Serikali: Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi

Huyo bado hatalipa Kodi kwan kwake atakuwa na purchases tu bila sales or relatively low sales
 

Kwa hivyo mtu asiye na kipato anadaiawaje Kodi?. Kodi inamfaa mtu mwenye kipato.
 
Naona kodi ya kichwa imerudi
 
K
Matumizi ya serikali ambayo ni hospitali, mashule(sasa elimu bure mpaka form 6), majeshi, polisi nakadhalika.

Hayo mashule walijenga kwa kutumia Nini Hapo kabla?. Kwa hivyo kodi, tozo na mikopo bado haitosh?. Nchi ngumu Sana hii.
 
Bunge lililopita Waziri alikuja na tozo kama namna ya kuongeza makato kwa watu kutumiana hela kwa ndugu na jamaa. Huu mkakati haikuwa sawa maana unatoza Kodi kwenye uzalishaji na soon kwenye miamala ya fedha kidogo sana watu wanazotumiana.

Sasa kwenye kumpatia kila mtu TIN kwa kila mwenye NIDA, hapa kuna maswali ya msingi ya kujiuliza na kumuuliza waziri na wachumi wetu.
Uzalishaji umekuwa ili kutoza kodi kwa kila TIN kama ilivyokuwa kodi ya kichwa?

Hoja ya msingi wabunge wamuulize waziri, hawa wenye TIN kwa sasa, ni wangapi ni regular taxpayers kwa mwezi au mwaka?
Maana kuna wengi Tu, wana TIN za leseni, wengine walilazimika kuwa na TIN kama namna ya ku-reflect kodi za mishahara.

Kuna input gani wizara inafanya ili kusisimua na kukuza uzalishaji wa wananchi ili wawe na uwezo wa kulipa kodi pasi hata kulazimishana kila mtu kuwa na TIN.

Kwa biashara zenye TIN, ni wanyapori Wana EFD machine na zinatumika kwenye kila mauzo ya bidhaa na huduma?

Mathalani, tuanze na wakulima wa Masai ya biashara kama (pamba, korosho, kahawa, mikoa, tumbaku, chai, katani, pateto) au wafugaji (wenye mifugo kuanzia 20); ni wangapi wamesajiliwa kwa kuwa na TIN ili kutozwa kodi kwenye mauzo yao kwa msimu?

Kama ambavyo suala la miamala lilizua maswali na takwimu zili-prove kupungua kwa watu kutumiana miamala, hapa napo waziri atujuze kimkakati, anawezaje kupata 'maziwa kutoka kwa ng'ombe' ambae hajala vya kutosha?

Au ndio yale ya kuwa na udahili wa wanafunzi wengi darasa la kwanza, kidato cha kwanza ila wanaomaliza la 7 na kidato cha 4 na kufaulu ni wachache!

Kama kuna namna Bora ya serikali kukuza makusanyo, lazima kusisimua biashara hasa kwa consumables zinazokuwa-imported zianze kuzalishwa ndani.
Bank ya uwekezaji iongezewe mtaji na mizengwe na umangimeza uondoke kwenye processing ya investment financing.

# kazi iendelee.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hili suala sijui wanafeli wapi,
1. Waondoe kodi kwenye manunuzi yanayofanyika direct kutoka kwenye bank/mobile money.
2. Waongeze kodi katika withdraw zote za bank/mobile money
3. Then kila transaction inayofanyika directly kupitia bank/mobile moneybiwe recorded
4. Wenye kufanya manunuzi mengi kupitia bank/mobile money wawe awarded either kupitia new bahati nasibu waliyoianzisha au wapate punguze kwenye some services, mfano mzuri kwa wenzetu walipa kodi wazuri wanapewa urahisi wa kukodi nyumba za serikali sasa kwa huku watafute bonus servise ya kiwapa walipa kodi wazuri
5. Hapo wataongeze base ya walipa kodi na kuongeza makusanyo big time
 
Wanaolipa kodi kwa uhakika nchi hii ni watumishi tu( PAYE)
Wengine ni wakwepaji, wanalipa kiduchu tu
watafute namna ya kukusanya kodi effectively kutoka kwa wafanyabiashara
 
"Miaka 18 na mwenye kipato"

Kipato gani sasa maana umri huo bado ni wanafunzi au kutoka kwenye pocket money za wazaz
 
Naomba kufahamu "Service Levy" ikoje na inalipwa na akina.nani?
Je ina manufaa gani kwa mlipaji?
 
Kwa maana nyingine... kodi ya kichwa imerudi. Anyways, nchi ya watu zaidi ya mil 60, kuwa na walipa kodi mil 2.5 sio fair.
 
K

Hayo mashule walijenga kwa kutumia Nini Hapo kabla?. Kwa hivyo kodi, tozo na mikopo bado haitosh?. Nchi ngumu Sana hii.
Kwan wasiwasi wako ni upi?
Manunuzi na maizo au mapato yapo kwenye Tin , ikiwa faida au tofauti yake itazidi au kufikia kiwango cha kulipa Kodi utalipa....mfano ikiwa kwa mwezi hiyo tofauti haiizidi 270,000 hutalipa....maisha bomba
 
Kodi ilikuwa kwa watumishi na wafanyaniashara Tu,sasa hivi tulipe Kodi wote,sio wengine ndio wanajenga hospital, shule, barabara, alafu wengine wanatumia bure kwa Kodi za wenzako.
 
Matumizi ya serikali ambayo ni hospitali, mashule(sasa elimu bure mpaka form 6), majeshi, polisi nakadhalika.
Ikiwa tozo zimeshindwa kuleta unafuu katika hizo sekta, hiyo kodi ya kichwa isiyo na uhakika itaweza?

Wekeni wazi tu kuwa zinatafutwa nauli za mama yenu ambae hajawahi kumaliza hata wiki moja ofsini bula kusafiri tangu aingie madarakani.
 
Kodi ilikuwa kwa watumishi na wafanyaniashara Tu,sasa hivi tulipe Kodi wote,sio wengine ndio wanajenga hospital, shule, barabara, alafu wengine wanatumia bure kwa Kodi za wenzako.
Ukweli ndio huo, wafanyakazi wanatukata mshaara ukiingia tu, LOANS BOARD wengi wangi tu wame kwepa ila mtumishi wa uma makodi yote wana fyeka. Nime gundua watanzania wengi hawapendi kulipa kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…