Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe una matatizo. Upendeleo wa aina yoyote ile ni ukiukwaji wa KATIBA waliyoapa kuilinda na kuitetea. Acha kushabikia ujinga mkuu. Watu wa sampuli yako ndio mnasababisha serikali isiboreshe shule za umma. Punguza ujinga kama huwezi kuacha.Nafikiri umekurupuka, pia sio mbaya serikali ikiwapendelea hao, sioni ubaya wake.
Bi wa Kizimkazi kishasema muache kulaumu na kulalamika.Hapa Tunachotakiwa kuilaumu serikali Ni kutokuboresha mazingira mazur gov schools
Kwahiyo suluhisho ni kutujazia watoto wote wa darasa moja kwenye shule moja tena darasa moja?? Inaonyesha hujaelewa kabisa nini kinajadiliwa..!! Ishu ipo hivi, Mwenye C huko private aende hizo za kutwa na mwenye C huko primary za serikali naye aende huko sekondari za kutwa..!! Lakini kumchukua mwenye A wa private kumpeleka sekondari ya kutwa halafu mweye C toka kayumba aende shule maalumu ndo upendeleo ulipo..!! Na ndo kinacholalamikiwa..!! Hakujatajwa uwezo wa mzazi kulipa mamilioni au kushindwa kulipa mamilioni huko private..!!! Na kwa taarifa yako, si kila aliyeko Kayumba maana yake ameshindwa kulipa ada za mamilioni huko private. Ni maamuzi na mitazamo ya shule zipi kila mmoja anaona zinafaa kuwapeleka watoto wake.Hakuna aliyeshushwa. Tatizo wengi wenu mnaowapeleka watoto huko private mnajilazimisha wakati vipato vyenu ni vya kubangaiza. Na bado akienda chuo anaweza asipate mkopo au akapata kwa % chache.
Wewe una matatizo. Upendeleo wa aina yoyote ile ni ukiukwaji wa KATIBA waliyoapa kuilinda na kuitetea. Acha kushabikia ujinga mkuu. Watu wa sampuli yako ndio mnasababisha serikali isiboreshe shule za umma. Punguza ujinga kama huwezi kuacha.
Hapa ndo unaharibu!Dawa ya hii serekale pigana upate Hela huduma zote utapata bila bughudha lakini ukianza kutaka huduma yao only 20% is available out of 100%
Umesoma kwa makini matokeo ya shule mbili alizotolea mifano?Sidhani.
Nahisi wanaochaguliwa kwenda shule teule ni waliofaulu kuliko wote nchi nzima.
Nipo tayari kukosolewa.
Kwani Nani amezuia serikali usiweke mazingira mazuri ya watoto kupata elimu Bora Kama wanavyofanya shule binafsi?shule za gharama sio vipaji,kwanini sio vipaji? unaweza kujiuliza, jibu. shule za gharama Ina kila kitu cha kumfanya mwanafunzi apate alaama A.mfano nikupe chukua mwanafunzi ambaye amesoma shule za kawaida amepata alama A.je angesoma shule za gharama huyo mwanafunzi angepata alama gani? toa jibu mbona umekaa kimya
Nimeshangaa sana hawa jamaa. Kuna dogo kijijini kwetu amepata wastani wa C mbovu kabisa eti amepangiwa korogwe girls alafu wale madogo waliopiga A wamepangiwa shule za kata. DuhKuna mdau aliandika humu, hakuna kitu hata kimoja ambacho serikali inafanya kwa ufasaha na usahihi. Ni kuunga unga tu mradi pakuche
we bwege endelea kuwasomesha shule binafsi, ulivyowapeleka shule binafsi shule ya msingi ulikuwa una malengo waende shule teule? Serikali iko makini, km hutaki waende hiyo shule ya kata warudishwe huko binafsi. Na ukae ukijua wataenda kusoma vyuo vya serikali na hawatakuwa na mikopo. Kupanga ni kuchagua. Mnaopeleka watoto hizo shule za gharama ni mabwege tu mnaoliwa hela na wajanja, walimu wanaowafundisha huko private ni watanzania wale wale waliosoma vyuo vya serikali, tofauti ni gharama na kiinglishi cha kuongea mtaani siyo kiinglishi cha kitaaluma. Watanzania wakiwa na vijihela kidogo ni malimbukeni.Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Katiba inatamka wazi kuhusu USAWA. Wewe unashabikia UPEBDELEO na UBAGUZI. Una akili timamu kweli?
nyie ni mna mambo ya kipumbavu, msiipangie serikali namna ya kuendesha shughuli zake, pambananeni na watoto wetu mnavyotaka mabwege nyieKwa kweli hii serikali ina mambo ya kipumbavu sana. Sijui wanafikiri kwa kutumia kiungo gani (Masaburi).
wakati mnapeleka watoto wenu private primary mlikuwa mna malengo gani, na kwanini leo mtake tena shule za serikali, kwanini msiendelee kuwasomesha huko private? Hata hivyo unatakiwa ujue vyuoni ataenda vyuo vya serikali tena akifaulu vizuri. Tatizo watanzania wanapenda sana social classes, elimu imekuwa km maonesho. Mwisho msitake serikali ifanye kazi kwa maslahi yenu, pambanneni na hali zenu.Hivi unajua unachokiongea kweli mkuu? Hesabu gani hizo ambazo hazifuati ufaulu? Ina maana hizi nafasi zinagawiwa kama njugu kwa matakwa ya watu kutoka juu? Ili iweje?
kuna mitihani ya Cambridge wapeleke huko hao watoto wako we kenge.Kwanini sasa wasitungiwe mitihani tofauti? Kama unasapoti ujinga huu, basi kuna haja ya kuwa na mabaraza mawili ya mitihani.....private na public. Au basi wawe wanatunga mitihani aina mbili...for private and government candidates.
Huwezi kusema hakuna usawa wakati wote wanasoma mtaala mmoja na vitabu vimoja. Bado hjanishawishi. Tangu lini nchi hii kila kitu kikawa sawa?