Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Mkuu huzuiliwi kujifungia ndani,jifungie tu na familia yako tuache tukatafute mkate wa watoto wetu, total lockdown bila chakula ni zaidi ya corona mkuu tafadhari sana usishabikie lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungejibu maswali niliyokuuliza ungekua umesaidia sana.

Halafu nimewakumbusha munaposisitiza lockdown, muishauri pia serikali itakavyoitekeleza. Hili halihitajo kaulizi za jumlajumla kwamba tutakufa au ni uzembe. Kunahitajika solutions. Tuambie wale wamama kule kijijini wanaotembea km2 au 3 kufuata ndoo ya maji na kaunga sokoni wataishije? Nyie munaosema lockdown huenda ndani muna umeme na gesi na akiba ya mafuta. Tuambieni wale wanaosafiri kutafuta mkaa wa siku au kuni au mafutaa ya taa kwenye chupa, huko lockdown watapika na nini hata kama wakiwa na chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Total lockdown hapana,
Maduka yawe wazi hasa ya vyakula na dawa ,wahudumu wanawe kila wanapohudumia mteja mmoja Hadi mwingine,wateja wanawe kabla hajatoa pesa na wakati akishahudumiwa,
Kwa mijini usafiri Ni big challenge Happ ndo palipo na maambukizi kea 75%,watu watembee ama watumie baiskweli,
Congo street machinga,makoroboi waende likizo kwa mda,mle Ni mbanano huwezi kukwepa maambukizi na tatizo la virus inaweza kufuta hata mji mzima ,
Ni bahati tu strain ya virus waliopiga hodi Africa iko weak kuliko strain iliyoko Italy,watu wangekwisha vibaya
 
Asante mchambuzi kwa uchambuzi wako yakinifu
 
Hitimisho langu:

Nikisoma maoni, matusi, maonyo, hofu na taahadhari ya waotamani serikali itangaze total lockdown, hakuna hata mmoja anayetoa suluhisho au mbinu ya utekelezaje wake. Hakuna anayetoa data yoyote kiuchumi, kijamii, afya, nk. Hawatuambii watanzania wasio na maji, ajira, umeme, nk ambao wataathirika kuanzia siku ya kwanza ni asilimia ngapi na watasidikaje. Hoja yao ni moja tu, HOFU na watu wengi watakufa tusipotangaza Lockdown sasa. Hakuna scientific argument yoyote wanayotoa yenye ushawishi au theory and practices za crisis management or outbreaks control/response.

Kauli zao zinaonesha kifo kinachotisha ni cha Corona pekee. Vifo vitokanavyo na njaa, malaria, kipindupindu, kuhara, na utapiamlo (baadhi ya maradhi ambayo yatakumba wengi kukiwa na lockdown ya muda mrefu) havitishi wala sio tatizo. Tatizo ni Corona tu kwa madai kwamba tutakufa kama Italy na Spain. Wakati hofu hizi ni za msingi ila hazitakiwi kuwa msingi wa maamuzi na kufikiria kwetu.

Watu hawa hawaelevi bado inamaanisha nini hasa kuwa kwenye total lockdown. Hawatazami multiplying effect ya lockdown. Hawaelewi makampuni mengi yatafungwa na wafanyakazi watapoteza kazi. Hakuna mwajiri ataendelea kulipa mshahara watu wasiofanya kazi na yeye hazalishi. Hata makampuni yatakayooperate yatapunguza wafanyakazi kwa sehemu kubwa maana hakuna biashara. Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa sekta ya utalii wako majumbani hawana kazi na hawajui kazi itarejea lini. Waliobahatika kubaki na ajira wengine wameahidiwa wanalipwa nusu ya mshahara kwa miezi 3 au 5 wakati kisha maamuzi mengine yatafuata.

Kinachotokea na kitakachotokea zaidi, uwezo wa serikali kukusanya kodi utakua mdogo maana hakuna biashara; uzalishaji unapungua; PAYE itapungua maana watu wamepoteza kazi. Nchi yetu bado inategemea makusanyo ya kila mwezi kugharamia mahitaji muhim ya nchi kama kulipa wafanyakazi, kununua madawa, ulinzi na usalama, na kazi za utawala wa nchi.

Hivyo unapoishauri serikali kukimbilia total lockdown sasa na kwa muda usiojulikana (maana ndio tuko asubuhi mwa mlipuko), tuiambie pia itaendeshaje nchi. Kama hatuelewi complexity ya lockdown basi tuendelee tu kuisilikiliza kwenye vyombo vya habari kuliko kujiona sisi ni wataalamu wa utekelezahi wa total lockdown. Nirudie tena, huwezi kukimbia kung'atwa na mbwa (Corona) kwa kukimbilia walipo chui na simba (madhara ya total lockdown).

Namishukuruni waliosoma, waliochangia, waliokosoa, waliosahihisha, walioniita mjinga, na hata walionitukana. Wote wametumia uhuru weo kadiri ilivyowapendeza. Bado kuna mambo mengi ya muhim ya kuchambua na kujadili kuhusu Covid-19.

Mubarikiwe.

MM Togolani.
 

... kauli za jumla jumla tutakufa kizembe zimekuja baada ya baadhi ya watu na wewe kusema lockdown itatufanya tufe na njaa!??! njaa inaambukiza?? au huoni corona itakavyo cost Maisha ya watu...dabo dabo?? tunaosema lockdown sio kwamba ndani kuna vitu vya kutosha ndani..ila tunachukua tahadhari tuu kupunguza movements..badala ya kwenda sokoni mara nne unaenda mara mbili,haizuii kuambukizwa, ila rate ya chances za wewe kuambukizwa zinapungua….and ofcourse hatuwezi WOTE kujifungia ndani, kuna vitu necessary kuwa navyo,hata wale panic buyers kuna mavitu waliyonunua yataisha na itawalazimu kutoka nje na kununua tena..point yangu ni free movements kuzuiiliwa kasi yake ,hakutaondoa corona,bali ita control infection rate kipindi hiki ambacho bado hatuna matibabu/chanjo..

