Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Ligi ishavurugwa tayari. Taarifa zilizopo ni Yanga kudai pointi 3 kwa mpinzani kutoonekana uwanjani muda wa mchezo.

Serikali imelikoroga.
 
Napenda kusoma vitabu, lakini hicho kitabu chal walichozindua leo sitotaka kuliona hata cover lake
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri basi lazima itekelezwe, serikali lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!

Bro mi nadhani kuhusisha tukio la kuahirishwa mechi na uzinduzi wa kitabu ni hisia tu. Mbona zinduzi nyingi tu za vitabu zimefanyika bila hata kuathiri shughuli zingine?
TFF watoe tu maelezo ya kwa nini mechi haikuchezwa.
 
Naona huelewi bado hii nchi
 
Poor us
Athari na chembechembe zingine zilizobaki za utawala wa awamu ya tano kujitolea matamko.

Michezo ina mfumo wake maalum ambayo hupangwa kwa muda mrefu lakini mazoea ya awamu ya 5 yameharibu kabisa utawala wa sheria, mifumo, taratibu na kanuni.

Nchi inategemea zaidi tamko la waziri, wizara, mkuu serikali za mkoa au rais au rais wa TFF bila kuzingatia mambo mtambuka kisheria, kimichezo n.k

Utasikia hata humu JF mtu anaweka " Rais wa Kenya aruhusu waTanzania ..." huku ni kuonesha jinsi jamii ya Tanzania ilivyoathirika na kutegemea zaidi matamko, hisani za mtu / watu wenye mamlaka badala ya kufuata sheria, katiba, kanuni , taratibu labda tu pale panapotokea hali ya hatari kwa wananchi na hizo pia zimeainishwa katika sheria na katiba kwa wingi kabisa nini kifanyike.
 
kumbe na dole unawekewa aisee
Zawadi yako hiyo kenge wewe
tapatalk_1576166751572.jpeg
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri basi lazima itekelezwe, serikali lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!
Kuna mtu alikua anajipendekeza. Walizoea kujipendekeza, sasa wamelewa madaraka wanajipendekeza kila sehemu. Hili wamelikoroga, ngoja tuone wanalinywaje?
 
Kama suala dogo kama hili mama amechemka je ataweza ku handle makubwa?

Awezi kukwepa lawama kabisa
siasa michezoni ndo ubaya wake watatafuta kisingizio na pengine kupanga terehe nyingine ya mechi na sharti watu wachache wenye barakoa mwelekeo mpya
 
Hamna kachemka tu kwani ungechezwa saa 1 ndio hizo barakoa zingevaliwa?

Mbona tunarahisisha mambo wakati uzembe umefanyika
 
🤣 🤣 Mkuu wa mkoa analinda kutumbua chake kisiingie mchango.
 
Back
Top Bottom