Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Moja ya Uchawi mkubwa watz waliorogwa ni kudhani serikali ni watumishi wa Serikali.
kufuatia matokea ya kidato cha nne, form four 2024 yaliyotoka 23/1/2025 inaonyesha shule za dini zinafanya vizuri sana, lakini ukiingia ndani zaidi unakuta ni dini fulani huku zini zingine zikiachwa nje .
Je, ni wakati muafaka kwa SERIKALI KUTAIFISHA SHULE ZA DINI ili kila mtoto awe na usawa kwenye kufaulu ama serikali iache kila dini ijiamulie ama ELIMU DUNIA ama ELIMU AKHERA?
Hapa kuna hoja muhimu:
1. Uhuru wa Kidini: Katiba ya Tanzania inaheshimu uhuru wa dini. Kutaifisha shule za kidini kwa sababu ya matokeo yao ya kitaaluma kunaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa uhuru huu tu.
2. Ubora wa Elimu: Mafanikio ya shule yanatokana na mambo mengi, kama vile usimamizi bora, walimu wenye sifa, nidhamu, na rasilimali. Badala ya kutaifisha, serikali inaweza kujifunza na kuboresha shule nyingine kwa kuiga mifano bora kutoka shule zinazofaulu.
3. Haki na Usawa: Kutaifisha shule za kidini kunaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na malalamiko kutoka kwa dini husika. Ni vyema kuweka usawa kwa kushirikiana na taasisi zote za kidini badala ya kuziondoa umiliki.
4. Ushirikiano na Sera Bora: Serikali inaweza kushirikiana na shule za kidini kwa kuweka sera zinazoweka usawa wa fursa kwa wanafunzi wote bila kuingilia umiliki wa shule hizo.
MDAU MMOJA KIJIWE cha kahawa hapa Posta Mtaa wa Mkwepu anasema badala ya kutaifisha shule, serikali inapaswa kuimarisha mfumo wa elimu kwa ujumla na kushirikiana na taasisi zote kwa njia ya usawa ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa ya elimu bora.
Ktk nchi yenye utawala wa kidemokrasia maana ya serikali ni Ummah. Ndio maana tunasikia shirika la umma, shule za ummah.
Sasa umma ni nani. Jibu rahisi umma ni sisi wananchi. Unauliza tena je umma una utamaduni mmoja. Jibu hapana. Ummah uko Diversity. Kwa maana tuna tofautiana ktk tamaduni.
tukirudi ktk kanuni moja ya demokrasia ni wengi hutunga sheria.
hata hivyo kwa kipindi kirefu tz zinaendeshwa kama jamii yenye utamaduni mmoja. Matokeo yake wale ambao wanalazimika kufata tamaduni za wengine wanashindwa kuperform.
Nini kifanyike. Kwanza kubadili mfumo wa utawala wa serikali na kuwa na mfumo wa utawala wa serikali za kanda zenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe.
Tukifanikiwa hili wale wasiopenda shule za kidini kwa kuwa zinafaulisha sana ukilinganisha na shule zinazosimamiwa wa watumishi wa umma na kwamba eti badala ya watumishi wa umma kwenda kujifunza kwa shule zinazofanyw vema kama kweli wako na dhamira njema, hawatokuwa na mamlaka za kufikiria kuzitaifisha shule za dini (utakaduni) wa wengine