Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Kama serikali imeamua hivyo ni jambo jema sana ila wasi wasi wangu kuna baadhi ya watu watajipa mamlaka ya hivyo vishikwambi kuliko hata serikali na kusudio lake... Hivyo huenda visifike kwa walimu wote
 
Tanzania kubadilika ni ngumu sana tunajikwamisha wenyewe hsa watendaji wa serikali wanakwamisha mambo mengi sana mazuri.

Mimi ni shuhuda 2021 nilipeleka a very good ict project kwa tamisemi na wizara ya elimu kwaajili ya shule zetu hizi za umma na ilikuwa simple na inayoendana mazingira yetu.

Kilichotokea huko ni kusifiwa tu good project ooh hii itaeta mabadiliko sasa kwenye ushirikiano hupewi hata kupata kibali tu nilisota mwaka na sikupata the end vijana wa ict waliograduate kama 13 ambao ndio waliunda mfumo huo wa elimu walianza kutawanyika mmoja mmoja na ndio mchezo ukausha hivyoo.

Hii nchi ni ngumu sana kufanikiwa hasa km wewe ni mtu wa kunyoosha mambo.

Ni ngumu sana hii nchi.
Ndio maana kuna gap kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Ukiwa siriaz utapiga pesa sana kwani wengi ni wachuuzi tu lkn ukiwekeza vizuri kwenye tech hapa bongo utaula sana
 
Hii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?

Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.

Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
Akumbuke siyo shule zote zina umeme
 
Hii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?

Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.

Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
Well said [emoji120] [emoji120]... Hivi vilitakuwa kutolewa kwenye research institutions kwa mfano kufanyia kazi kama kuandaa surveys mbalimbali, data collection, uandaaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi za vijiji, kuandaa CCROs, kuhesabu mifugo yote nchini etc etc...
 
Sasa kishikwambi kitamsaidia nini mwalimu kuandaa masomo yake, ni bora hata wapewe laptop. Bongolala kuna watu wanakurupuka sana.
Nina jirani yangu ni mwalimu, tena wa sekondari, kuna siku aliniletea laptop yake nimssidie ku install some programs.. Umeme ukakatika nikamwambia iache baadae ukirudi nitakuwekea. Uliporudi nikamuwekea na kila kitu fresh. Wakati napitia ile laptop sikuona hata faili moja la shule (mitihani, maandalizi ya masomo etc) laptop imejaa movies, miziki, mapicha etc unakuta faili moja la movi GB 50 (seasons hizoo daah...
 
Acha dharau wewe. Hujui kuwa siku hizi kuna online books na other teaching materials tena kuanzia level ya shule ya msingi. Si kila kitu lazima ucomment ndugu, kama huna taarifa pita kimya au uliza ufahamishwe.
Anachosema mdau ndiyo ukweli wenyewe huo, wewe bisha tuu lakini si tupo hapa? Tuombe Mola atupe uhai ndani ya miaka 3 ijayo utaniambia... Niko nimekaa paleee kijiji cha Nanguruwe..
 
Mkuu mimi sijadharau mtu hapa.

Wangefanya pilot study kwanza kwa shule chache hasa vijijini huko, waone kama hivyo vishikwambi ni feasible kwenye kutolea elimu.

Kitendo cha kuchkua mzigo wa tablets na kuzigawa bila kufanya utafiti wa ufanisi wake ni risk kubwa, inaeza kuleta hasara tu.

Hizo tablets zinafaa zaidi kwenye higher learning institutions kufanyia survey na data collection, ila kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi tutadanganyana.

Shule nyingi ziko huko vijijini (usiangalia shule za mjini tu) huko bush umeme shida na network hamna. Hizo tablets wanazitumiaje? Fanyeni pilot study muone feasibility ya huo mradi wenu
 
Well said [emoji120] [emoji120]... Hivi vilitakuwa kutolewa kwenye research institutions kwa mfano kufanyia kazi kama kuandaa surveys mbalimbali, data collection, uandaaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi za vijiji, kuandaa CCROs, kuhesabu mifugo yote nchini etc etc...

Hapo mkuu umeongea sawa kabisa.

Hawa walimu tu notes zao hawaweki kwenye laptop wanatumia vitabu hardcopy

Na mazingira wanayokaa wengi wao ni vijijini huko, hakuna umeme wala network. Na hawajafanya pilot study hata kwa shule chache waone feasibility ya hio ishu

Tuwape muda tu
 
Acha ushamba, Walimu kibao tu wanatumia technology kufundishia. Mbona mna chuki sana kwa walimu?

Sawa mimi ni mshamba.

Hakuna haja ya kutumia maneno ya kejeli kuniita “mshamba” na sina chuki kwa walimu.

Wewe kama mwalimu weka point yako hapa namna gani unatumia hata laptop tu na smartphone yako kufundisha hao watoto shule ya msingi.

Kama hivyo vifaa huvitumii sidhani kama tablet itakua na tofauti yoyote ukipewa.
 
Anachosema mdau ndiyo ukweli wenyewe huo, wewe bisha tuu lakini si tupo hapa? Tuombe Mola atupe uhai ndani ya miaka 3 ijayo utaniambia... Niko nimekaa paleee kijiji cha Nanguruwe..

Tuwape muda, wanatumia hisia zaidi badala ya ku reason. Mara tuna chuki na walimu mara ni washamba

Lakini deep inside wakikaa na kutafakuri kwa kina, wanaona kabisa hili suala liko kisiasa
 
Mhe. Rais Samia Suluhu amekuwa akihimiza matumizi ya TEHAMA ili kuboresha huduma kwa jamii.

Kuonesha mfano, Serikali anayoiongoza itagawa vishkwambi zaidi ya 300,000 kwa walimu wote nchini ili kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Rais Samia Suluhu amedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania
 
Back
Top Bottom