Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.

Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na hapa, walikuwa wanatoka saa 6 mchana, sasa mwaka huu nikaona nimtafutie nursery bora angalau hata mwakani aanze la kwanza.

Aisee sasa hivi ndio nimekaa nyumbani, yapata muda kidogo wife alinambia siku hizi dogo hapendi shule, nikamwambia labda hajapata marafiki hiyo shule mpya!

Sasa hawa watoto wa nursery wanaamka saa 11:30 saa 12 gari lipo getini, kutoka shule saa 12, homework kibao, mtoto muda wote namuona kachoka.

Leo kaamshwa kwenda shule mtoto analia tu, yaani hawa watoto wana ratiba ngumu kuliko hata watumishi, hivi kweli nursery mkiwaachia saa 7 kuna tatizo gani? Wanacheza na kurelax saa ngapi hawa watoto?

Leo naenda kukiwasha shuleni, mwanangu mwisho saa 8 atakua anakuja kuchukuliwa anapelekwa nyumbani, kama hawataki poa tu nitatafuta shule nyingine, uzuri private zipo kama utitiri.

Serikali wekeni miongozo ya elimu, hwa watoto wana ratiba ngumu hata physiological sidhani kama wanafurahia shule kama miaka yetu ile.

Elimu yenyewe hii ya kuja kukutana na mishahara ya laki 4 ukitoka chuo, upuuzi tu!
Tafuta shule ambayo ni karibu na unapo ishi ili mtoto apate muda wa kulala na kumaliza usingizi hii ndo suluhisho
 
Naona mpumbavu umekuja jibu watu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mwelevu kwanini umpeleke shule ya ambali ambayo tena wakati unampeleka mtoto wako na taratibu uliambiwa?

Mwelevu usiejitambuwa kuwa wewe ni mjinga labda nikusaidie kitu kimoja tu ili mwanao asiamke muda huo ambao wewe unaona haufai

1. Mpeleke mwenyewe shule kwa usafiri wako au mkodi hata bodaboda

au

2. Nenda kakae karibu na shule unaependa mwanao akasome

Ni ujinga ambao ni wa kiwango cha juu sana kufikiria kuwa kuamka mapema ni kanuni ya shule hata ukiwa unakaa karibu na hiyo shule.
 
Hili nimeliona, nimeenda kuongea nae wananisusia eti utajua mwenyewe, nafanya utaratibu wa usafiri awe anaenda saa 2 saa 8 anatoka

Wengine tunatafuta kipato mbali kidogo na familia zetu hivyo tukipata hata muda wa kupumzika wiki 2 ndo mambo kama haya tunayaona

Hongera
 
Tutafute hela kwa wingi watoto wasiteseke....
Darasa la 4&7 wanaumizwa sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Yaani la nne na la saba wanaanza saa 12 mpaka saa 2 usiku. Serikali inatakiwa itoe waraka ili shule zote zifuate. Tulikua private sababu wana walimu wa kutosha wangeruhusu watoto mapema kumbe sio.
 
Mlete dumu fagio aje awe anabishana Kuhusu Simba na Yanga

Kiufupi shule za private zipo vizuri katika kuamua destiny ya mtoto huko baadae Mimi shule za serikali nazichukia sipendi mtoto wangu asome huko dumu fagio ni uchafu Sana .
80% ya mashoga original Yao shule za private.fanya utafiti
 
Mlete dumu fagio aje awe anabishana Kuhusu Simba na Yanga

Kiufupi shule za private zipo vizuri katika kuamua destiny ya mtoto huko baadae Mimi shule za serikali nazichukia sipendi mtoto wangu asome huko dumu fagio ni uchafu Sana .
Kuna wakati niliwahi mpeleka mwanangu.

Kila siku wanamwibia masaftari, kalamu, chupa ya maji na hata begi. haipiti wiki na ngeu mpya
Haipiti wiki ana UTI.

Mbaya zaidi teachers theydont care
 
Shule nyingi hizi za Yes No zina changamoto ya usafiri, unakuta shule nzima ina magari ma4 (mfano), gari la route ya Tabata hilohilo ndo linakwenda kuwakusanya watoto Tandika. Matokeo yake watoto kuashwa saa 9.

Nafikiri kwenye usajili na ukaguzi wa hizi shule hili pia liwe linaangaliwa. Kuna wakati vitoto vinapakatana.
 
Kuna wakati niliwahi mpeleka mwanangu.

Kila siku wanamwibia masaftari, kalamu, chupa ya maji na hata begi. haipiti wiki na ngeu mpya
Haipiti wiki ana UTI.

Mbaya zaidi teachers theydont care
Mi mtoto nishamwambia akipigwa akija nampiga, akiibiwa kitu sitamnunulia.

Nikawafata walimu wake nikawaambia pia.

Haya mambo yanalelewa na walimu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom