Serikali inanunua ndege kwa mbwembwe huku wanafunzi 65,000 wanakaa chini!

Kwa hiyo wakishajenga ofisi nzuri ndo ndo ufumbuzi wa kupata hayo madawati 65,000?
Ama kweli kuwa chawa ni aibu kwa taifa. Yani mtu unazungumzia madawati kana kwamba hauoni au haujui kinachofanyika nchini. Kwa sasa serikali imejielekeza katika ujenzi wa shule za kisasa (msingi na sekondari) huku swala la madawati, vyoo na nyumba za walimu vikipewa kipaumbele. Miaka minne ijayo hakuna mwanafunzi atakaekuwa anakaa chini pia hakuna mwanafunzi atakaekosa darasa. Hii ndio serikali ya mama Samia.

Well said.
 
Chawa na kunguni ni wewe unayechanganya mada.

Wenzako wanaongelea madawati wewe unavimba na ofisi za Chadema!

Foolish.
 
Pesa ya kuazima haisitiri umasikini wako!

Madarasa na miundombinu ya kujengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe ni suluhisho la kudumu?!!
 
Matatizo yetu ni mengi sana ikiwemo upingaji wa kodi hizo hizo kwa sababu za kisiasa na elimu kuwa duni.

Nadhani unakumbuka namna tozo zilivyopingwa wakati huduma nzuri zitokanazo na kodi hizo kila mtu anazitaka.
 
Yeyooooo

Ova
 
Tuliambiwa kupitia tozo za miamala zitapelekwa kwenye elimu na sehemu nyingine sasa hao sumbawanga siyi watanzania?
 
Jf ligi haziishagi

Bora nliamuaga kuwa nutro

Ova
 
Bila picha au uthibitisho ni UCHONGANISHI
 
Sidhani kama unatumia akili za kawaida zaidi ya kutumia akili za kichawi kichawi kichawi.
 
Pesa ya kuazima haisitiri umasikini wako!

Madarasa na miundombinu ya kujengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe ni suluhisho la kudumu?!!
Huyo hana uwezo wa kuyajibu hayo maswali uliyo muuliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…