Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Wanaochaguliwa hawaend,nafas znabak vacant wanaanza kuokoteza wabovu,wanaohamia na watovu wa nidhamu wanaohamia toka shule mbalimbali ilimradi tu shule zisikose wanafunzi

Ndo maana skuhz shule teule hazifanyi vzur sn Kama miaka ya zamani maana zinachanganyiwa Sana makapi
Mkuu naona taratibu tunaanza kueleewana sasa. Na haya makapi ndio hao wanafunzi wa shule za kata wanaopendelewa.
 
Kwenda special schools ni swala la bahati tu


Wanaopata A ni wengi mno hivyo hawawezi wote kuzingatiwa

Hata form four hivyo hivyo watu wanapiga one kali na wanapelekwa A level shule za kawaida
Kama wanaopata A ni wengi kuliko nafasi zilizopo kwenye special schools, kwanini isichezeshwe bahati nasibu ili kuleta usawa badala ya kupendelea wanafunzi wa shule za Kayaumba?
 
Akili za CCM, hovyo kabisa, kipaumbele ilibidi iwe, aliyepata A, aende shule Bora, bila kujali ametoka shule gani, binafsi au ya kata primary,
Sasa kwa akili za CCM, wanaona wakipereka wenye A wote shule teule,shule zao za kata zitabakia na wenye uwezo mdogo, na mstokeo baadae yatakuwa mabaya!
Angalizo, wanafunzi wa shule za msingi za serikali, wengi wanafeli sio kwa vile hawana uwezo, sababu ni uhaba wa, miundombinu ya kufundishia, vitabu, maktaba,waalimu wenye Hari, wingi wa wwnwfunzi darasani,
Mtoto akipewa mazingira mazuri ya kusoma, uwezekano wa kufsnya vzr, unsongezeka, wale walifanya vibaya wakipelekwa shule zenye miundombinu Bora, wanaweza kufsnya vzr tu
 
Mambo usiyoyajua mkuu usikimbilie kuja kuilaumu serikali, kilichofanyika hapo ni hesabu ya hali ya juu! Wewe umeshindwa kungamua tu!! Kwa hili naipongeza serikali! Kilichofanyikq hapo mm nakijua ni utaratibu na hesabu ndizo zinazofanya hivyo mkuu wala sio ubaguzi!!
CCM kujifsnya wana akili kama Eron Musk! Onyesha hizo hesabu za Hari ya juu!
Kupanga wanafunzi, kuna hitaji integration!? Pls chawa wa CCM, oneni aibu!
Kama kupanga wanafunzi kuna hitaji akili kubwa kama ya kutengeneza drone, indio maana vitu vikubwa vinatushinda, umeme shida, mwendo kasi shida, air Tanzania shida,
 
Kiongozi kwenye selection za form one Kuna vigezo ambavyo huangaliwa. Na selection zintofautiana.

Kwanza huwa ni uwiano kwa maana waliosoma shule binafsi na kutwa kuja kuunganishwa pamoja. Hapa anachukuliwa mwanafunzi aliyefanya vizuri private na government wanapelekwa shule za bweni au kutwa.

Pia wanachukua wanafunzi walifanya vizuri kutoka kila Halmashauri kuwaunganisha. Yani hata kama walioongoza wote wanatoka Temeke wao wanachukua labda watano kutoka kila Halmashauri, maana yake hata wale wa Buhigwe ambao was kwanza wao alikuwa na B anachukuliwa. Na mambo huenda kubadilika wkikutanishwa pamoja. Hao unaowaona wamefanya vizuri sana kutoka private wakati mwingine hulambishwa mchanga na hao unaoona hawajafanya vizuri.

Na selection ipo ya kutwa, bweni ufundi, bweni kawaida, bweni ufaulu mzuri na bweni mahitaji maalum. Serikali huhakikisha huko kote waliosoma mijini, vijijini, private na government wote wanapata nafasi kwa uwiano uliowekwa.

Serikali ingekuwa inabagua si ingeamua tu waliosoma private wabaki hukohuko, lakini haifanyi hivyo kwa sababu wanataka utangamano wa wanafunzi
 
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.

Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.

Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.

Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!

Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Assumption ni kua Wazazi waliolipia miaka 7 ya primary kwenye Private School hawatoshindwa kulipia miaka minne O level kwenye Private School
 
kubase kwenye marks/matokeo au kwasababu hakusoma shule bora.
Mkuu upo serious au unatania? Kwa hiyo wanafunzi wawe wanachaguliwa based on POVERTY rather than MERIT? Sasa hiyo itakuwa shule au uchaguzi wa VITI MAALUMU? Tuwe serious na mambo ya elimu jamani; vinginevyo nchi itachelewa sana kupata maendeleo.
 
@tpaul hajaotoa ushahidi au hoja yoyote ile yenye mashiko inayounga mkono madai yake kwamba Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi.
Utafiti hukosolewa kwa utafiti. Kama unaona utafiti haujakamilika, basi wewe nenda kafanye utafiti wako makini utuletee majibu hapa mkuu. Vinginevyo ukae kimya. Huna hoja,
 
Upo uwezekano mkubwa wa hao wa 2 waliochaguliwa kutoka shule binafsi wasiende huko walikochaguliwa.
This is not the matter we are talking about here. Please read the topic afresh and come again.
 
Wenye A karibu wote wa PHILADELPHIA PRIMARY SCHOOL iliyopo Kongowe ya Mbagala Dar, wamepelekwa Mwandege kutwa..!!
Waliopata A Shule binafsi ni wengi tu hawawezi kuenea wote kwenye hizo shule teule lazima waende baadhi tu.

