Serikali kujenga madarasa mapya manne katika kila shule ya Sekondari ya Serikali. Watoto wote 1M kuanza shule Januari 2022

Kikwajuni One asante Sana,

Tuendelee kumwombea na kumsemea Rais wetu Mzalendo wa kweli,

Kunawaliotamani afeli wamcheke ila Mungu amemsimamia hadi wanashangaa,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
Wewe mwenzetu ni msomi kupita sisi,usiache kutupa habari za maendeleo ya nchi yetu,kwa kweli sio siri,mashule,hospital na huduma nyingi,zimezidi kuimarika.Mungu ampe afya na umri mrefu,Rais wetu.
 
Mungu akubariki Rais wetu,jana nilitembelea shule moja ya secondary,jinsi ilivyo,utafikiri uko ofisi za kimataifa,tiles shule nzima,Rangi safi,vyoo vya kisasa na safi,mabustani,shule utafikiri uko Marekani.
Mungu akubariki sana Kikwajuni One

Mama anafanya makubwa sana,

Hakuna mwaka yalijengwa madarasa elfu 15 kwa mkupuo,

#KAZI IENDELEE
 
Wewe mwenzetu ni msomi kupita sisi,usiache kutupa habari za maendeleo ya nchi yetu,kwa kweli sio siri,mashule,hospital na huduma nyingi,zimezidi kuimarika.Mungu ampe afya na umri mrefu,Rais wetu.
Sifa ziwe na Mungu wetu daima,
 
Nawasalimu kwa jina la JMT,

Tanzania inajumla ya shule za sekondari 5,143 hii ni kwamujibu wa Shirika la Taifa la takwimu yaani NBS huku kati yake shule 3,863 ni shule za Serikali |Umma huku shule 1,280 zikiwa ni shule binafsi|Private schools,

Rais Samia Suluhu baada ya kupata anachokiita "Kijipesa " mahali sasa ameamua kuwatua mzigo wazazi kwa kujenga jumla ya madarasa mapya elfu 15,"Hii haijawahi kutokea " alisikika Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI akisisitiza chanzo ni " UTV Habari" jana trh 01|10|2020 Saa 2 Usiku,

Sasa ukichukua haya madarasa yote 15,000 ukayagawanya kwa shule zote za sekondari za Serikali 3,863 kila shule itapata wastani wa madarasa mapya manne ( 4 ) kwa lugha rahisi Rais Samia Suluhu Hassan ataongeza wastani wa madarasa manne katika kila shule ya serikali Tanzania nzima hakika Rais Samia Suluhu ni masikini anayekumbuka masikini wenzake,

Mtakumbuka pia ni jumla ya watahiniwa elfu 460 ndio wanatarajiwa kumaliza kidato cha nne mwezi ujao huku matarajio ya Wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza ni jumla ya wanafunzi milioni moja sawa na ongezeko la zaidi ya wanafunzi elfu 500,Hawa ndio walimnyima Mama Samia Suluhu Hassan usingizi na tayari amelimaliza hili, nakufanya kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuripoti kwa tarehe moja nchi nzima ambayo ni trh 06|01|2022

Hata hivyo watoto hawa hawatalipa ada hata mia kwani tayari Rais Samia ameshapeleka jumla ya Tshs 62.3bl kwa halmashauri zote 184 yaani mambo ni bam bam,

.........Kazi iendelee .........

==================================

Kidato cha kwanza 2022 wote kuanza shule siku moja
MONDAY SEPTEMBER 27 2021

Summary

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wanafunzi watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja.

Ummy amesema hayo leo Jumatatu Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma.

Amesema amepata maagizo kutoka kwa kiongozi huyo kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa asingependa kuona mwakani wanafunzi wanapishana kuanza shule kwa kisingizio cha uhaba wa madarasa.

“Ujumbe wako Rais nimeupata, hakuna cha kusubiri, madarasa lazima tuyajenge na nikuhakikishie tayari tumeshaanza kuyafanyia kazi, na wanafunzi wote itakapofika siku ya kufungua shule Januari 6, wote wataanza kwa pamoja, hakuna cha wa kwenda baada ya kusubiri miezi miwili au mitatu ili tumalize madarasa,” amesema Waziri huyo.

Alimshukuru Rais Samia kwa kuendeleza sera ya elimu bila ada, kwani katika miezi yake miwili ya bajeti yake ya kwanza ya mwaka 2021/22 wameshapeleka kwenye halmashauri zote 184 Sh62.4 bilioni.

“Tunakushukuru Rais, kwani kulikuwa na uzushi kwamba elimu bila malipo itafutwa chini ya uongozi wako lakini wote ni mashahidi fedha zimeshakwenda katika halamshauri zetu katika shule zetu za msingi na sekondari.

“Katika hili tunakushukurum, umesaidia watoto wa maskini kupata elimu,”amesema Ummy.

Kutokana na sera hiyo ya elimu bila malipo, Waziri huyo amesema wanafunzi wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza ni takribani milioni moja wakati wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni 460 elfu kwa hiyo kuna ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza zaidi ya 500 elfu

VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA

View attachment 1960234

Hivi hiyo hela ni yake mfukoni? Hivi kwenye hiyo hela yeye na wale vigogo ambao kodi haiwahusu wanachangia nini?

