#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
rubbish
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
 
Corona hebu tembelea viongozi wakuu wa nchi..waguse kama wawili watatu hivi ili waamini kwamba wewe upo na umekuja kivingine this time.
 
Mkuu

Korona unaona mbaya nchi za jirani sababu wanapima na kutangaza

TZ hatujapima tangu mwaka jana mwezi wa tatu mpaka leo

Pia serikali ilikataza kutangaza habari zake

Hivyo ni wazi unaona TZ hakuna tatizo maana hakuna kupima wala kutangaza

Nadhani mnajidanganya and you know it....

Tuseme tuwafate mkitakacho,hakuna korona,are u happy bums?
Mie siseme kuwa Tz hakuna corona bali mimi nahoji tu maana kila mtu anasema lake. Kama kuhusu kupima watu humu wanasema kuwa huko hospitali wagonjwa wanapimwa corona ukiacha na kule mabibo watu wanakopima kwa ajili ya kutaka kusafiri,ila tu hawatoi takwimu.
 
Corona hebu tembelea viongozi wakuu wa nchi..waguse kama wawili watatu hivi ili waamini kwamba wewe upo na umekuja kivingine this time.
Yani unachokisema hapa ni sawa kwamba wewe unajua kuwa corona ipo ila hao viongozi wa nchi ndio hawajui kama corona ipo kwamba hadi wafe wenzao.
 
Chukua tahadhari wewe na mkeo tu
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
 
Sasa hivi kuna wimbi kubwa la watu wanaofariki kwa ugonjwa wa Pneumonia akiwemo msanii almaarufu kwa jina C-PWAA zamani uhuni na uongo ulikuwa unafanywa na mtu mmoja mmoja ila awamu hii serikali inakuwa inafanya uhuni na utapeli kwa level za taifa na kimataifa.
 
Pneumonia inafanana dalili zake na za corona,sasa sijajua wanadanganya kusingizia pneumonia au sie tukisikia pneumonia katika kipindi hiki cha corona tunaona itakuwa ni corona ila tunadanganywa pneumonia.
 
Askofu Bagonza naye alisema kuwa Karagwe vifo vya watu kwa ugonjwa wa kushindwa kupumua vinaongezeka
 
Ishu ya corona chagua wa kumuamini Kati ya mwanasiasa au mtaalamu na umfuate
 
Kunaumuhimu chadema waazishe oparesheni tokomeza korona harafu waje na mifano ,mana hii mifumo upumuaji kufeli sio mchezo
 
Mambo haya yanaibuka tena baada ya uchaguzi kuisha,tatizo bongo siasa tumeweka mbele sana hawa hawa wanaopigia kelele hapa za corona miongoni mwao ndio walikuwa wakishangilia nyomi za watu kwenye mikutano ya kampeni.
 
Ishu ya corona chagua wa kumuamini Kati ya mwanasiasa au mtaalamu na umfuate
Na kwanini uchagua kuamini?

Kama corona ipo na hadi majirani zetu inawasumbua kwanini ukubali kuamini mtu akikwambia Tz haipo? kwanini hadi mtu akuaminishe kuwa Corona ipo Tz na watu wanakufa wakati balaa la Corona linajulikana na wezi kuficha?
 
Mkuu kuna majirani zako wowote wamekufa vifo vya kutatanisha?
tangu nizaliwe sijawahi kusikia jirani yangu au ndugu yangu aliyefariki kwa malaria, je hicho ndio kiwe kigezo kusema hakuna malaria au malaria haiui!!!
 
Corona ipo tena umepamba moto, watu wanakufa sana sisi tumeamua kuendekeza siasa. Uliza madaktari wa Muhimbili na Mloganzila wakupe picha kamili
Ndugu zako wamekufa wangapi, mbona hamna anayejibu hili swali mnakwepa kwepa tuu na story za vijiweni??????
Kila mtu aweke data hapa tufikie conclusion, sio sijui maDR wa wapi wanasema bla bla. Mambo hayaendeshwi hivyo.
 
Sijui msanii C pwaa kafa kwa nn?

Tz zaidi ya uijuavyo
 
Ndugu zako wamekufa wangapi, mbona hamna anayejibu hili swali mnakwepa kwepa tuu na story za vijiweni??????
Kila mtu aweke data hapa tufikie conclusion, sio sijui maDR wa wapi wanasema bla bla. Mambo hayaendeshwi hivyo.
Nilipoteza shemeji yangu wa karibu na hii kitu na hapa tuna msiba wa Mama wa rafiki yangu mazishi keshokutwa. Kama wewe hujaguswa, kaa kimya tu hutapoteza chochote. Tuendelee kuchukua tahadhari.
 
Back
Top Bottom