Mkuu naona taratibu tunaanza kueleewana sasa. Na haya makapi ndio hao wanafunzi wa shule za kata wanaopendelewa.Wanaochaguliwa hawaend,nafas znabak vacant wanaanza kuokoteza wabovu,wanaohamia na watovu wa nidhamu wanaohamia toka shule mbalimbali ilimradi tu shule zisikose wanafunzi
Ndo maana skuhz shule teule hazifanyi vzur sn Kama miaka ya zamani maana zinachanganyiwa Sana makapi
Kama wanaopata A ni wengi kuliko nafasi zilizopo kwenye special schools, kwanini isichezeshwe bahati nasibu ili kuleta usawa badala ya kupendelea wanafunzi wa shule za Kayaumba?Kwenda special schools ni swala la bahati tu
Wanaopata A ni wengi mno hivyo hawawezi wote kuzingatiwa
Hata form four hivyo hivyo watu wanapiga one kali na wanapelekwa A level shule za kawaida
CCM kujifsnya wana akili kama Eron Musk! Onyesha hizo hesabu za Hari ya juu!Mambo usiyoyajua mkuu usikimbilie kuja kuilaumu serikali, kilichofanyika hapo ni hesabu ya hali ya juu! Wewe umeshindwa kungamua tu!! Kwa hili naipongeza serikali! Kilichofanyikq hapo mm nakijua ni utaratibu na hesabu ndizo zinazofanya hivyo mkuu wala sio ubaguzi!!
Assumption ni kua Wazazi waliolipia miaka 7 ya primary kwenye Private School hawatoshindwa kulipia miaka minne O level kwenye Private SchoolSerikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Mkuu upo serious au unatania? Kwa hiyo wanafunzi wawe wanachaguliwa based on POVERTY rather than MERIT? Sasa hiyo itakuwa shule au uchaguzi wa VITI MAALUMU? Tuwe serious na mambo ya elimu jamani; vinginevyo nchi itachelewa sana kupata maendeleo.kubase kwenye marks/matokeo au kwasababu hakusoma shule bora.
Utafiti hukosolewa kwa utafiti. Kama unaona utafiti haujakamilika, basi wewe nenda kafanye utafiti wako makini utuletee majibu hapa mkuu. Vinginevyo ukae kimya. Huna hoja,@tpaul hajaotoa ushahidi au hoja yoyote ile yenye mashiko inayounga mkono madai yake kwamba Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi.
Waliopata A Shule binafsi ni wengi tu hawawezi kuenea wote kwenye hizo shule teule lazima waende baadhi tu.Wenye A karibu wote wa PHILADELPHIA PRIMARY SCHOOL iliyopo Kongowe ya Mbagala Dar, wamepelekwa Mwandege kutwa..!!
MajibuMdau nikuulize maswali haya na unijibu
1. Unafikiri watoto wa private wana akili kuliko wa government? Kwakuwa ndo wamefaulu sana?
2.sisi masikini ambao hatuna uwezo wa kuwapeleka watoto private hizi nafas hazituhusu? Maana ufaulu wa shule za serikali unajulikana
3. Mbona kuna watu walitoka huko shule private na ufaulu mzuri kuliko waliotoka serikalin tulipokutana advance wakawa wanazidiwa? Huko private kuna nini? mbona kwenyewe walifaul vizur?
4. Wanaopanga wengine wamepita huko private michezo ya huko wanaijua vizuri tu
5. Kama unamtoto huko private muulize wakati wanakaribia kufanya mitihana walisovu maswali ya kufanania na wakayakuta kama yalivyo? Akupe majibu
Kwa hiyo unashauri NECTA wawe wanatunga mithani ya aina mbili.....mmoja wa private na mwingine wa government schools au unataka kusema nini mkuu? So long as mtihani ni mmoja kwa shule zote, equality lazima itawale.....kufanya kinyume ni ubaguzi. Na hii ndiyo hoja iliyopo mezani hapa.Genius wa private atapimwa na wenzake huko private, na genius wa government atapimwa na wenzake huko government!
Unachosema kipo nje ya mada tunayojadili mkuu.shule za gharama sio vipaji,kwanini sio vipaji? unaweza kujiuliza, jibu. shule za gharama Ina kila kitu cha kumfanya mwanafunzi apate alaama A.mfano nikupe chukua mwanafunzi ambaye amesoma shule za kawaida amepata alama A.je angesoma shule za gharama huyo mwanafunzi angepata alama gani? toa jibu mbona umekaa kimya
Mkuu tumekuelewa na tumekufikia. Tunaomba sasa ujikite kwenye mada. Mbona unakuwa kama kuku anayetaka kutaga? Hutulii. Jikite kwenye hoja usizunguke tu kama kipepeo bila muelekeo.hata hao wa kwenu ni vilaza waliokaririshwa majibu, wajinga ndio waliwao. Hao watoto wenu wakifika vyuoni wanapigwa mbaya sana na hao wa shule za serikali, mnajilisha upupo tu na kuliwa mapesa kwa ulimbukeni wenu
Hapa unataka kusema niniHuwezi kulinganisha ufaulu wa Kagera na Mtwara au Lindi na Mbeya au Katavi na Kilimanjaro.
Huwezi kuweka mizani sawa hata siku moja. Kata ya Umasaini iwe sawa na kata ya Dsm! Nooo!!
Mimi si mmoja wao. Ni fikra zangu zinanifikirisha hivyo