UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Mbona malaria inauwa na hakuna anayebisha mkuu au kwamba kila mtu aliumwa na malaria?Corona ipo watu hamuamini mpaka yawakute.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona malaria inauwa na hakuna anayebisha mkuu au kwamba kila mtu aliumwa na malaria?Corona ipo watu hamuamini mpaka yawakute.
Mwanzo ilikuwa vifo vya corona vinatangazwa na idadi ya wagonjwa hutangazwa, ila sasa hawafanyi tena hivyo sasa unategemea utapataje uthibitisho kuwa ipo au haipo?Hakuna vifo vilivyothibitishwa kua vimetokana na corona hata mimi na watu walionizunguka hakuna hata dalili ya corona miongoni mwetu sijui
Hapa kinachoongelewa ni juu ya Covid19 na sio malariaMbona malaria inauwa na hakuna anayebisha mkuu au kwamba kila mtu aliumwa na malaria?
Yote ni maradhi ndio maana nimetoa mfano huo kuwa sio mpaka mtu aumwe malaria ndio aweze kujua kuwa malaria ipo na inauwa,sawa na corona kama corona ipo basi sio mpaka mie niumwe ndio niweze kujua ipo.Hapa kinachoongelewa ni juu ya Covid19 na sio malaria
Acha kuongea kama fala nina uchungu sana hapa nlipo mmoja wa family members wangu kaipata hii nlikuwa sitaki kuamini kama Corona ipo but wanasema mdharau mwiba humchomaKabisa mkuu vyuoni kuna misongamano mikubwa mno isiyofuata tahadhari yoyote full kukumbatiana na kisses kibao kwa wapendanao
Achilia mbali makanisani kwenye vyombo vya usafiri, masokoni mbona watu wangeanguka sana kama kweli ingekuepo .
Pole kwa kupoteza mpendwa wako mkuu na siongei kama fala naandika ninachokiamini usitake niamini uaminivyo mkuuAcha kuongea kama fala nina uchungu sana hapa nlipo mmoja wa family members wangu kaipata hii nlikuwa sitaki kuamini kama Corona ipo but wanasema mdharau mwiba humchoma
Magufuli ameshamsifia balozi wa china kwa kutovaa barakoa.Jamani kwenye hili swala la Corona nipo na Magufuli. Nyie mnaolalamika mmekatazwa ku take precautions? mmeambiwa msinawe mikono au kuna mtu amekatazwa kuvaa barakoa? Hebu kama mmepewa neema ya kutougua na hamuugui why kelele kelele kila siku mara ooh ugonjwa upo,Yess ugonjwa upo lakini una impact kubwa kama mnavyosema?.mnataka aitangazie nchi kuna corona watu wafe kwa presha?.watu wakose amani na kujifungia? sasa kwa taarifa yenu watanzania tuna survive kwa sababu ya huu muingiliano tunaopata kila kisu kati ya watu na watu tuna exchange virus tunaugua mwili unajenga immunity zake. Hizi shughuli za kila siku tunashinda juani ni tiba tosha. Hatuna hofu hii ni tiba kubwa kabisa kuliko ku declere kuna janga na kuleta mtafuruku. My take:; Kirusi hakifi kirahisi dawa yake ni kuufanya mwili wako uweze kupambana nacho tule vyakula vya kuongeza kinga mwili.
Siishi dunia ya peke angu mkuu naishi na nachangamana na binadamu wenzangu likitokea jambo na mimi ni rahisi kuhusishwa na kujua kwa maana iyo sasa toka corona imetoweka nchini sijaskia kisa chochote kihusianacho na huo ugonjwaMwanzo ilikuwa vifo vya corona vinatangazwa na idadi ya wagonjwa hutangazwa, ila sasa hawafanyi tena hivyo sasa unategemea utapataje uthibitisho kuwa ipo au haipo?
Tatizo ni kufikiri serikali ni viongozi hata wewe na waandishi humu ndani ni sehemu ya serikali, kuna njia mbalimbali ya kutoa taarifa. Tahadhari ni muhimu kwa kila ugonjwaKuna watu wanasema kuwa ishu ya Afya ni personal issue, kwamba wewe raia wewe mwenyewe chukua tahadhari!, ni sahihi kwa upande mmoja lakini siyo sahihi kwa upande mwingine kwa sababu kazi mojawapo ya serikali ni kuwa wakweli na kuupa umma information sahihi kuhusu hali ya situation ili hao raia wachukue tahadhari husika.
