Katika kitu ambacho hakitakiwi kufanyiwa masihara basi ni ulinzi wa Rais. Hii ni kawaida sana kwa nchi zote duniani toka enzi na enzi, sio Tanzania tuu. Na endapo likitokea la kutokea basi watu wa karibu kabisa na Rais ndiyo huwa prime blamees. Hamtaweza kuepuka lawama kwani usalama wa Rais uko mikononi mwenu na sio mikononi kwake.
Katika kuangalia usalama wa Rais wote mnaohusika mnapaswa muwe wakweli na muweke maslahi ya nchi mbele kwani Rais ndiyo nchi yenyewe, mkizembea kumlinda Rais ni sawa na kuzembea kuilinda nchi. Katika kutekeleza hili jukumu kubwa kwa nchi yapaswa uwe tayari kwa lolote iwe kupoteza kazi yako, kupoteza uhai wako ili mradi unasimamia kilicho kweli na sahihi.
Hata kama unaona Rais anakosea mnatakiwa msimamie ukweli na kumueleza kinagaubaga wa namna mambo yanavyotakiwa kuwa, mnatakiwa mbaki kwenye mstari sahihi bila kumuogopa Rais mwenyewe kwani likitokea lolote nyie ndio mtahusika 100% na vizazi vyote vitawalaumu nyie na sio Rais mwenyewe.
Sasa kwa kinachoendelea duniani wala haihitaji akili ya form six kujua kwamba we are no exception katika kupatwa na magonjwa. Haiwezekani dunia nzima inapambana na mlipuko wa COVID19 lakini nchi moja inajifanya yenyewe inajua sana kusali na kumuomba Mungu mpaka imeushinda huo mlipuko. Kibaya zaidi nyie mnaohusika na usalama wa Rais mkajifanya kutia boriti machoni na kumuacha Rais aranderande huku na huko bila tahadhari yoyote, mkiwa mmesahau kwamba Rais naye ni mtu na anaweza kuugua pia na kwa kuwa nyie ndiyo mlimshindwa kumshauri vyema basi lawama zote mtabeba nyie.
Nampongeza sana Waziri wa Afya aliyepita, Mh Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Mh Faustine Ndungulile kwa kusimamia ukweli wa sayansi inavyosema na kupambana nayo mwaka jana mpaka maambukizi yakafifia. Nakumbuka namna Mh Ngungulile alivyosimama bungeni na kupinga kujifukiza waziwazi kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi kunazuia au kutibu COVID19, lakini mwishowe alitenguliwa katika hiyo nafasi.
Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa, wasimamizi wa Rais wanapaswa kumuambia na kumshauri ukweli wa mambo ulivyo bila kuangalia consequences zitakuwa nzuri ama mbaya, wasaidizi wa Rais hawapaswi kutanguliza matumbo mbele bali wellbeing ya Rais na taifa kwa ujumla. Sote tunakumbuka katika utawala wa Rais Trump kule Marekani kuna viongozi waandamizi wengi sana walijiuzulu nafasi zao kwa sababu ya kutofautiana na Trump. Hii yote ni kwa sababu walibaki kusimamia ukweli wa mambo ulivyo hata kama Rais yuko kinyume nao. Huu ndio uzalendo wenyewe sasa, uzalendo ni kusimamia ukweli wa mambo ulivyo, uzalendo sio kukubaliana na kila jambo analosema Rais kisa yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi.
Sasa mwaka huu katika mlipuko wa pili wasaidizi wa Rais mmetanguliza maslahi yenu mbele, mmeshindwa kumshauri Rais vizuri na matokeo yake mmeiweka nchi katika taharuki kuu kuliko wakati wowote ule. Hivi likitokea la kutokea mtatujibu nini Watanzania? Mtakuja na excuse kwamba Rais hashauriki? Kama hashauriki inakuwaje bado mpo kwenye hizo ofisi, kwa nini hamkuachia ngazi ili na wengine wajaribu kuinusuru nchi kwenye hiki kiza kinene?
Mnachotakiwa kujua ni kwamba Rais sio Mungu kwamba anajua kila kitu. Ndiyo maana kuna wizara za sekta mbalimbali. Kila waziri anatakiwa amshauri Rais accordingly kulingana na mambo ya wizara husika. Kama wewe ni waziri wa afya na ukajitokeza hadharani unapiga nyungu na kisha kuutangazia umma kwamba hiyo ni dawa ya ugonjwa fulani, basi hata Rais ataamini sababu wewe ndiye mtaalamu mkuu wa hiyo sekta. Hivyo ikitokea watu wakapata madhara kutokana na muongozo wako basi utabeba lawama wewe mwenyewe.
Its not too late, wasaidizi wakuu wa Rais simamieni ukweli bila kuogopa kupoteza chochote, mkitanguliza maslahi binafsi mbele mnampoteza njia Rais na taifa kwa ujumla.