#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Mbona kama Cpwaa alikua amevimba mashavu? si kwamba alikua na matatizo yake mengine?.basi mtu akifa tuu siku hzi corona
 
Mbona kama Cpwaa alikua amevimba mashavu? si kwamba alikua na matatizo yake mengine?.basi mtu akifa tuu siku hzi corona
Ndio hayo ambayo mie nayasema humu,ukihoji unaambiwa Tz sijui sio kisiwa,kwahiyo kwa sababu Tz sio kisiwa basi ndio kila kifo kiwe ni corona.
 
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
Corona hakuna Tanzania wacha kuichafua inchi.

100% ya watu watokao Tanzania kuingia inchi za nje hawana corona.

Mfano,, baharia yeyote akiingia saudia lazima apimwe tena corona baada ya siku 14 lock down.

Lakini hakuna hata mmoja aliyekutwa covid 19 positive..
Na mabaharia wa Tanzania ndy wanaotamba kwa sasa ..saudia,Dubai.nk.
 
Kama unajua ni nini kinaendelea ndio ueleze humu watu nao waelewe na sio kutaka kuwaaminisha watu vitu kisa unaishi na madaktari utakuwa huna tofauti na waliyowaaminisha watu kuwa hakuna corona.

Kabla ya kuwepo corona tunajua mwisho wa mwaka huwa kuna ajali nyingi hutokea na husababisha vifo,sasa wewe unakuja kusema tu vifo vimeongezeka bila kueleza kwa kina wakati unajua kuna vifo vya ajali pia ambavyo havihusiani na maradhi ya corona.
Wewe Pimbi hebu acha kunipotezea muda kwani huna unachokijua na bakia na huo huo Ujuha wako kuwa Tanzania hakuna Deportivo la Corona.
 
Imeshangata family members au jirani zako wangapi?? Labda tuanzie hapo. Nadhani kila mtu aanzie kwa immediate family members na sio hadithi za sijui mtaani wanasema nini, kama mtaani ipo na familia zetu pia zipo huko huko mtaani so hawawezi ugua au kufa bila sisi kujua
Hii kitu ipo bro, tuache stori za mtandaoni, kujifanya tumeishinda corona. Desemba 13 tumepoteza dada wa jirani yangu hapa ninapoishi kwa matatizo haya haya ya kupumua. Usihitaji maelezo zaidi. Kikubwa ni kuendelea kunawa kwa maji na sabuni.
 
Wewe Pimbi hebu acha kunipotezea muda kwani huna unachokijua na bakia na huo huo Ujuha wako kuwa Tanzania hakuna Deportivo la Corona.
Kuna wajinga wa aina mbili,kuna mtu anafanya au hafanyi jambo fulani kwa sababu ya ujinga ila kuna wale ambao hufanya jambo fulani ili asionekane kuwa ni mjinga aonekane kuwa nae msoni ni mtu wa hadhi fulani. Ila kiujumla wote ni wajinga.
 
Hii kitu ipo bro, tuache stori za mtandaoni, kujifanya tumeishinda corona. Desemba 13 tumepoteza dada wa jirani yangu hapa ninapoishi kwa matatizo haya haya ya kupumua. Usihitaji maelezo zaidi. Kikubwa ni kuendelea kunawa kwa maji na sabuni.
Vifo vya matatizo ya kupumua before corona takwimu zake zilikuwa zikoje ukilinganisha na sasa?
 
Kuna watz ni wajinga sanaa, hivi mf jirani yako umasikia analia shamba lake la mahindi limeliwa lote na ng'ombe, je ww mashamba yako ambayo yapo mwanzoni kabisa yatakuwa yamepona kweli??? Au kwamba ng'ombe toka kuzimu walikula shamba la jiran lillilo katikat ya mashamba yako???

Chukueni hizo akili mlizoshikiwa mfikirie tu sec 30 jibu utapata.
Tusiwe nyuma kwa kila jambo aseee
 
Mkuu
Missile of the Nation
Issue ya covid-19 ni tete sana.
Watu kitaa wanasema, ila at the end of the day inabaki kuwa ni ishu yako na familia yako, serikali haitaki kuendelea na jitihada za kuwaamsha wananchi kuzidisha jitihada za kujilinda. Wale wasio na elimu na ufahamu wanaamini kauli ya serrikali kuwa Tanzania hakuna Korona na hivyo hawajilindi kabisa
 
Kuna wajinga wa aina mbili,kuna mtu anafanya au hafanyi jambo fulani kwa sababu ya ujinga ila kuna wale ambao hufanya jambo fulani ili asionekane kuwa ni mjinga aonekane kuwa nae msoni ni mtu wa hadhi fulani. Ila kiujumla wote ni wajinga.
Foolish!
 
Imeshangata family members au jirani zako wangapi?? Labda tuanzie hapo. Nadhani kila mtu aanzie kwa immediate family members na sio hadithi za sijui mtaani wanasema nini, kama mtaani ipo na familia zetu pia zipo huko huko mtaani so hawawezi ugua au kufa bila sisi kujua
Jumatano ilopita niliingia dukani mitaa ya clock tower kwa khimj ,then duka moja la nguo karibu na DIOMOND TRUST BANK.

WADOSI wote wamevaa Barakoa.

Nilipolipa bundle la pesa noti,mara alipomaliza kuhesabu Akajisanitize !!

Nikasema hii ni nini?
Tuchukue tahadhari COVID 19 ni kama bado IPOIPO.
 
Hilo siwezi kulisemea. Lkn huyu marehemu jirani alikufa kwa corona, kwa mujibu wa madaktari. Kwenye proess zote, hatukuruhusiwa kuaga maiti.
Unajua kuna vitu vya msingi ambavyo ndio tulitakiwa tuvijadili katika mada hii ya corona ila bahati mbaya ukiuliza unaonekana umeaminishwa hakuna corona.

Mfano kama hapo kutokana na maelezo yako hayo ni kwamba kumbe bado sasa kuna baadhi ya misiba watu hukatazwa kuwaaga maiti kwa sababu marehemu alikufa kwa corona,mimi nilijua hili suala halipo tena,lakini pia kumbe vipimo vya corona huko hospitali vinaendelea kama kawaida na watu hukutwa na corona na majibu hutolewa.
 
Sasa bora wewe unaamini ipo ila unataka kila mtu apambane na hali yake ILA kuna watanzania wenzako mamilioni kwa mamilioni hawaamini kuwa korona ipo na hawana mpango wa kuchukua tahadhari. Kazi hii ya kuwaaminisha watanzania kuwa hakuna Korona anaendelea kuifanya Magufuli kila apatapo nafasi ya kuongea na umma
 
Back
Top Bottom