Wewe ni mpotoshaji sana!
Hapo wapo kwenye barabara ya mwendo kasi ambayo bado haijaanza kutumika.
Unamtukana bure huyu mleta uzi...kimsingi wafanyabiashara wa Mbagara wengi wao hufanya biashara barabarani kiasi kwamba, magari na vyombo vyengine vya moto hulazimika kutumia njia moja badala ya mbili. Kwakusema ukweli mbali na usumbufu wanaouleta kwa watumiaji wa barabara lakini pia usalama wa wafanyabiashara hawa na watembea kwa miguu upo hatarini.
Kwa upande wangu nadhani, kuna umuhimu wa serikali kuandaa utaratibu mzuri zaidi ili kuondoa changamoto hii. Kwa ujumla, katika eneo hili kuna watu wachache wenye nguvu ni kama wamejianzishia utawala wao. Kikundi hiki cha watu wachache, hukusanya ushuru na kodi kutoka katika vizimba vya wafanyabiashara. Kwa mfano, ile kona ya zamani kuelekea Charambe, pale kila meza ya biashara unayoiona tena ipo barabarani hulipiwa kati ya 3000 hadi 5000 kwa siku (fedha hizi huingia mifukoni mwa watu wachache)
Aidha, Kikundi hiki cha wachache waliojipa madaraka (Godfathers) ndio huwahakikishia ulinzi na usalama wafanyabiashara hawa kwa kutumia sehemu ya fedha wanazokusanya kuzuaia hatari yoyote inayoweza kujitokeza. Kwa mfano, serikali ilipoamua stendi ya magari ya kusini ihamishiwe kijichi, Kikundi hiki kilitumia ushawishi na nguvu walizonazo stendi iliweza kurudishwa Mbagara. Aidha, watu wa Mkuranga walikaribia kunufaika na mvutano huu, hadi kufikia stendi yao (Mwandege Azam) kupata magari mengi sana. Lakini, lilikua suala la muda tuu kabla stendi kurudi Mbagara.
Soko zuri limejengwa pale Zakhem lakini hadi sasa wafanyabiashara wanasuasua kuhamia. Za ndaaani zinasema kwamba, kikundi hiki cha wanufaika wametengeneza mazingira ya kutofunguliwa na hatimaye kutumika (kumbuka kuna kiongozi alikuja kwa ajili ya ufunguzi bila mafanikio).
Sina shaka juu ya utendaji wa Serikali hususani vyombo vya ulinzi na usalama (Ni Imani yangu kwamba, vyombo hivi vimeweza kupandikiza watu kwaajili ya kuendeleza tunu yetu adhimu ya usalama na amani). Lakini wasiwasi wangu ni kwamba, ikiwa vikundi vya namna hii vikiendelea, basi ushawishi wa vikundi hivi unaweza kuhatarisha usalama wa amani.
Katika hali na mazingira tuliyonayo, baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa hili wanaweza kutumia vikundi vya namna hii kuhatarisha usalama wa nchi. Hivyo basi, Serikali iendelee kuwa macho na hai wakati wote ili kuzuia mambo ya namna hii kutokea. Aidha, Serikali iwekeze nguvu kubwa kuhakikisha kwamba, biashara hazifanywi katikati ya barabara.