Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi

Asilimia 60 ya vifo Afrika vinatokana na magonjwa

Mtoa maada. Kwa takwimu za mwaka huu, Africa katika vifo vya watu 100, basi watu 60 wamekufa kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukizwa. Tafsiri yake inamaa kwamba kuna kundi kubwa tu la watu ambao wanatembea lakini afya zao ni mbovu hasa ukizingatia huku africa watu hawana utaratibu wa kwenda hospitali kufanya check up.

Na ukiangalia hao watu 60 utakuja kuona pia asilimia kubwa hapo ya hivyo vifo ni magonjwa ya moyo.

Hili la watu kuwa na magonjwa itafanya corona iuwe watu wengi huku africa kuliko hata tulivyoona kule ulaya.

I swear kama corona ikienea Dar kwa mfano, 1/3 hadi 1/2 ya population inaweza kuwa wiped out.

Africa watu wanakula kama Nguruwe, hata hawajali afya zao.
 
Wewe si unakula na kulala nyumbani alikoolewa dadako, kwahiyo huna unalofikiria.

Hapo penyewe una coment ukiwa umejilaza kwenye kochi la sebuleni kwa dadako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah umenifanya nicheke hadi majirani wamesikia

Hawa watu wanaolelewa hayajui hata ndoo ya maji inauzwaje ndo wanaachama midomo ukute na siasa zishawaingia wanaona wao wanajua kila kitu,,,akikua atajifunza mwache aendelee kulala kwenye sofa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dish lako linayumba wewe,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Togolani, you are missing the point, dhumuni la msingi la Total lockdown sio kuzuia Covid 19, ni kupunguza rate ya maambukizi. Point hiyo tu imenifanya nikuone hujui unachokitetea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi dada unaamini kuwa Togolani atakuelewa, mtu ambaye hajui hata dhana ya Lock-down, anasema nia ni kuzuia COVID 19, mtu kama huyu siwezi kupoteza muda kuongea nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mbona unawavamia watu tu hata pasipo kuwajua, ukifikiri wana ufahamu wa chini kama wewe...huyo ni Mwandishi wa Hotuba za Rais mstaafu mind you, ni Mtu ana akili kuliko wewe[emoji3]
Macka, be serious, mtu akiwa mwandishi wa hotuba za rais ndio ana akili kuliko watu wengine.

Wapi uliona kazi hiyo ilitangazwa wakajitokeza watu kisha interview zikafanyika na the best candidate akapatikana. Hizo ni kazi za kupeana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama lengo ni beyond what you see, you can not stop it. Wewe fuata masharti tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barikiwa sana mkuu nimeipenda makala yaki mpaka basi.
 
Nakushauri tafuta data toka sources sahihi. Habari za magazeti sio reliable sources kwenye jambo nzito kama hili unalizungumzia. Hawa wakati mwingine wanaandika kwa lengo la kuuza tu. Kama huwezi kupata nijulishe nikutumie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha, hapo "hata ya kimila" nimefurahi sana
 
nimeshindwa kusoma haya maelezo malrefu au kwa kuwa ana kazi amejifungia ndio anaandika gazeti
 
Mkuu umeandika ''nitajihu'', nadhani tu tuelewe kwamba makosa ya kiuandishi ni mambo ya kawaida tu kama ujumbe unaweza ukaeleweka.

Ndugu ndio walewale,
Nashukuru sana kuliona hili. Ndio mana napata shida sana mtu anapotumia muda mwingi na nguvu kubwa kuacha kujadili mada anajielekeza kumshambulia mwandishi aliyekosea lugha, neno au herufi. Tena unafanya hivyo kwenye social media ambapo hakuna peer-review process nor proofreading as a prerequisite requirement for posting.
 

Asante sana ndugu ndio walewale . Natamai ungejitokeza mapema unisaidia kujibu hizi hoja.

Tatizo watu "wanaotamani na kulilia" lockdown, wanaona anayetofautiana na matamanio yao ni kwamba ataka watu wafe au hataki tujikinge. Ndio mana hawajibu hoja za nini kitatokea kwenye lockdown wala hawatoi pendekezo lolote la namna ya kuitekeleza. Wanachojengea hoja zao ni hofu ya watu kuambukizwa na kifo pekee. Wanasahau ule msemo wa kiswahili wa "kuruka nanihii na kukunyaga naniliu" (siyajui hayo maneno).