Ukisema korona ipo chukua tahari wewe mwenyewe ni sahihi, LAKINI SWALI LA MSINGI NI JE, WATANZANIA WANGAPI LEO HII WANAJUA, AU WANAAMINI KUWA KORONA IPO TANZANIA?
Serikali ilishatangaza ushindi dhidi ya Korona kitambo sana na ikaacha kutoa information zozote juu ya hali ya korona nchini na raia wengi wanaimini serikali yao kuwa korona haipo na hawachukui tahadhari yoyote.
Hapa ndo tunaitaka serikali itoke mafichoni iseme, Hapa Tanzania hii kitu ipo au haipo ili wale raia wanaoamini Tumeishinda Korona wasijiachie sana!
Mkuu kilitumika kipimo gani kuweza kujua kuwa corona imetoweka? kwa sababu nachojua serikali iliacha kupima na kutoa takwimu katika kipindi ambacho corona ndio imepamba moto.Siishi dunia ya peke angu mkuu naishi na nachangamana na binadamu wenzangu likitokea jambo na mimi ni rahisi kuhusishwa na kujua kwa maana iyo sasa toka corona imetoweka nchini sijaskia kisa chochote kihusianacho na huo ugonjwa
Rais kila mara anawatangazia watu kuwa Tanzania hakuna korona.Unataka kuambiwa na nani na mara mgapi kwamba ugonjwa upo, swala la kujilinda ni la mtu binafsi.
Chukua tahadhari kama ichukuliwayo katika magonjwa mengine, malaria, ukimwi, kuhara bila kuzua HOFU.
Inakisiwa vijirusi vinabadilikabadilika, inamaanisha hata maambukizi, dalili na hata ukali wake unatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Pia haijatambuliwa madhara yake ya muda mrefu yatakua ni nini kwa aliyeugua katika mfumo wa mwili.
Ni ujinga kufikiri kuwa matokeo ya ugonjwa ni kifo. Kila ugonjwa una mlango wa kutokea ikiwa ni pamoja na kupona, kupata kilema na kifo kama tokeo. Kufikiri katika Hofu ya kifo tu ni matumizi mabaya ya akili.
Pole kama ulinusurikaHii kitu (COVID-19) imenilaza hospital kwenye oxygen for 3 weeks December 2020
Hiyo ya corona, hapana!Ikifika zamu yangu. Tayari watu milioni 6 wamechanjwa Marekani.
Wewe hutaki chanjo? Hujawahi kuchanjwa?
Hujalazimishwa.Hiyo ya corona, hapana!
Wasiotumia condom na chandarua wako wengi pamoja na kujua kuwa kuna ukimwi na malaria,ukiangaloa sasa hivi jinsi ukimwi unavyochukuliwa ni kama wanadharau ukimwi sasa wakiambiwa hakuna ukimwi ndio kabisa.Tuache lawama zisizo na msingi kwa mtu au taasisi. Muda huu tukiambiwa hakuna Ukimwi na Malaria tutaacha kutofanya ngono zembe au kutumia chandarua?
Jilinde na walinde na ndugu zako.
Kila kitu kimeainishwa katika miongozo ya wizara ya Afya. Tuna vyombo vya habari. Kutokutimiza wajibu kwa kila mmoja wetu ndio kutatuletea majanga
Ukiangalia miji na nchi zinazoumia ni zile zenye miingiliano mikubwa ya wasafiri.
Nimeona nyuzi nyingi humu zinaelezea uwepo wa corona Tz kwa habari za kusikia tu kwa watu zenye et et nyingi zisizokua na uhakika. Acheni kuleta taharuki nyie watu corona Tz haipo na watu hawajaanza kufa leo wala jana pia kwa hao wanaokufa hakuna uthibitisho wa kidaktari kua wamekufa kwa corona ni hisia za nyie wapenda hofu zisizo na msingi tu.
CORONA HAIPO NCHINI
Nawasilisha
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.
Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.
Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.
Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc
Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo
Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc
Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.
Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!
Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.
Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?
Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?
Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?
Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata
Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!