Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Profesa Makame Mbarawa amekuwa akisema DP world ilipewa mkataba wa bandari kwa kuwa ilishinda kwenye kuomba zabuni ya uwekezaji wa Bandari (akidai ikizishinda kampuni zingine saba) na wakati huo huo document za mikataba ambazo zimetiwa saini na Professor Mbarawa huyo huyo zinaonyesha DP world walipewa mkataba moja kwa moja bila kupitia mchakato mwingine wowote wa kuomba zabuni baada ya Rais Samia kutembelea Dubai na kutia saini makubaliano ya DP world kuja kuwekeza kwenye bandari yetu.
Kwa kuwa suala la uwekezaji wa bandari ni suala la kisheria, na sheria ya utoaji Zabuni inataka kufanyika mambo kadhaa muhimu ikiwemo.
1. Kutoa tangazo la Zabuni kwenye gazeti la serikali.
2. Kufunguliwa (kuwekwa wazi) kampuni zilizoomba Zabuni.
3. Kushindanishwa (kujadiliwa) kwa Zabuni kwa haki ili kumpata mzabuni mmoja atakayepewa mkataba.
4. Kutangazwa rasmi kwa mshindi wa Zabuni.
Sasa ili kuondoa huu utata, bila kumumunya maneno, tunaitaka sasa serikali ifanye haya;
-Ituambie ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari yetu ilitangazwa
-Ni lini makampuni yaliyoomba hizo Zabuni yaliwekwa wazi (zabuni ziliwekwa wazi)
-Ni kampuni gani hizo Saba zilizotajwa na Profesa Mbarawa ziliomba kuwekeza kwenye Zabuni za Bandari.
-Ni lini na wapi Zabuni za uwekezaji wa bandari zilifanyika.
-Ni vipi ushindani wa Zabuni ya uwekezaji wa bandari ungekuwa wa haki ikiwa DP world tayari walikuwa wameanza ubia na serikali ya Tanzania kupitia urais wa Tanzania katika kutaka kuwekeza bandarini.