Wewe unaepinga upo kila mtaa, Kijiji na wilaya?
Watu Kama ninyi, ndiyo mnasababishaga watu kupigwa burn na mods maana unapiga tu shetani nini?
Sijapinga nimeuliza swali dogo tuu!!! Kama kila mmoja wetu anaechangia humu akitoa data kuhusu close family members tutapata picha halisi ya jinsi watu walivyoathirika. Nianze na mimi binafsi thanks God mpaka sasa sijasikia mtu wangu aliyeugua corona/pneumonia au hata homa kali tangu covid ianze.
 
COVID ipo na uzuri haichagui, hata hao wanaosema haipo inaendelea kuwafyeka tu Jamaa zao na wao hawana kinga wala exception kusema COVID haiwezi kuwafikia.
Ndio Maana wame ji isolate, Mbochi Tocha
jikinge Mwenyewe usiwangoje wakwambie
 
Immunity, not immunite
 
Covid ipo na uzuri haichagui, hata hao wanaosema haipo inaendelea kuwafyeka tu Jamaa zao na wao hawana kinga wala exception kusema Covid haiwezi kuwafikia.
Ndio Maana wame ji isolate, Mbochi Tocha
Jikinge Mwenyewe usiwangoje wakwambie
Wanaujua ukweli ila kwa kuwa wana ego, wako tayari kuilinda ego yao kuliko kuchukua measures za kulinda wananchi dhidi ya janga hili
 
Mleta mada ahsante sana. Hii kitu ipo aisee...Madaktari wanakuandikia Pneumonia au ARDS/ C19.
Tangu tarehe 26 /12/2020 - 6/01/2021 nilikua Hospital aisee na dada yangu. Ila inawezekana mimi ndiyo nilimuambukiza. MUNGU mwema tulipata huduma na kutoka hospitali ila watu walikua wanadondoka jamani.
Serikali isione aibu katika hili.
 
Kwani kuchukua tahadhari unasubiri hadi Magufuli akuambie?
 
Kuna rafiki yangu yupo morogoro amenipigia simu Leo kuniambia kuwa Corona ipo nichukue tahadhari

Mtaani kwao modeko wamezika mtu alikuwa na dalili zote za Corona alipokuwa hai.
Pana watu yafaa washatakiwe kwa kumisslead watu Ili wapotee Hali wao wamejificha majumbani kwao kukimbia corona,nani alikuambia sisi ni kisiwa.
 
Kweli kabisa, yani mtu anang'ang'ania vitu visivyo hata na hoja, hivi kuna mtu asiyejua corona ipo hapa duniani?
Kwangu naiona serikali ipo sahihi kabisa kupiga kimya.
 
Lakini njia za kujikinga na corona ni zipi hizo? Mbona hizi zinazofahamika duniani bado zinaendelea kuwaumiza watu?
 
Lakini njia za kujikinga na corona ni zipi hizo? Mbona hizi zinazofahamika duniani bado zinaendelea kuwaumiza watu?
Ndugu yangu, hivi kwa sababu wewe una uelewa unadhani wananchi wenzako hawa ambao majuzi tu katika baadhi ya mikoa walikuwa wanafundishwa na taasisi moja ya Taifa kubwa duniani kuosha mikono baada ya kunya nao ni waelewa kama wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…