#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Ipo sana. Kama mtu haaamini aende hospitali ya amana watu wanaumwa lakini hawambiwi ni nini,ila wanatumia oxygen (nina ndugu hapo) usiku kuna mzee mmoja kafa alikua anatumia oxygen pia
 
Hospital hawafunguki tu wazi mpaka uwe umezidiwa lakini ukweli corona ipo na saiv imekuja kwa kasi.
Ukienda hospitali unakuta kuna vifaa vya kunawia, wanakuambia magonjwa ya kuambukiza ni mengi hakikisha unanawa.
 
Hamna kitu kinaniuma Kama Raisi wa nchi kufanyia hili janga mzaha na kuwa na kebehi.

Asiweke lockdown ila asisitize watu kujikinga na huu ugonjwa. Ata Kama watu wanakufa wachache, uhai wa mtu mmoja unathamani Sana.


CHUKUA TAHADHARI CORONA IPO NA INAUA KWELI KWELI.
Ukweli ni huo imebakia tu kuchukua tahadhari mwenyewe no way
 
Sijui hii niliyoumwa ndio corona? homa kali sana, kikohozi kisichosikia dawa(si kawaida kwangu kuumwa kifua), kwakweli kwa wiki mbili niliteseka mpaka nikahisi kufa.
 
Ukweli ni huo mzee
Ipo sana. Kama mtu haaamini aende hospitali ya amana watu wanaumwa lakini hawambiwi ni nini,ila wanatumia oxygen (nina ndugu hapo) usiku kuna mzee mmoja kafa alikua anatumia oxygen pia
 
Hadi tukifika hatua ya kutangaziwa ugonjwa upo... Hali itakuwa ya hatari kuliko tunavyotarajia
 
Mimi niliumwa kichwa na koo. Sauti ikapotea na kukauka.

Nilitafuna tangawizi na kunywa iliyochemshwa. Nikameza vitunguu swaumu na kunywa mchachai.

Ndimu pia nimetumia. Nimepona ila barakoa siachi.

Mungu mkubwa sana.
 
Toa maoni nini kifanyike badala ya kila mmoja kulialia na kutupa lawama huku na kule.

Watanzania tunapaswa kupambana kivyetu kwa sababu Corona haijatuathiri kama yale mataifa ya Ulaya tutiane moyo badala ya kutishana.

Karibu kwa maoni.

Maendeleo hayana vyama!
 
10126120311.jpg
 
Ibakie hivi hivi, mpk hapo tutakapopata akili sahihii na mbinu sahihi ya kukabiliana na mgeni huyu korona.

Hivi Sasa tutaishia kuchoshana tu.
 
Ni wapumbavu tu.

Leo hii Lebanon watu 2 wamekufa wakiandamana kupinga lockdown maana wameona haisadii chochote zaidi ya kuongeza ugumu wa maisha.

Hapa kwetu mijitu inazurura kariakoo ila ipo mitandaoni kulaumu rais kwamba hajali maisha ya watu. Kwani ukiaamua wewe kukaa kwenu usiende kuzurura mjini rais atakuja kukutoa ndani kwa lazima?

Natamani siku Magufuli atufungie ndani walau wiki 2 hivi ili mijitu aakili zikae sawa.
 
Iache upotoshaji na hoja za kijinga za kufanya maombi na kubeza barakoa.

Sote tunajua uwezo wetu kifedha, ni kweli hatuwezi kununua chanjo za corona na pia hatuwezi lockdown.

Lakini tunaweza kuvaa barakoa, kunawa mikono na kufanya social distancing panapo wezekana.

Pia tunaweza kuweka kipaombele cha kuwalinda walio kwenye makundi hatarishi.

Ikiwezekana rais akae kimya! Amekua akiongea mambo ya ajabu kabisa tangu mwanzo mwa janga hili, the best he can do for our country is to shut up.
 
Tumshukuru Mungu kuwa Waafrica madhara ni kidogo sana ,serikali iwape nafasi wataalamu afya kuelekeza mbinu kuwakinga wachache,wazee na wenye kinga duni.
 
Mkuu johnthebaptist mbinu na njia ile ile iliyotumika wakati wa Wimbi la kwanza, itumike na katika Wimbi la Pili.
Yona 3:5-6 "Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu"
 
Bila unafiki tukubali tu lockdown haihitajiki Tanzania.

Kinachotakiwa ndicho kinachoendelea bwashee.
 
Back
Top Bottom