Na mimi nitaelezea uzoefu wangu katika swala hili la selection kwa kidato cha kwanza. Jambo hili naweza kusema kwamba halijaanza leo, linaweza kuwa limeanzia tangu miaka ya 2008 na litaendelea. Kwanini nasema hivi? Sababu ni hii mimi mwenyewe nilikumbwa na kadhia hii hii japo nilisoma shule ya serikali. Matokeo yetu ya shule ya msingi yalikuwa mazuri mno kwani shule yetu ilikuwa inafahamika kwa kufaulisha vizuri. Lakini lilipokuja swala la selection za kidato cha kwanza hadi waalimu pale shuleni walibaki kushangaa. Kwani kwa ufaulu nilioupata na kupelekwa shule ya kata nilipofika kule nilishangaa. Nilitegemea kupelekwa shule ya mkoa kama si wilaya. Kwani kuna wanafunzi waliokuwa na ufaulu kama wangu wa shule nyingine na walipelekwa shule za mkoa au wilaya. Na kibaya zaidi aliyefaulu kwa ufaulu wa juu zaidi pale shuleni kwetu aliishia kupelekwa Azania wakati mdada aliyemfuata ndiye aliyepelekwa Shule ya Vipaji yaani Kilakala. Kwa kweli ilikuwa ni sintofahamu sanaa. Kwahiyo nataka kusema hili swala kwa sasa hv ndo linaanza kuonekana ukubwa wake. Lakini lilianzia miaka ya nyuma kabisa. Kuwa na amani, muhimize kijana wako asome kwa bidii katika shule aliyochaguliwa atafaulu, au laa ukiona haujaridhika baadae umuhamishie shule nyingine ya serikali utakayoona ina uhafadhali kuliko hiyo. Shule za Kata zimekuwa zikitazamika vibaya katika jamii zetu kutokana na miundombino pamoja na vitendea kazi vya kufundishia lakini pia na aina ya wanafunzi wapelekwao huko. Wengi wao wanakuwa ni wale wasindikizaji hili linazidi kuzifanya shule hizi kuzidi kudharaulika lakini, wewe kama mzazi lisikuvunje moyo mpambanie mwanao na atafanikiwa. Mimi nilifaulu vizuri kuliko hata baadhi ya waliopelekwaga shule za mkoa na wilaya sijisifii lakini natoa ushuhuda.