#COVID19 Serikali inatudanganya kuhusu Corona au ni siasa za kuomba hela IMF na Europian Union?

#COVID19 Serikali inatudanganya kuhusu Corona au ni siasa za kuomba hela IMF na Europian Union?

Hizo za Tanzania au Uingereza?

Tanzania asilimia ya waliochanjwa ni ngapi na Uingereza ni ngapi?
Je who inasema ukichajwa unavua mask?

Mbona waliochajwa hawatakia kusikia viziba mdomo?
 
Waharakishe izo chanjo tu, haya mambo ya kutishana sio poa. Serikali ni moja ile ile ya ccm ila haieleweki mara corona ipo mara tena haipo.

Walete chanjo tu watu wachanjwe maisha yaendelee kama zamani ila wakianza tu kuleta siasa, tutaishi kama wakimbizi nchini kwetu.
 
Uingereza asilimia ya waliopata chanjo ni ngapi, Tanzania ni ngapi?
Hii ni hoja dhaifu, kuchanjwa sio solution ya corona, kikubwa ni kuachana na kutiana hofu, serikali saiv mnatutisha mno, huu ugonjwa ni kama magonjwa mengine sema viongozi mnaukuza mno!!! Mm nilishasema sivai mabarakoa yenu hayo
 
Waharakishe izo chanjo tu, haya mambo ya kutishana sio poa. Serikali ni moja ile ile ya ccm ila haieleweki mara corona ipo mara tena haipo.

Walete chanjo tu watu wachanjwe maisha yaendelee kama zamani ila wakianza tu kuleta siasa, tutaishi kama wakimbizi nchini kwetu.
Hata wakileta hiyo chanjo watachanjwa wao ila mimi sichanjwi
 
Je who inasema ukichajwa unavua mask?

Mbona waliochajwa hawatakia kusikia viziba mdomo?
Kwa hiyo kama WHO haijasema ukichanjwa unavua mask maana yake imesema usipochanjwa usivae mask?

What kind of logical non sequitur is that?

Unaelewa kwamba chanjo ndiyo imewapa Waingereza nafuu ya kuwawezesha kutupa barakoa?

Wewe ni kama unamuangalia mtu aliyevuka mto wenye mamba wengi, kafika upande wa pili, ameutupa mtumbwi kwa sababu hauhitaji kwa sana tena, hususan kwa sasa. Anaona kashavuka mto.

Unataka kumgeza, wewe hujavuka mto, unasema unataka kutupa mtumbwi.

Unasemq "Ona yule kautupa mtumbwi wake baada ya kuvuka mto. Na mimi sijavuka mto, huu mtumbwi hquna maana niutupe tu"
 
Hii ni hoja dhaifu, kuchanjwa sio solution ya corona, kikubwa ni kuachana na kutiana hofu, serikali saiv mnatutisha mno, huu ugonjwa ni kama magonjwa mengine sema viongozi mnaukuza mno!!! Mm nilishasema sivai mabarakoa yenu hayo
Nakwambia hivi, kuchanjwa ndiko kumewawezesha Waingereza kupata nafuu mpaka kuona hawahitaji barakoa.

Na unapowataja Waingereza kuacha barakoa, usijilinganishe nao kama wewe hujachanja bado.

Ukitaka kuongelea solution, kutegemea na unavyo define solution, unaweza kusema ugonjwa wowote wa kuambukizwa, kwa kuwa unaambukizwa, hauwezi kuwa na solution 100% kwa sababu unaweza kulipuka anytime.

Sasa wewe unataka kuwaiga Waingereza ambao wamechanja zaidi ya 50% ya population yao wakati wewe hata kuchanja en masse hujaanza?
 
Back
Top Bottom