Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Hiyo nia njema ya kusogeza mbele huo mchezo ilikuwa ni ipi? Binafsi nilitegemea waeleze pia kwa nini waliahirisha lakini pia watoe "commintment" kuwa siku nyingine na wao wataheshimu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia na kuendesha shughuli nyingine na sio mtu tu kukurupuka na kuwaingiza watu hasara za kipuuzi.
Hii ni nchi ya hovyo sn
 
Mechi inavurugwa kunusuru Team ya Chama dhidi ya kipigo
Hivi hiyo timu ya chama ni ipi?

Majaaliwa ni simba.

Ndugaye ni simba .

Na hao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho ukimwacha mama Samia ambaye hana timu.
 
Athari na chembechembe zingine zilizobaki za utawala wa awamu ya tano kujitolea matamko.

Michezo ina mfumo wake maalum ambayo hupangwa kwa muda mrefu lakini mazoea ya awamu ya 5 yameharibu kabisa utawala wa sheria, mifumo, taratibu na kanuni.

Nchi inategemea zaidi tamko la waziri, wizara, mkuu serikali za mkoa au rais au rais wa TFF bila kuzingatia mambo mtambuka kisheria, kimichezo n.k

Utasikia hata humu JF mtu anaweka " Rais wa Kenya aruhusu waTanzania ..." huku ni kuonesha jinsi jamii ya Tanzania ilivyoathirika na kutegemea zaidi matamko, hisani za mtu / watu wenye mamlaka badala ya kufuata sheria, katiba, kanuni , taratibu labda tu pale panapotokea hali ya hatari kwa wananchi na hizo pia zimeainishwa katika sheria na katiba kwa wingi kabisa nini kifanyike.
Bila kumuondoa yule pm hatutakuwa na mabadiliko
 
Aisee...! Hilo elekezo la kwanza kuhusu" mechi ya Simba na Yanga iliyohairishwa "mbona linanichanganya. Linasema, mechi irudiwe!! mechi itarudiwaje wakati haijachezwa? Unarudia kitu ambacho hujakifanya!? Au ni mbinu ya kuhalalisha madai ya Simba ya kutaka wapewe ushindi wa mezani wa 3 points na 2 goals?
===
Nisaidieni, yawezekana kiswahili ndicho kinanipiga chenga.
Imeandikwa haraka haraka maana wanajua watanzania ni wapimbafu hawataisoma. Umesema ukweli.
 
Waambie utopolo waendelee kugoma.
Na tarehe MPYA wataopangiwa na wale wale waliosogeza mbele muda
Mpira ni saa 1 usiku!!!!!
Hiyo ndiyo sheria ya FIFA kuwa mpira lazima uchezwe saa 1 usiku?
 
TUNATAKA WATUAMBIE SABABU ILIKUWA NINI?
HATA YA KUTUNGA WASEME TU
 
Wanadhani kila mtu anahitaji sana kusikiliza hizo hekaya za huyo mzee aliyekuwa anataka Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani.
Juhudi za kujipendekeza zilizaa matunda kwani kijana wake sasa hivi ni prezidaaa
 
Back
Top Bottom