Na lazima uchukue na wengine baadhi kutoka shule za umma waliofanya vyema nao waende hizo shule teule.

Huwezi kupeleka kundi moja tu shule teule.
 
Mdau nikuulize maswali haya na unijibu

1. Unafikiri watoto wa private wana akili kuliko wa government? Kwakuwa ndo wamefaulu sana?

2.sisi masikini ambao hatuna uwezo wa kuwapeleka watoto private hizi nafas hazituhusu? Maana ufaulu wa shule za serikali unajulikana

3. Mbona kuna watu walitoka huko shule private na ufaulu mzuri kuliko waliotoka serikalin tulipokutana advance wakawa wanazidiwa? Huko private kuna nini? mbona kwenyewe walifaul vizur?

4. Wanaopanga wengine wamepita huko private michezo ya huko wanaijua vizuri tu

5. Kama unamtoto huko private muulize wakati wanakaribia kufanya mitihana walisovu maswali ya kufanania na wakayakuta kama yalivyo? Akupe majibu
Majibu
1. Ndio. Mpaka sasa kipimo kinachotumiwa ni ufaulu wa masomo kwenye mitihani. Wee unayelazimisha kipimo kingine kitumike nje yya ufaulu (UPENDELEO) unachekesha sana. Hki ndicho ninachokataa na ndicho ninachokemea kwenye hoja yangu.

2. Uchauzi wa wanafunzi haupaswi kuangalia kigezo kingine zaidi ya ufaulu. Kwenda nje ya ufaulu ndio ubaguzi wenyewe ninaoongelea hapa. Kumbe wewe umeishanielewa.

3. Kinachoangaliwa kwenye selection sio matokeo ya baada ya uchaguzi. Hata wanafunzi kutoka kayumba wanachaguliwa wakiwa na A zote lakini wakienda sekondari wanatoka na sifuri. Kigezo cha ufaulu baada ya kuingia sekondari, hakijawahi na wala hakitakaa kitumike kwenye selection.Kama kikitumika, huo utakuwa ubaguzi uliopindukia.

4. Michezo gani? Kama una ushahidi weka hapa. Vinginevyo, hoja hii ipeleke kwenye kijiwe cha kahawa; hapa JF sio mahali pake.

5. Mtihani wa NECTA ni mmoja tu na ndio unatumika kufanya selection. Huo mtihani wako unaopendekeza sio rasmi na wala haueleweki.
 
kama mwanao ulikuwa unamsomesha shule za gharama na amepata alama A hicho sio kipaji. sasa utajiuliza kwa nini sio kipaji?
Kwani wanafunzi wanaochaguliwa kwenda shule za vipaji maalumu wanachaguliwa kwa kuangalia kigezo gani mkuu?
 
Genius wa private atapimwa na wenzake huko private, na genius wa government atapimwa na wenzake huko government!
Kwa hiyo unashauri NECTA wawe wanatunga mithani ya aina mbili.....mmoja wa private na mwingine wa government schools au unataka kusema nini mkuu? So long as mtihani ni mmoja kwa shule zote, equality lazima itawale.....kufanya kinyume ni ubaguzi. Na hii ndiyo hoja iliyopo mezani hapa.
 
shule za gharama sio vipaji,kwanini sio vipaji? unaweza kujiuliza, jibu. shule za gharama Ina kila kitu cha kumfanya mwanafunzi apate alaama A.mfano nikupe chukua mwanafunzi ambaye amesoma shule za kawaida amepata alama A.je angesoma shule za gharama huyo mwanafunzi angepata alama gani? toa jibu mbona umekaa kimya
Unachosema kipo nje ya mada tunayojadili mkuu.
 
hata hao wa kwenu ni vilaza waliokaririshwa majibu, wajinga ndio waliwao. Hao watoto wenu wakifika vyuoni wanapigwa mbaya sana na hao wa shule za serikali, mnajilisha upupo tu na kuliwa mapesa kwa ulimbukeni wenu
Mkuu tumekuelewa na tumekufikia. Tunaomba sasa ujikite kwenye mada. Mbona unakuwa kama kuku anayetaka kutaga? Hutulii. Jikite kwenye hoja usizunguke tu kama kipepeo bila muelekeo.
 
Kwenye serikali unaionea bure uchaguzi kwa shule teule wanaangalia VIGEZO MUHIMU KAMA ALAMA KWA KILA SOMO NA PIA A UNAYOSEMEA INATEGEMEA NI A YA NGAPI ?UNAWEZA KUPATA 41 NI A NA MWINGINE AKAPATA A YA 48 KWA SELECTION HUYO WA A 48 ATAPATA SHULE TEULE
 
Pia shule teule huwa nafasi kwa kila wilaya na siyo A tu bali kila wilaya wanapewa labda Nafasi tatu za wasichana waende msalato moja tabora boys.Ikiwa wewe ni wa mjini usitegemee nafasi hizo kupata kwa sababu nafasi ni fixed kwa kila wilaya
 
Huwezi kulinganisha ufaulu wa Kagera na Mtwara au Lindi na Mbeya au Katavi na Kilimanjaro.
Huwezi kuweka mizani sawa hata siku moja. Kata ya Umasaini iwe sawa na kata ya Dsm! Nooo!!

Mimi si mmoja wao. Ni fikra zangu zinanifikirisha hivyo
Hapa unataka kusema nini
 
Hivi huwa mnawaza watoto wote wanaofanya vizuri kwenda baadhi ya shule wenye ufaulu wa wastani wanabaki, form matokeo yao yatakuwaje
 
Back
Top Bottom