1. Tin haitozwi Kodi ila tofauti ya manunuzi na mauzo kwenye Tin ndiyo yatakayotozwa kodiBunge lililopita Waziri alikuja na tozo kama namna ya kuongeza makato kwa watu kutumiana hela kwa ndugu na jamaa. Huu mkakati haikuwa sawa maana unatoza Kodi kwenye uzalishaji na soon kwenye miamala ya fedha kidogo sana watu wanazotumiana.
Sasa kwenye kumpatia kila mtu TIN kwa kila mwenye NIDA, hapa kuna maswali ya msingi ya kujiuliza na kumuuliza waziri na wachumi wetu.
Uzalishaji umekuwa ili kutoza kodi kwa kila TIN kama ilivyokuwa kodi ya kichwa?
Hoja ya msingi wabunge wamuulize waziri, hawa wenye TIN kwa sasa, ni wangapi ni regular taxpayers kwa mwezi au mwaka?
Maana kuna wengi Tu, wana TIN za leseni, wengine walilazimika kuwa na TIN kama namna ya ku-reflect kodi za mishahara.
Kuna input gani wizara inafanya ili kusisimua na kukuza uzalishaji wa wananchi ili wawe na uwezo wa kulipa kodi pasi hata kulazimishana kila mtu kuwa na TIN.
Kwa biashara zenye TIN, ni wanyapori Wana EFD machine na zinatumika kwenye kila mauzo ya bidhaa na huduma?
Mathalani, tuanze na wakulima wa Masai ya biashara kama (pamba, korosho, kahawa, mikoa, tumbaku, chai, katani, pateto) au wafugaji (wenye mifugo kuanzia 20); ni wangapi wamesajiliwa kwa kuwa na TIN ili kutozwa kodi kwenye mauzo yao kwa msimu?
Kama ambavyo suala la miamala lilizua maswali na takwimu zili-prove kupungua kwa watu kutumiana miamala, hapa napo waziri atujuze kimkakati, anawezaje kupata 'maziwa kutoka kwa ng'ombe' ambae hajala vya kutosha?
Au ndio yale ya kuwa na udahili wa wanafunzi wengi darasa la kwanza, kidato cha kwanza ila wanaomaliza la 7 na kidato cha 4 na kufaulu ni wachache!
Kama kuna namna Bora ya serikali kukuza makusanyo, lazima kusisimua biashara hasa kwa consumables zinazokuwa-imported zianze kuzalishwa ndani.
Bank ya uwekezaji iongezewe mtaji na mizengwe na umangimeza uondoke kwenye processing ya investment financing.
# kazi iendelee.
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
2. 2 2 milioni registered tax payers
Hapo awali ilikuwa hutauza bila Efd receipts, sasa kibao kinageuka hutanunua bila Tin number...tafsiri take ni kuwa Tin zitageuka ndio kitabu cha TRA kukotoa Kodi ndio maana italazimuka kila mmoja awe na Tin na hakuna kununua pasipo TIN...wenye efd machine hawatoweza kutoa riaiti isiyo na TIn ya mnunuaji