UK again sababu ya pili maambukizi yanaanza ku slow down ni baada ya kufanya lockdown,(sio total)kwangu mimi imekua sababu ya pili baada ya social distance, sasa kama kuna observable results zinazoonyesha kupungua kwa maambukizi following certain intervention, huoni is important to deploy such intervention to our country?

Mimi nitamshauri Rais wetu....

1. lockdown miji yenye misongamano mkubwa wa watu; Mfano Dar sio tu watu ni wengi,bali kuna movements nyingi sana,wafanya biashara wanaosafiri kwa vyombo vyote-wengi wapo Dar..hii inaongeza risk za maambukizi....

2. Ni kupiga campaign, watu wabaki nyumbani .. LOL...ni hayo tu mheshimiwa.. LOL
 
Mkuu je kuhusu hizo hoja za mtoa mada
Sielewi pointi yako ni nini
haeleweki huyo, hajajibu hoja zaidi ya kuzunguka tu
 

Rebeca 83 Nikushauri kama utaona ni vema. Unapoongelea hoja za kisayansi jitahidi kuzijadili kwa evidence ya data. Usiotoe kauli za jumla. Kwa mfano, unaweza kutuonesha data za UK zinaononesha maambukizi yamepungua? Mimi ninazozitazama hapa hazioneshi hivyo. Hizi hapa.





 
Mkuu naona hiyo sio sababu ya kutofanya lock-down umasikini usitufanye tukose maarifa ya kupambana na hili janga la covid 19.....kwanza umasikini wa Tz sio wa leo au jana ni sehemu ya maisha yetu tumesha zoea tutajua jinsi ya kuishi, hamna mtu atakae kufa na njaa hizo ni propaganda za kipumbavu sanaa......ili badaye serikali ilaumiwe kwa kutojali wana nchi wake dhidi ya ungonjwa leo Tz wanaiona kama kituko kwa kutochukua hatua dhabiti kuhusu hu ugonjwa..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwenye makala yangu na kote nilikojibu watu, sina hakika kama kuna mahali nimetumia neno UMASKINI. Ukisoma kwa tafakuri tunduizi utaelewa ni kwa nini. Pili, toa data za kuonesha namna ambavyo mumewahi kuwa na lockdown halafu mukaendelea kuishi na ilikua ni ya muda gani.
 
My kaka naona hatuelewani, na moja ya sababu ni kwamba huelewi kwamba lockdown inasaidia ni ku protect MAJORITY ya watu katika jamii..na kufanya hivi kutacost lives za WACHACHE .sasa wewe unapigania tofauti ; watu WACHACHE wawe protected Majority wafe...mfano wako wa huyo mama wa kijijini..unge quantify jinsi ambavyo anaenda sokoni na kuambukiza ama kuambukizwa na kuiletea familia yake maafa, ungeona kwamba asingeenda sokoni ama akapunguza safari za sokoni kuna ka cheni hapo angekua amekakata, Hii ni scenario inaonyesha jinsi hili swala lisiangalie upande mmoja tu wa mtu mmoja mmoja,bali angalia jamii kwa ujumla….


Kujibu mliosema hamuogopi Corona sababu kukaa ndani, sijui mahitaji yenu nini..na pengine hili haliwashtui...mna matatizo kibao ya kudeal nayo,malaria,typhoid mmeshazizoea..na hamtakaa nyumbani..naomba tu kuwaambia jamani. NDIO TUNA MATATIZO MENGI,ila KUJA KWA CORONA , hakupunguzi ama kureplace matatizo tuliyonayo!!!...ni kwamba unaweza kuwa na malaria, kipindu pindu..na corona inakuja ku complicate mambo EVEN MORE!!!..hamtakua na ugonjwa mmoja wa ku deal nao….choices zinabaki kwenu!!!!!

Lastly tutakua wajinga kama tunaona yanayoendelea duniani halafu hatuchukui hatua….Coronavirus: UK should have gone into lockdown 10 days ago, Italy's scientific adviser warns

Ni kweli niliona mahali infection rate ya corona Virus inapungua UK, nimeshindwa ku locate hio article.japokuwa vifo vimeongezekaThe lockdown looks to be reducing the number of people infected

UK coronavirus infection rate slowing due to lockdown, scientists say

'Confinement is working' – New analysis shows Spain's coronavirus lockdown having effect as long-term infection rates fall - Olive Press News Spain

Coronavirus measures may have already averted up to 120,000 deaths across Europe | Imperial News | Imperial College London
 

Nikurudishe palepale unapokwepa. Zaidi ya haya maelezo yako ya jumla, ni sayansi au theory gani unayotumia inayokuambia lockdown inazuia watu kufa au itazuia watu wengi kuambukizwa? Na itakua kwa muda gani?

Mbili, hii hoja ya watu kufa wote wakiambukizwa unaitoa kwenye data au utafiti gani? Unaweza kutupa data zinazoonesha watu wote wanaopata corono wanakufa? Crude Mortality Rate and Mortality Rate ya Covid-19 ni kiasi gani na tafsiri yake ikoje? Unaitafsije kwa conetxt ya kila nchi?

Inarahisisha sana ukijibu CLAIMS za kisayansi au kitafiti kwa data.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndo uandishi mzuri unatakiwa kuwa hivi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…