Serikali inavuna ilichopanda: Fundi Maiko Syndrome - Goba Collapse

Mtoa mada yupo sahihi nawe pia upo sahihi but yeye anaongelea quality.huu mtindo wa force account aliouanzisha Magufuli ni hovyo kabisa na hautakiwi kwa karne hii ya 21.
Watu wanaenda shule kusomea haya mambo kwa lengo la kuminimize risks zilizokuwa zinatokea kabla Nchi hatujawa na wataalamu hao.

Inachokifanya Serikali kuounguza gharama za ujenzi kwa njia ya kutumi local fundi kwa kisingizio cha supervision kutoka kwa engineer wa Halmashauri ni zaidi ya ujinga
 
Chochote kinachohusisha utalaamu lazima kiwe na gharama,hakuna ujuzi ambao cheap sababu ya gharama za wakandarasi kuwa kubwa ni kutokana na ukirikimba wa serikali nyenyewe ikiwemo ucheleweshaji wa malipo.
 
False account na ubora wa hilo jengo binafsi unahusiana vipi?
Majengo yote yenye mfumo wa ghorofa kuna kanuni sake za ujenzi ikiwemo kutumia kandarasi kuanzia design,ujenzi wa mifumo na jengo lenyewe.Sasa kama wewe Serikali ambaye ndio msimamizi mkuu wa kila kitu katika Nchi unatumia local fundi katika majengo ya Umma vipi Mwananchi wa kawaida
 
Frame za hivi zipo nyingi Sana Dsm zinatakiwa kukaguliwa
 
Yaani foreman akisaidiwa na injinia mkuu uko serious kweli? Yaani una maanisha injinia amsaidie kazi foreman? Acha dharau asee!!
Soma sentensi nzima uone anachosaidiwa!! Kama huwezi kufanya kitu au kusoma mchoro si unasaidiwa na anaejua ama??
 
Utaalamu unawekwa pembeni wakati watu wanataka kupanda chati za kisiasa
 
Emetumia nguvu nyingi mkuu, usichukulie kila kitu serious this is jf....nlipoandika mwandiko skumaanisha lazima wewe uelewe nlichoandika
 
Kuna watu wanachekesha sana nchi hii,hata kama mi sio engineer lakini siwezi kufanya upuuzi kama uwo.juu umeweka tofari za kutosha alafu chini hamna tofari.unategemea uzito usizidi kweli
 
Kuna watu wanachekesha sana nchi hii,hata kama mi sio engineer lakini siwezi kufanya upuuzi kama uwo.juu umeweka tofari za kutosha alafu chini hamna tofari.unategemea uzito usizidi kweli
Tofali za kwako ni za kwako.
Jenga nyumba unayoitamani.
 
Profession za watu CCM wanazifanyia mzaha kwa kufuata mawazo ya akina msukuma na kishimba. Watavuna kwa wakati wao.
 
Emetumia nguvu nyingi mkuu, usichukulie kila kitu serious this is jf....nlipoandika mwandiko skumaanisha lazima wewe uelewe nlichoandika
Huwa sipendi mtu mmoja kumdharau mwingine.
Haya bana.
 
Mtoa mada na baadhi ya wachangiaji hawaelewi kabisa dhana ya force account.

Lakini pia hajui taratibu za kifedha na manunuzi za Serikali kuwa ni tofauti na mtu binafsi

Pia haamini kuwa kuna watu wengi nchini wamejenga bila vibali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…