Nimebahatika kutembea karibu Tanzania yote hasa miji midogo na vijijini. Sioni kabisa ni kwa jinsi gani lockdown inatekelezeka. Wale waliobahatika kuzaliwa mijini kwenye mazingira mazuri au yenye huduma muhim kama Mikocheni, Osterbay, Njiro, Masaki, Area C, Mtaa wa Uzunguni au Shanti Town; wakasoma shule za kueleweka; na sasa wana maisha mazuri, wanaweza wasielewe kwa nini lockdown haitekelezeki. Kuna maisha ya walio wengi hawayafahamu.

Hatupingi kuzua ugonjwa na hatutaki watu waambukizwe kwa wingi. Ila hatuwezi kutekeleza hilo kwa kupuuzia hali halisi na kusababisha janga juu ya janga.

MM Togolani
 

Huwa ninashauri sana tusitaje evidence za nchi zingine kirahirahisi kwa kutegemea unachokiona kwenye news. Hakuna nchi duniani imekabiliana na Covid-19 kisayansi kama UK. Kila hatua wanayoichukua ina backup kubwa sana ya sayansi na tafiti. Kila siku wanapotoa briefing, hoja na maswali mengi yanajibiwa na mshauri mkuu wa serikali wa sayansi (chief governemnt scientifc adviser) na mganga mkuu wa serikali (chief medical officer). Ukimtazama Trump utaona pia kazungukwa na kundi la wanasayansi na wakati mwingine wanabishana naye kabisa kuhusu hatua za kuchukua. Hivyo mtu awe makini anaporejea hizi nchi kuhusu application of research, science and knowledge in decision making preocess.

Kitu kimoja lazima uelewe ndugu mulwanaka . Tunaposema kutumia scientific evidence haimaaishi watu wakafanye tafiti ndio zije zitumike kutatu tatizo. Hapana. Tunamaanisha kufanya maamuzi au kuchukua hatua kuongozwe na taarifa na thinking za kisayansi ambazo ziko informed. Watafiti na wanasayansi hawaitwi hivyo kwa sababu wanakesha field kufanya tafiti na kujifungia kuandika papers. Pamoja na hayo, maisha yao wanafanya kazi ya kurejea na kuchambua maandiko na tafiti nyingi sana. Ndio kazi yao. Hivyo kichwani wana ufahamu mkubwa wa mambo mengi based on volumes of literature consulted, ideas, theories, etc. Wana uwezo wa kuunganisha mambo mengi kutafuta solution ambayo imetazama angles nyingi ambazo mtu mwingine asiye mtafiti/mwanasayansi hata kama amesoma hawezi kuona.

Ili unielewe namba nikuulize maswali marahisi. Wewe umesoma papers/tafiti ngapi za crisis/emergency management and response kwa miaka 2 iliyopita? Umesoma ngapi ngapi kuhusu epidemics surveillance and response or diseases control?

Njia rahisi ya kuelewa ninachofafanua hapa ni kujiuliza kwa nini pamoja na kwamba sote tunaweza kusoma Biblia au Kuruani au kitabu kingine chochote kile cha dini wenyewe, lakini bado tunakwenda kwa watumishi (wachungaji, mapadri, waalimu, mashekhe, maimamu, nk) kutafuta ushauri au msaada wao wa kiimani? Ni kwa sababu tunajua kwamba uelewa na ufahamu wao kuhusu imani na kila tunachokiamini ni mkubwa. Tofauti na waumini wanaosali au kusoma neno mara moja moja, wao wana muda mwingi kuomba, kutafakari, kusoma, kusikiliza na kuchambua mambo yahusuyo imani. Wamekutana na maswali na changamoto nyingi za kiimani na wanajua nini kinafanya kazi vipi, wapi, kwa nani na kwa nini.

Tungelijua hili tungeheshimu sana sayansi na fikra za wanasayansi wanaotushauri badala ya kubishana nao.

MM Togolani
 
Nilikuwa nimelewa jana ndio maana nikaomba hivyo na bahati mbaya nikakosea!Kuna typing error na syntax error,i hope umeelewa!Naomba niulize,hivi hangover iking'ang'ania unatumiaga nini kupata nafuu?
Hahahaaaa Tigershark
Mbona wewe hukumuuliza kwanza MM Togolani iwapo aliandika akiwa kalewa, kwenye hangover au kwenye daladala, hivyo ikawa sababu ya yeye kukosea?
 
Mkuu yamepita!Sasa ngoja nitulie kidogo hangover iiishe nitakuja na mchango wangu kwenye hii hoja!

Ila kulewa sio jambo jema kabisa hasa kipindi hiki cha Corona. Unaweza kujikuta umebusu watu bila kujijiua ukaondoka na virusi halafu huku unataka sisi tukawekwe lockdown.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…