Mabibi na mabwana kupeana ulio ukweli hata kama ni mchungu vipi ni jambo la msingi sana.
Haisaidii kuukimbia ukweli.
Kwa hakika hali ya ugonjwa huu ni mbaya sana labda kuliko hata maelezo. Niko Kagera kwa mazishi ya kigogo wa mahakama kuu Mwanza.
Nakutana na misiba zaidi. Itoshe kuonyesha hali hii:
"Bwana Tumsiime mmiliki wa zile shule maarufu Dar kafiwa na mama mkwe na pia shemeji yake ndani ya siku 2 tu."
Pole nyingi ziwafikie yeye na familia yake.
Alianza shemeji, akaenda kuzika na kurejea Dar. Juzi tena, mama mkwe aliyekuwa msibani kwa mwanaye naye kafariki. Amelazimika kurejea kwa mazishi tena.
Changamoto zile zile, watanzania wale wale.
Kwani mengine yapi ni mageni wapi?
Ukweli mchungu, watu wanakufa sana na ugonjwa huu.
Maswali yangu ya msingi kwenye vita hivi nikidhani tuko sote, yamekuwa haya hapa:
Sijapata majibu yake popote.
Ni wazi kuwa kudhani kuwa vita hivi vingepiganwa katika umoja wetu kama taifa, kama ilivyo kwingine, hakupo.
Basi wala isiwe taabu.
Rasmi sasa hapa tulipo ni kila mtu na lwake. Kila mtu ikiwamo serikali, sasa na apigane kivyake.
Kila mtu na achukue njia yake. Kila mtu achukue mzigo wake. Tuachane njia panda.
Kama binadamu mwenye kuwajibika na familia yangu, nami ninachukua njia yangu japo nikiwa nimechelewa sana.
Tusijuane.