Serikali: Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi

1. Tin haitozwi Kodi ila tofauti ya manunuzi na mauzo kwenye Tin ndiyo yatakayotozwa kodi
2. 2 2 milioni registered tax payers

Hapo awali ilikuwa hutauza bila Efd receipts, sasa kibao kinageuka hutanunua bila Tin number...tafsiri take ni kuwa Tin zitageuka ndio kitabu cha TRA kukotoa Kodi ndio maana italazimuka kila mmoja awe na Tin na hakuna kununua pasipo TIN...wenye efd machine hawatoweza kutoa riaiti isiyo na TIn ya mnunuaji
 
Tupeni ajira,mitaji kwanza ili tuweze kulipa hiyo Kodi. Vinginevyo mna visa na vijana. Uwingi wa tozo zisizo na kichwa Wala miguu unatosha.Kama vipi punguzeni mishahara ya wabunge. Vijana tuacheni kwanza
 
Wanaolipa kodi kwa uhakika nchi hii ni watumishi tu( PAYE)
Wengine ni wakwepaji, wanalipa kiduchu tu
watafute namna ya kukusanya kodi effectively kutoka kwa wafanyabiashara
Acha kazi fanya biashara kama unadhan ni rahisi
 
Okey. Hapa nimeelewa
 
"Miaka 18 na mwenye kipato"

Kipato gani sasa maana umri huo bado ni wanafunzi au kutoka kwenye pocket money za wazaz
Kwa huyu hatolipa Kodi kwa sababu tin yake itao esha purchases ndio nyingi kwan hana sales anayofanya
 
Huduma za jamii mnataka kodi hamtaki kutoa, hongereni watanzania
 
Vijana mtaani ni majobless sasa wapambane watoe ela kwaniaba yakula nyie tena aisee duuh fanyeni strategic paln zingne za kuingiza kipato ila iyo sioni kam inatija
 
Matumizi ya serikali ambayo ni hospitali, mashule(sasa elimu bure mpaka form 6), majeshi, polisi nakadhalika.
Elimu bure sindio kitu cha kwanza kufutwa baada ya mama enu kuingia madarakani na kurudisha posho za vikao na semina kwa watumishi
 
Hio kodi wanayogombania kutoza tunaomba waoneshe wanaitumiaje na kama ndio upangaji budget ya maendeleo matumizi yanaonekana ni 80% na maendeleo ni 20% naomba watuache kabisa.
 
Poijt
Point taken.
Hoja yako inaeleweka sana.

Ila bado kama wale wenye EFD machine ukinunua baadhi hawatoi risiti either watasema hamna network, au karatasi zimeisha au machine mbovu au baadhi wana undervalue.

Kabla ya kusajili kila mtu mwenye NIDA awe na TIN, je wale waliosajiliwa, kiasi gani wanaingiza based on daily sales?

kuna uwajibikaji kweli?

Sehemu ngapi za huduma iwe hotel,maduka hawatoi EFD?

Ila pia kuna mkakati gani wa kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kukuza exports na kuzalisha ku-cut down imports?

#kazi iendelee
 
Ufunuo 13:16 Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao. 17 Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.
18.Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666.
 
Ikiwa tozo zimeshindwa kuleta unafuu katika hizo sekta, hiyo kodi ya kichwa isiyo na uhakika itaweza?

Wekeni wazi tu kuwa zinatafutwa nauli za mama yenu ambae hajawahi kumaliza hata wiki moja ofsini bula kusafiri tangu aingie madarakani.
Kodi inaingiaje serikalini, ni kwa utaratibu utakaowekwa.
Inatumikaje mkwide mbunge wako aulizie bungeni.
 
Kesho wakiondoa hiko kipengele utapongeza tena
 
Machinga wanatafutwa.... Na watalipa tu kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…