagonjwa wa dharura.

Hapo nipo na mzee wangu ambae nilimleta hospital akitokea kigoma. Namcheki mzee anatetemeka kusikia jenerali, nadhani alikuwa anawaza vita ya kagera na iddi amini😀😀😀

Dakika chache akaja MP wa jeshi akauliza kuna nini hapo na mbona mmezingira gari ya mzee (akimaanisha hiyo gari ya mkuu wake) nikashuka nikamsalimia salamu ya kawaida tu, habari yako kiongozi, imetokea bahati mbaya wakati natoka nimeigusa gari ya mkuu kidogo sana hapa (huku namuonesha sehemu nyingine) jamaa akasema mbona padogo saana, hata mzee hawez kupaona, mimi mwenyewe sijaona shida iliyopo..

Jamaa akaagiza lock zifunguliwe then niruhusiwe niondoke, suma wakafanya hivyo naondoka ety wakanizuia tena kuona yule MP kaondoka, ety ooh mzee akija akigundua atatumaindi sie, tuachie chochote tumpange mzee akitoka. Nikacheka saaaanaaaaaaaaa 😀😀😀😀😀😀

Mlipaswa muongee hivyo mapema kabla yule MP hajairuhusu gari yangu na nyie kukubali. Nitaenda kumwambie yule bwana mnaniomba rushwa...daah jamaa waligeuka nyuma bila kuuliza kitu.
 
Ukute dingi aliona hii ndio nafasi ya kukumbushia kurenga😂 hapo funzo ni serikali iwakumbuke maigp kwenye vijisafari vya nje huko wakarelax
Nasikia hakusoma pia
 
Kuna watu wanahitaji kutiwa adabu waheshimu wastaafu acha awape doscipline
Mbona wastaafu hawavagi beji kifuani ili watambulike na hivyo waheshimiwe?
Kwani hivi asingekuwa na hio silaha angefanyaje ?
Nadhani huko kumiliki gari na kuli park mahali sio sahihi na kutumia silaha kinyume cha maelekezo ya Umiliki wa silaha Kisheria kulifungua gari, kunatosha kuwa ni kiashiria na kielelezo cha wazi kwamba jamaa kwa sasa anatatizo la kiakili na kwa hiyo anahitaji msaada. Serikali ilitazame hilo.
 
Jamaa lilibaka House girl na kukataa mtoto na Bado halikufungwa.. kwake haka ka issue ka bastola ni kadogo sana
 
Hivyo ndivyo na issue ya mahita ingeliweza kumalizwa kwa mtindo huo na sio kupiga risasi simply eti kwa kuwa anayo bastola.
 
Hapana ndugu. Manispaa ya Morogoro inapoajiri watumishi haiangalii kama ni wenyeji wa siku nyingi au wametoka mikoa mingine.
Hivyo hata mtu kutoka Kigoma au Pemba anawezaajiriwa na manispaa ya Morogoro. Kusema kwamba wakazi wa Morogoro wote wanaijua gari ya mahita sio kweli.
Mimi nimeishi pale chuo Cha Sokoine SUA kama miezi minne na na nikienda mjini karibia kila siku na sikuwahiona gari la mahita.
 
Anatumia gari aina Gani huyo dingi
 
Hapendagi ujinga
 
Mkuu, it seems hiyo gari wanaoijua ni wale watu wa aina yake mahita (Wababe)na pia hawajui, hawakubali na hawatambui uwepo wa watu raia wengine wasio wa aina yao na wanaotokea maeneo tofauti na anapopark gari yake hiyo ila wameajiriwa na katika Ajira mtu unaweza kubadilishwa kituo cha kazi wakati wowote.
Huko ni kufilisika kimawazo.
 
Fungeni magaru yao ndo mtajua hao cdf ni watu wema au la
 
Sasa wewe uishi chuo cha sokoine, Kuna umuhimu gani kumfahamu mahita. Gari ya shabiby wala abood hujawahi iona. Ila maisha yakiwa ya mjini utafahamu tu, haswa kwa hao watu wa parking.
Mm nimemjua mahita kabla sijafika mzumbe, na nikiwa mzumbe 3 years sikuwahi kuona gari yake. Ila nimeishi mjini, nimefanyakazi, na nilikua na duka, na nimemuona tena mahita tena zaidi ya mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…