Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
Post yako haitoi solution but inaegemea kuficha aibu ya shule zisizo za kidini (kayumba) na dini fulani
kufuatia matokea ya kidato cha nne, form four 2024 yaliyotoka 23/1/2025 inaonyesha shule za dini zinafanya vizuri sana, lakini ukiingia ndani zaidi unakuta ni dini fulani huku zini zingine zikiachwa nje .
Je, ni wakati muafaka kwa SERIKALI KUTAIFISHA SHULE ZA DINI ili kila mtoto awe na usawa kwenye kufaulu ama serikali iache kila dini ijiamulie ama ELIMU DUNIA ama ELIMU AKHERA?
Hapa kuna hoja muhimu:
1. Uhuru wa Kidini: Katiba ya Tanzania inaheshimu uhuru wa dini. Kutaifisha shule za kidini kwa sababu ya matokeo yao ya kitaaluma kunaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa uhuru huu tu.
2. Ubora wa Elimu: Mafanikio ya shule yanatokana na mambo mengi, kama vile usimamizi bora, walimu wenye sifa, nidhamu, na rasilimali. Badala ya kutaifisha, serikali inaweza kujifunza na kuboresha shule nyingine kwa kuiga mifano bora kutoka shule zinazofaulu.
3. Haki na Usawa: Kutaifisha shule za kidini kunaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na malalamiko kutoka kwa dini husika. Ni vyema kuweka usawa kwa kushirikiana na taasisi zote za kidini badala ya kuziondoa umiliki.
4. Ushirikiano na Sera Bora: Serikali inaweza kushirikiana na shule za kidini kwa kuweka sera zinazoweka usawa wa fursa kwa wanafunzi wote bila kuingilia umiliki wa shule hizo.
MDAU MMOJA KIJIWE cha kahawa hapa Posta Mtaa wa Mkwepu anasema badala ya kutaifisha shule, serikali inapaswa kuimarisha mfumo wa elimu kwa ujumla na kushirikiana na taasisi zote kwa njia ya usawa ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa ya elimu bora.
Elimu bora na hayo matokeo hayaji bila uwekezaji, uqekezaji ni pesa. Ndio hapo shule za kidini zinapo ng'ara, wamefanikiwa kuboresha elimu ya internally , is why wanapata matokeo ya juu
Badala ya kuficha aibu, wengine wakajifunze huko wao wanafanyaje mpaka wana attain ubora wa juu