Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Mkuu acha uvivu....pitia hayo matokeo uone uovu wa serikali yako. Wanafunzi waliopata B wa shule za kata wameenda shule teule huku wanafunzi waliopata A wa shule binafsi wamepelekwa sjule ya kata Changanyikeni. Huu ni ujinga usiovumilika. Acha kutetea uhuni na upuuzi wa serikali ya CCM.
Upo sahihi, kuna upendeleo fulani.

Ila labda watakua na vigezo fulani mkuu, private na kayumba wanatofautiana
 
Kwa hiyo una uhakika kuwa wanafunzi wa St Kayumba ndio wamepata A kali zaidi au unataka kutetea nini mkuu?
Nilitaka tu kumueleza huypo aliyesema nanukuu...

1703093474752.png


Kwamba hakuna cha huwezi jua, vitu vyote vinajulikana..!!
 
Watoto wenu mlitaka wachaguliwe shule gani zaidi ya kata?mtoto kapata A ya 92 unataka apelekwe shule ambayo inachukua A ya 98_100?
Mbona hatujawahi kuona wanafunzi wa vigogo wanachaguliwa kwenda shule za kata au wao wanafaulu sana? Acha kutetea upumbavu mkuu. Watu kama nyie ndio mnasababisha serikali ya CCM igome kuboresha mazingira ya shule za kata badala yake inawabeba wanafunzi vilaza na kuwasombea sekondari kwa kigezo cha mazingira magumu halafu inaumbuka baadaye.

Huu upumbavu wanaofanya serikali kwa kuchagua wanafunzi kwa upendeleo wa kipuuzi ndio unaosababisha uwepo wa wanafunzi vilaza kwenye sekondari zetu hivyo kuongeza wingi wa illiterates na ujinga kwenye nchi

 
View attachment 2848422
View attachment 2848424

View attachment 2848425
HAYA NI MATOKEO YA WALIOSOMA PHILADELPHIA PRIMARY SCHOOL.

NA ALMOST WOTE WAMEJAZWA MWANDEGE CHECK HAPA CHINI..!!

View attachment 2848428

View attachment 2848429

View attachment 2848430
Hii hali inahuzunisha na kusikitisha sana. ikiwa tutaendelea kukaa kimya ipo siku bomu la elimu litalipuka ktk nchi hii ya kusadikika. Hili sio jambo la kupuuza hata kidogo. Wananchi tuamke. Tunakanyagwa sana na hii serikali ya mchongo aisee.
 
Kuna mdau aliandika humu, hakuna kitu hata kimoja ambacho serikali inafanya kwa ufasaha na usahihi. Ni kuunga unga tu mradi pakuche
Na hali itazidi kua mbaya..kama waalimu wakuu na wasimamizi wa shule ndio wale tunawaona wanachangisha fedha kwa ajili ya ku support chama fulani unadhani atayasemea nani mambo kama haya?
 
Serikali hii inaamini kwamba, watoto wanaosoma shule za private wazazi wao Ni wafuasi na wanachama wa chadema na wanaosoma shule za kanumba wazazi wao Ni wafuasi na wanachama wa CCM.
Wanahisi wakiwachagua waliotoka shule za kulipia wanawapa ujiko chadema.
 
Nimeshangaa sana Mkuu...tumepitia changamoto nyingi kama Taifa...ila kwa hili walilofanya hawa wakuu ni la hovyo sana siju wana akili gani? Njaa mbaya sana.

Cha ajabu hata sijaona kiongozi ea serikali aliyekemea au kutoa ufafanuzi hata wa kinafiki kupunguza makali ya Hilo jambo.
 
Na mimi nitaelezea uzoefu wangu katika swala hili la selection kwa kidato cha kwanza. Jambo hili naweza kusema kwamba halijaanza leo, linaweza kuwa limeanzia tangu miaka ya 2008 na litaendelea. Kwanini nasema hivi? Sababu ni hii mimi mwenyewe nilikumbwa na kadhia hii hii japo nilisoma shule ya serikali. Matokeo yetu ya shule ya msingi yalikuwa mazuri mno kwani shule yetu ilikuwa inafahamika kwa kufaulisha vizuri. Lakini lilipokuja swala la selection za kidato cha kwanza hadi waalimu pale shuleni walibaki kushangaa. Kwani kwa ufaulu nilioupata na kupelekwa shule ya kata nilipofika kule nilishangaa. Nilitegemea kupelekwa shule ya mkoa kama si wilaya. Kwani kuna wanafunzi waliokuwa na ufaulu kama wangu wa shule nyingine na walipelekwa shule za mkoa au wilaya. Na kibaya zaidi aliyefaulu kwa ufaulu wa juu zaidi pale shuleni kwetu aliishia kupelekwa Azania wakati mdada aliyemfuata ndiye aliyepelekwa Shule ya Vipaji yaani Kilakala. Kwa kweli ilikuwa ni sintofahamu sanaa. Kwahiyo nataka kusema hili swala kwa sasa hv ndo linaanza kuonekana ukubwa wake. Lakini lilianzia miaka ya nyuma kabisa. Kuwa na amani, muhimize kijana wako asome kwa bidii katika shule aliyochaguliwa atafaulu, au laa ukiona haujaridhika baadae umuhamishie shule nyingine ya serikali utakayoona ina uhafadhali kuliko hiyo. Shule za Kata zimekuwa zikitazamika vibaya katika jamii zetu kutokana na miundombino pamoja na vitendea kazi vya kufundishia lakini pia na aina ya wanafunzi wapelekwao huko. Wengi wao wanakuwa ni wale wasindikizaji hili linazidi kuzifanya shule hizi kuzidi kudharaulika lakini, wewe kama mzazi lisikuvunje moyo mpambanie mwanao na atafanikiwa. Mimi nilifaulu vizuri kuliko hata baadhi ya waliopelekwaga shule za mkoa na wilaya sijisifii lakini natoa ushuhuda.
 
Hivi umekielewa kilichoandikwa au umedandia tu..!!??

Nakutolea mfano, Philaldephia primary school ilipo Kongowe ya Mbagala ni PRIVATE, lakini wanafunzi wake karibu wote wenye wastani wa A, wamepelekwa Mwandege kutwa ya serikali..!!
Ni sahihi kabisa. St Kayumba nao wanastahili kusoma pazuri. Ingekuwa mimi shule za private wote ndo wangeenda kutwa.
 
Back
Top Bottom