#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Mabibi na mabwana kupeana ulio ukweli hata kama ni mchungu vipi ni jambo la msingi sana.

Haisaidii kuukimbia ukweli.

Kwa hakika hali ya ugonjwa huu ni mbaya sana labda kuliko hata maelezo. Niko Kagera kwa mazishi ya kigogo wa mahakama kuu Mwanza.

Nakutana na misiba zaidi. Itoshe kuonyesha hali hii:

"Bwana Tumsiime mmiliki wa zile shule maarufu Dar kafiwa na mama mkwe na pia shemeji yake ndani ya siku 2 tu."

Pole nyingi ziwafikie yeye na familia yake.

Alianza shemeji, akaenda kuzika na kurejea Dar. Juzi tena, mama mkwe aliyekuwa msibani kwa mwanaye naye kafariki. Amelazimika kurejea kwa mazishi tena.

Changamoto zile zile, watanzania wale wale.

Kwani mengine yapi ni mageni wapi?

IMG_20210216_033337_511.jpg


Ukweli mchungu, watu wanakufa sana na ugonjwa huu.

Maswali yangu ya msingi kwenye vita hivi nikidhani tuko sote, yamekuwa haya hapa:

IMG_20210214_214251_251.jpg


Sijapata majibu yake popote.

Ni wazi kuwa kudhani kuwa vita hivi vingepiganwa katika umoja wetu kama taifa, kama ilivyo kwingine, hakupo.

Basi wala isiwe taabu.

Rasmi sasa hapa tulipo ni kila mtu na lwake. Kila mtu ikiwamo serikali, sasa na apigane kivyake.

Kila mtu na achukue njia yake. Kila mtu achukue mzigo wake. Tuachane njia panda.

Kama binadamu mwenye kuwajibika na familia yangu, nami ninachukua njia yangu japo nikiwa nimechelewa sana.

Tusijuane.
 
Usichukue tahadhari subiri tamko la shinikizo.
Kila mtu na lwake. Unapata wapi hata uthubutu wa kunishauri miye wewe?

Wewe pambana na hali yako nami napambana na yangu.

Tusijuane!

Ninamsubiri anayekusanya kodi. Si alisema atakuja nyumba kwa nyumba?

Basi atanikuta!
 
Tumeambiwa kunawa mikono kwa sekunde 20 kwa maji tiririka na sabuni. Maji tiririka wengine tunayapata wakati wa mvua tu.

Napambana na hali yangu. Serikali na apambane na hali yake.

Tusijuane.

Ninamsubiri mkusanya kodi. Si alisema hata atakuja nyumba kwa nyumba?

Atanikuta!
 
Mabibi na mabwana kupeana ulio ukweli hata kama ni mchungu vipi ni jambo la msingi sana..
Ni kweli kabisa, kila mmoja na lwake. Serikali hii haina uwezo wowote wa kupambana na majanga. Ni ulaghai wa kisiasa na ushamba wa kimadaraka tu. Hakuna janga waliloweza kulimudu.

Ni kuanzia tetemeko la ardhi Bukoba mpaka covid19/21. Sasa kila mmoja apambane kivyake awe hai au amekufa. Hatuna serikali.
 
Tumeambiwa kunawa mikono kwa sekunde 20 kwa maji tiririka na sabuni. Maji tiririka wengine tunayapata wakati wa mvua tu.
Hivyo ile maabara ya serikali iliyompima corona mbuzi bado ipo?! Maana takwimu za upimaji hazijatolewa karibu mwaka sasa! Nchi ya wagagagigikoko.
 
Ni kweli kabisa, kila mmoja na lwake. Serikali hii haina uwezo wowote wa kupambana na majanga. Ni ulaghai wa kisiasa na ushamba wa kimadaraka tu. Hakuna janga waliloweza kulimudu. Ni kuanzia tetemeko la ardhi Bukoba mpaka covid19/21. Sasa kila mmoja apambane kivyake awe hai au amekufa. Hatuna serikali.

Tumewavumilia vya kutosha. Tumewashauri vya kutosha.

Sasa basi!
 
Hivyo ile maabara ya serikali iliyompima corona mbuzi bado ipo?! Maana takwimu za upimaji hazijatolewa karibu mwaka sasa! Nchi ya wagagagigikoko

Bila shaka hata huyo mbuzi alikuwa hewa na labda hata majibu nayo yalikuwa hewa pia.

Wanaaminika wapi watu hawa?
 
Hii Hakuna takwimu na wanasema wameudhibiti ugonjwa. Lakini wachezaji 3wa Namungo wamekutwa na maambukizi Angola.

Wanasema ugonjwa hamna, Maalim Seif Makamu wa rais anathibitisha anaugua.

IMG_20210216_044017_271.jpg


Yule Prof wa OUT anatoa yake ya moyoni, anaonywa:


Hivi wanatuchukulia je sisi hawa?

 
Habari njema nikuwa chanjo zinaanza kuonesha kilichokuwa kinategemewa. Israel juzi wametangaza asilimia 94% wagonjwa wa wamepungua waliopata chanjo na UK pia jana wamesema baada ya watu milion 15 mpaka sasa kupata chango wagonjwa na vifo vinapungua daily na hii ni dalili njema kwa dunia.

Na kuna jambo nimesikia huu ni ugonjwa wa dunia nzima sio wa mtu fulani kuamua ili kuudhibiti ni lazima chanjo dunia nzima vinginevyo nchi moja wa kidharau hawa virus wanatabia kujigeuza na wanaweza wakaleta maafa dunia nzima tena na hili halikubaliki.

Kuna mawili yatatokea, ikiwa mzee ataleta kiburi basi na kuhakikishia wa Tanzania hata hapo Rwanda tutakuwa marufuku kuingia wala hakutakuwa na ndege hata moja inakuja maana nchi zote zitapiga ban raia wao au ndege kutua TZ au mzee abadili gear angani hakuna ujanja. chanjo inafanya kazi dunia inataka kurudi katika hali yako hii sio option ni lazima. either na sisi au na corona.
 
Habari njema nikuwa chanjo zinaanza kuonesha kilichokuwa kinategemewa. Israel juzi wametangaza asilimia 94% wagonjwa wa wamepungua waliopata chanjo na UK pia jana wamesema baada ya watu milion 15 mpaka sasa kupata chango wagonjwa na vifo vinapungua daily na hii ni dalili njema kwa dunia..
Hakuna kuzuia ndege kuja kwetu HAPANA, TUSIKUBALI.

Uamuzi sahihi ni Dunia kutusaidia kumwonfoa muuaji. Haiwezekani Dunia ikae kimya ikimwangalia kichaa mmoja akiangamiza mamilioni ya watu. Siyo sahihi. Dunia ibebe jukumu lake la msingi laf kuifanya Dunia mahali salama.
 
Back
Top Bottom