Mabibi na mabwana kwamba sasa hivi:
1. Misibani Dar zaidi 90% ya waombolezaji wametupia barakoa,
2. Kutofungua majeneza kwa ajili ya heshima za mwisho inazidi kushika kasi,
3. Matumizi ya microphone kwa ajili ya matangazo mbali mbali misibani inaanza kuwa old fashioned,
4. Waombolezaji bila kukumbushwa wanaanza wenyewe kupeana nafasi baina ya mtu na mtu,
Kwamba haya yanatokea kwa wananchi kujiongeza wenyewe, hizi ni ishara za wazi kuwa wale waliokuwa wakipotosha ukweli kuhusiana na ugonjwa huu wanaelekea kugonga ukuta.
Itambulike kuwa hayapo mashindano ya kutafuta mshindi dhidi ya ugonjwa huu bali ni umuhimu uliopo katika kuyahami maisha ambayo kwa hakika ni adimu kuliko vyote.
Itambulike kuwa somo linalotufikisha huku tumelifahamu kwa bei kubwa sana. Yaani baada ya kuandamwa na vifo vilivyo husishwa na shughuli za mikusanyiko ya watu kama hii.
Tuliita changamoto za kupumua na tunaendelea kuvumbua majina mapya kila uchao.
Haisaidii kuukimbia ukweli au kusingizia sababu za vifo. Kwamba ni changamoto za kupumua, pneumonia, uzee, ajali, magonjwa mengine, kufa ni jambo la kawaida nk wakati ukweli unajulikana?
Ama kweli njia ya mwongo ni fupi na mficha maradhi asitegemee mwuujiza.
Pasipo na kuuvaa ujasiri thabiti kama ulioonyeshwa wazi wazi na baadhi yetu, kwa hakika hatuwezi kutoboa.
Mikusanyiko ya watu misikitini, magulioni, masokoni, kwenye ma ferry, mabasi nk ni lazima idhibitiwe.
Kwa kuwaacha wananchi hawa kujifunza wenyewe namna ya kujifunza "in this very hard way," wenye mamlaka mjiandae tunayo maswali mengi kwenu.
Maswali ya kuwa mlitaka serikali ifanyeje yameshajibiwa mno na kwa hakika kwa sasa yako very irrelevant.
Ninawasilisha.