#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Naunga mkono sana hizi suggestions

Na kwa wale ambao wanasema TZ hakuna corona, haijalishi, Dunia ina Corona basi chukulia hizi hatua kama precautious au tahadhali

Hakuna utakachopoteza
 
Tanzania hakuna corona. Tuongeze uzalishaji wa mazao ili tuwauzie hao wenye kuteseka na nafaka kwa sasa maana hawatakuwa na chakula mwakani
Hata kama brother

Unaweza ukawa huna ukimwi lakini unavaa condom

Kinga ni bora kuliko Tiba

Hizi steps ni Bure kabisa

Piga batakoa, punguza kubanana, ukiumwa homa tullia home au vaa barako

shamba bado unaenda na kazi bado inapigwa

Simple
 
Kuchukua tahadhari peke yako hakukusaidii kitu.

Hii kitu inataka jamii mzima as whole ichukue hatua za kujikinga View attachment 1682937
Hii picha ina mislead kidogoo:

Kwani mtu akisambaza mate kwenye ukuta au meza na wewe ukaguss unaweza ukapata vimelea.

Hasa hasa baada ya kughsa sura.

So kuwa makini sana na kugusa sura na surfaces tha vitu...

Nawa mikono sk 20 kila utakapoweza..
 
Hii kitu kwa kweli ipo sana tu, juzi Kuna mtu wangu wa karibu amepoteza Dada yake kama masihara, ndani siku kama 3 alikuwa analalamika kifua na koo juzi akazidiwa kupelekwa hospitali doctor akasema ana shida ya upumuaji,akashauru awekewe mtungi wa oxygen ndani ya masaa 4 akavuta...
Mmebaki kusema MTU WANGU WA KARIBU kama ni kweli kwa nini usianike ukweli hapa jamii ielewe.

Hii kauli ni dalili tosha kuthibitisha umbea!
 
Naunga mkono hoja. Tusisubiri hadi watu wengi wafe ndio tuanze kuchukua hatua. Tuache kuishi kwa mazoea
 
Mwingine anakwambia alikuwa anajisikia mafua na kikohozi amekwenda hospital wamempima lakini wamemkuta Hana ugonjwa.[emoji16][emoji16][emoji16].Ila yeye anajua anaumwa Corona.
Hivi vitu vinachekesha sanaa.kuumwa Corona wao wanaona Ni fashion
Mmebaki kusema MTU WANGU WA KARIBU kama ni kweli kwa nini usianike ukweli hapa jamii ielewe.
Hii kauli ni dalili tosha kuthibitisha umbea!
 
Acha ushirikina wala hautakusaidia.Hapa sio Marekani.

Barakoa gani unaweza kuivaa ikakusaidia iwapo tu zile N95 zinazokubalika bei yake ni elfu 50,000 zile za kawaida hadi zaidi ya laki moja,na unaivaa masaa manne tu haifai.
Hizi za vitenge ni michezo ya kuigiza na huenda ndio zikasababisha ongezeko kubwa zaidi kuliko kutovaa.

Mungu alitupigania tangu mwanzo hatuna sababu ya kuwa na hofu kwani kifo kipo na kila mtu ataondoka kwa zamu yake.
 
Mmebaki kusema MTU WANGU WA KARIBU kama ni kweli kwa nini usianike ukweli hapa jamii ielewe.

Hii kauli ni dalili tosha kuthibitisha umbea!
Mjomba tema mate chini, hivi kuna mtu a anapenda kutania kuhusu kifo
 
Goma lipo kitaa,wabongo acheni ujinga....jikingeni.
Jamaa katonywa DOM hali tete kakimbia...
 
Back
Top Bottom