DOKEZO Serikali isipoingilia kati, kuna siku yatatokea Maafa ya kutisha Mbagala

DOKEZO Serikali isipoingilia kati, kuna siku yatatokea Maafa ya kutisha Mbagala

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hawa ni wamachinga wakifanya biashara zao barabarani bila kujali hatari inayoweza kutokea.

Ni kweli kwamba kila Mmoja wetu ana haki ya kujitafutia riziki, lakini riziki ya namna hii yaweza kuleta Maafa ya kukumbukwa milele.

20231025_174811.jpg
20231025_174814.jpg
20231025_174838.jpg


Baada ya Maafa Chalamila ataunda Tume ya Uchunguzi .
 
Wewe ni mpotoshaji sana!

Hapo wapo kwenye barabara ya mwendo kasi ambayo bado haijaanza kutumika.
Hivi we umewahi kwenda Mbagala mbona watu hovyo namna hii, anapotosha nini? Mbagala Zackiem hadi Rangi 3 kwote wafanyabiashala wametapakaa barabarani foleni haiishi yamagali pale iwe j3 hadi j2 foreni yani kutoka Zackiemu hadi Rangi 3. unaweza kutumia saa zima sehemu ya umbali mita kama 400 tu.
 
Waache! Magari yakianza kupita watatafuta sehemu nyingine ya kupayia riziki zao.

Leo hii unakaa tandika?

Si ulisema hizo ni sehemu za watu masikini?
Labda kama umejitoa akili , siku zote nikiwa Tanzania ninaishi Tandika Mwembeyanga au Kyela Kajunjumele , lakini sijawahi kuwa kapuku .

Jifunze kuwa na adabu , sisi ni viongozi wako wajao , usitukanetukane hovyo
 
Wewe ni mpotoshaji sana!

Hapo wapo kwenye barabara ya mwendo kasi ambayo bado haijaanza kutumika.
Kama ungekuwa unaishi maeneo ya huku usingesema haya Maneno, sijawahi kuona sehemu ambayo serikali imelala kama Jimbo hili la mbagala ni UJINGA unafanyika kwenye maeneo yote kama hapa rangi3 ni eneo ambalo biashara zinafanyika ndani ya barabara na ukipita muda wa jioni magari yanapita mojamoja kwenye lanes mbili
 
Hawa ni Wamachinga wakifanya biashara zao barabarani bila kujali hatari inayoweza kutokea .

Ni kweli kwamba kila Mmoja wetu ana haki ya kujitafutia riziki , lakini riziki ya namna hii yaweza kuleta Maafa ya kukumbukwa milele .

View attachment 2792653View attachment 2792670
Labda tuseme hawakuanza leo au mleta mada ndio umefika leo mjini na gari la maspika +255 kutoka songwe!
 
Back
Top Bottom