Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Tabu ni kwa mashabiki waliosafiri toka mbali kama Morogoro na Tanga ambao walitaraji kugeuza mapema baada ya mechi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani anatokea mtu mmoja kwa sababu ana madaraka tu anaagiza ratiba ya tukio kubwa kama hili liahirishwe, bila kujali maelfu ya wananchi ambao wako uwanjani, Hiki ni kiburi cha madaraka!

Wanadhani kila mtu anahitaji sana kusikiliza hizo hekaya za huyo mzee aliyekuwa anataka Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani.
 
Aisee. Inabidi hapa mtaani kwetu tuendelee tu kuvumilia kelele zao za vuvuzela....
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri, bali lazima itekelezwe, lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!

kiukweli walichofanya ni u***
 
Aisee. Inabidi hapa mtaani kwetu tuendelee tu kuvumilia kelele zao za vuvuzela....
Hii game sidhani kama itachezwa tena, psychollogy za wachezaji na viongozi zimeshavurugika, hao wapiga kelele wataondoka muda sio mrefu, Yanga wameshaanza kuondoka uwanjani.
 
TFF HAO wakaidi wakitoa timu uwanjani wapigwe faini.
mpira ule ule tofauti masaa Tu.
 
Hii game sidhani kama itachezwa tena, psychollogy za wachezaji na viongozi zimeshavurugika, hao wapiga kelele wataondoka muda sio mrefu, Yanga wameshaanza kuondoka uwanjani.
Hatakama ikichezwa haitakuwa na amsha amsha yeyote
 
HAO walioziweka hizo kanuni ndo wamezivunja SHIDA ipo wapi?.
wewe fuata maelekezo.
Polisi trafiki wameweka Sheria barabarani lakini WAO NDO WA KWANZA KUZIVUNJA.
mpira NI SAA 1 USIKU
Kanuni za ligi lazima ziheshimiwe, siyo kuendesha ligi kama ndondo cup
 
Serikali inatakiwa iwe makini sana, hao wanaowaita wanyonge usiwaguse kuhusu yanga na simba wataandamana hadi vijijini zingua vyote lakin sio simba na yanga
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri, bali lazima itekelezwe, lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!
1620486894458.png

Mkuu wewe ni mtu mzima acha uzushi-
 
Back
Top Bottom