Je kodi hiyo ni hii ambayo kakamuliwa huyu?

IMG_20210824_125202_848.jpg

Kisha sasa wanaitumia kama kampeni ya kujisimika mwanamke 2025?

Tunamsubiri:

Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

Huyu habari na imfikie, kuna komando wetu mzalendo mikononi mwa serikali yake kinyume cha sheria. Wamrejeshe akiwa hai:

IMG_20210824_125202_848.jpg
 
Hivi anajenga Nani hasa maana wabunge nao wanadai wanajenga wao ,katani nako madiwani hivyohivyo!
😀😀😀😀

Wanashirikiana wote na sifa ni za wote

#KAZI IENDELEE KWA KASI &NGUVU ZAIDI
 
Mkuu unataka kila kitu ifanye serikali kweli inawezekana?

Nadhani jitahidi kubadili namna ya kufikiri,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
Mkuu nafikiri wewe kidogo ulikuwepo hapo nyuma kuanzia kwa Mkapa kurudi nyuma

Kipindi hicho nakumbuka shuleni tuligawiwa madaftari, pen na penseli na ninaamini haya yalikuwa matunda ya Kodi za watu wetu pamoja na source zingine

Hii ya Sasa imezidi Kodi nyingi na kubwa bado Elimu nayo ni kama Mradi wa kuongeza Pato la Taifa.

Mbona kwa sasa Taifa limepata Mwanga na linaiona vyema Dunia kuliko zamani; na yale matendo bora ya kuwatia Moyo wanafunzi mbona yamekwama siku hizi?
 
Hivi hiyo hela ni yake mfukoni? Hivi kwenye hiyo hela yeye na wale vigogo ambao kodi haiwahusu wanachangia nini?

Je kodi hiyo ni hii ambayo kakamuliwa huyu?

View attachment 1960308

Kisha sasa wanaitumia kama kampeni ya kujisimika mwanamke 2025?

Tunamsubiri:

Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

Huyu habari na imfikie, kuna komando wetu mzalendo mikononi mwa serikali yake kinyume cha sheria. Wamrejeshe akiwa hai:

View attachment 1960308

Mkuu mnamsubiri wapi?

Kweli mtu anayejenga madaras manne kila shule Tanzania nzima haeleweki!

Kama mnaoshida kumshukuru Rais Samia basi mshukuruni Mungu kwaajili yake,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
 
Mkuu nafikiri wewe kidogo ulikuwepo hapo nyuma kuanzia kwa Mkapa kurudi nyuma

Kipindi hicho nakumbuka shuleni tuligawiwa madaftari, pen na penseli na ninaamini haya yalikuwa matunda ya Kodi za watu wetu pamoja na source zingine

Hii ya Sasa imezidi Kodi nyingi na kubwa bado Elimu nayo ni kama Mradi wa kuongeza Pato la Taifa.

Mbona kwa sasa Taifa limepata Mwanga na linaiona vyema Dunia kuliko zamani; na yale matendo bora ya kuwatia Moyo wanafunzi mbona yamekwama siku hizi?
Mkuu zamani aliyeona umuhimu wa Elimu alikuwa Serikali sio Mzazi,

Leo umuhimu wa Elimu anaona Mzazi sio Serikali kwa kiasi kikubwa,

Mkuu leo kuna watu wanalipa ada mil 42 kwa sekondri|msingi

Nadhani umegundua kwanini leo hivi,

Idadi ya wanafunzi pia ni kubwa sana

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
 
Mkuu zamani aliyeona umuhimu wa Elimu alikuwa Serikali sio Mzazi,

Leo umuhimu wa Elimu anaona Mzazi sio Serikali kwa kiasi kikubwa,

Mkuu leo kuna watu wanalipa ada mil 42 kwa sekondri|msingi

Nadhani umegundua kwanini leo hivi,

Idadi ya wanafunzi pia ni kubwa sana

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
Unaidanganya nchi Mkuu kusema Serikali haioni Tena umuhimu wa Elimu.

Hatujafanikiwa kabisa bado kuondoa ujinga. Vinginevyo tutaendelea kuwa na viongozi wasioweza kuapa siku zote.

