King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
1. Nyungu zirudi (Mh. Jafo ongoza hili kamanda wangu).
2. Gari za abiria zipakie level seat inclusive mwendokasi.
3. Barakoa iwe lazima kwenye maeneo ya mikusanyiko na vyombo vya usafiri.
4. Zingatia kusimama futi 6(1.5M) kutoka alipo mtu wa karibu yako.
5. Ukipatwa na homa usipaniki, endelea na maisha mengine lakini hakikisha unavaa barakoa ili kuwakinga wengine.
6. Maombi ya kitaifa yarudi tena ikiwezekana yawe nonstop(Viongozi wa dini tusaidieni kwa hili).
Naomba ieleweke corona virus anasababisha pneumonia. Pneumonia ni pneumonia, haijalishi imesababishwa na kirusi ama vumbi ama kupaliwa. Pneumonia inaweza kumpata mtu yoyote yule wa umri wowote ila makali yake yatayegemeana na nguvu za kinga za muhusika. Ndio maana watoto wachanga huwa wanapata chanjo ya pneumonia sababu kinga zao bado hazina nguvu.
Hata hii pneumonia inayosababishwa na corona ni pneumonia kama pneumonia zingine. Lkn tofauti inakuja kwenye namna huyu kirusi anavyosambaa kwa kasi. Na huyu kirusi anakula mapafu, kitu kinachofanya awe hatari kushinda visababishi vingine vya pneumonia.
Mama Gwajima, fieldmarshal wa sekta ya afya, rudisheni zile measures mlizochukua mwaka jana, hatutaki data zenu bali hatua madhubuti ili kuepusha usambaaji wa huyu mdudu. Watu wamerelax mnoo mtaani. Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba, tena iwe ya mapema kabla haijawa too late.
Nimeongea haya baada ya kumshuhudia jamaa yangu leo akihemea juu juu. Kwa kweli huwezi elewa ubaya wa hii kitu mpaka ikupate au umshuhudie nduguyo au jirani yako akiteseka nayo. Its very terrible bandugu, usiombe kabisa.
Ni hatari sana Mkuu.