Mbumbumbu ni wengi katika Serikali. Watu wanateswa na Mradi wa HESLB acha kabisa
 
Nawasalimu kwa jina la JMT,

Tanzania inajumla ya shule za sekondari 5,143 hii ni kwamujibu wa Shirika la Taifa la takwimu yaani NBS huku kati yake shule 3,863 ni shule za Serikali |Umma huku shule 1,280 zikiwa ni shule binafsi|Private schools,

Rais Samia Suluhu baada ya kupata anachokiita "Kijipesa " mahali sasa ameamua kuwatua mzigo wazazi kwa kujenga jumla ya madarasa mapya elfu 15,"Hii haijawahi kutokea " alisikika Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI akisisitiza chanzo ni " UTV Habari" jana trh 01|10|2020 Saa 2 Usiku,

Sasa ukichukua haya madarasa yote 15,000 ukayagawanya kwa shule zote za sekondari za Serikali 3,863 kila shule itapata wastani wa madarasa mapya manne ( 4 ) kwa lugha rahisi Rais Samia Suluhu Hassan ataongeza wastani wa madarasa manne katika kila shule ya serikali Tanzania nzima hakika Rais Samia Suluhu ni masikini anayekumbuka masikini wenzake,

Mtakumbuka pia ni jumla ya watahiniwa elfu 460 ndio wanatarajiwa kumaliza kidato cha nne mwezi ujao huku matarajio ya Wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza ni jumla ya wanafunzi milioni moja sawa na ongezeko la zaidi ya wanafunzi elfu 500,Hawa ndio walimnyima Mama Samia Suluhu Hassan usingizi na tayari amelimaliza hili, nakufanya kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuripoti kwa tarehe moja nchi nzima ambayo ni trh 06|01|2022

Hata hivyo watoto hawa hawatalipa ada hata mia kwani tayari Rais Samia ameshapeleka jumla ya Tshs 62.3bl kwa halmashauri zote 184 yaani mambo ni bam bam,

.........Kazi iendelee .........

==================================

Kidato cha kwanza 2022 wote kuanza shule siku moja
MONDAY SEPTEMBER 27 2021

Summary

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wanafunzi watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja.

Ummy amesema hayo leo Jumatatu Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma.

Amesema amepata maagizo kutoka kwa kiongozi huyo kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa asingependa kuona mwakani wanafunzi wanapishana kuanza shule kwa kisingizio cha uhaba wa madarasa.

“Ujumbe wako Rais nimeupata, hakuna cha kusubiri, madarasa lazima tuyajenge na nikuhakikishie tayari tumeshaanza kuyafanyia kazi, na wanafunzi wote itakapofika siku ya kufungua shule Januari 6, wote wataanza kwa pamoja, hakuna cha wa kwenda baada ya kusubiri miezi miwili au mitatu ili tumalize madarasa,” amesema Waziri huyo.

Alimshukuru Rais Samia kwa kuendeleza sera ya elimu bila ada, kwani katika miezi yake miwili ya bajeti yake ya kwanza ya mwaka 2021/22 wameshapeleka kwenye halmashauri zote 184 Sh62.4 bilioni.

“Tunakushukuru Rais, kwani kulikuwa na uzushi kwamba elimu bila malipo itafutwa chini ya uongozi wako lakini wote ni mashahidi fedha zimeshakwenda katika halamshauri zetu katika shule zetu za msingi na sekondari.

“Katika hili tunakushukurum, umesaidia watoto wa maskini kupata elimu,”amesema Ummy.

Kutokana na sera hiyo ya elimu bila malipo, Waziri huyo amesema wanafunzi wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza ni takribani milioni moja wakati wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni 460 elfu kwa hiyo kuna ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza zaidi ya 500 elfu

VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA

View attachment 1960234
Unajitutumua kweli mkuu, hongera kwa kuimba na kusifu, ila usije kata pumzi mapema tu.
 
Mkuu mnamsubiri wapi?

Kweli mtu anayejenga madaras manne kila shule Tanzania nzima haeleweki!

Kama mnaoshida kumshukuru Rais Samia basi mshukuruni Mungu kwaajili yake,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI

Tunamsubiri hapa:

Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

Anajenga madarasa kwa pesa asizochangia na tumshukuru kwa hilo? Sasa hapo anayejenga na kumpa yeye masurufu ya kufuru ni yeye au sisi?

IMG_20210930_170832_807.jpg

Ulipo wewe huoni hata umuhimu wa kumtaka kuwarejesha wote ambao kupitia kwa Sirro anaowashikilia kinyume cha sheria?
 
Mbona huu mwandiko kama wa yule jamaa,Hayati alisema kwa tafsiri ya kwao jina lake lina maana njaa
 
N vizur ila yasiwe madarasa hewa tafadhali na walimu tunao wa kutosha safi.
 
Hakuna aliyesifia hapa,

Mtu kafanya vizuri kuna kosa gani kusifia?

#KAZI IENDELEE KWA KASI NA NGUVU ZAIDI
Tumeishakugundua wewe ndio yeye, kizuri hujiuza na kibaya hujitembezq
 
Mbona asipofanya hamjilalamikii mnamlalamikia?

RAIS AKIPATIA NONGWA AKIKOSEA NONGWA SISI WATU WA NAMNA?

#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
Una kichaa nini? Is she doing us a favour ama anatimiza majukumu yake? Si aliomba hiyo nafasi mwenyewe? Kwani ni charity? Tatizo watanzania huwa tubaona kama tunafanyowa favour kuklmbe ni haki zetu

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Sijasema Serikali haioni umuhimu wa Elimu no,

Nimeseme ownership ya mtoto kupata elimu imekua zaidi kwa mzazi kuliko kwa Serikali zamani ilikuwa vesa versa,

Back
Top Bottom