CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😍😍😍Mungu ambariki na amfanye aendelee kututumikia Watanzania kwa upendo
Shule ipi?Serikali inaongea maneno mengi lkn ukienda kwenye mashule hakuna kinachoendelea
Sifa zote apewe Mungu wa Mbinguni,Wewe mtu unanipa raha sana,
Unaeleza vitu mpaka natama Samia atawale milele,
Hongera Rais Wangu,
Ushauri hayo madarasa yajengwe kwenye shule zenye upungufu sio kwa uwiano eti tuu kila shule iwe na madarasa 4..Rais Samia kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | Watoto wote 1M wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule Siku moja ambayo ni tarehe 06|01|2021
=====================================
Tanzania inajumla ya shule za sekondari 5,143 hii ni kwamujibu wa Shirika la Taifa la takwimu yaani NBS huku kati yake shule 3,863 ni shule za Serikali |Umma huku shule 1,280 zikiwa ni shule binafsi|Private schools,
Rais Samia Suluhu baada ya kupata anachokiita "Kijipesa " mahali sasa ameamua kuwatua mzigo wazazi kwa kujenga jumla ya madarasa mapya elfu 15,"Hii haijawahi kutokea " alisikika Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI akisisitiza chanzo ni " UTV Habari" jana trh 01|10|2020 Saa 2 Usiku,
Sasa ukichukua haya madarasa yote 15,000 ukayagawanya kwa shule zote za sekondari za Serikali 3,863 kila shule itapata wastani wa madarasa mapya manne ( 4 ) kwa lugha rahisi Rais Samia Suluhu Hassan ataongeza wastani wa madarasa manne katika kila shule ya serikali Tanzania nzima hakika Rais Samia Suluhu ni masikini anayekumbuka masikini wenzake,
Mtakumbuka pia ni jumla ya watahiniwa elfu 460 ndio wanatarajiwa kumaliza kidato cha nne mwezi ujao huku matarajio ya Wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza ni jumla ya wanafunzi milioni moja sawa na ongezeko la zaidi ya wanafunzi elfu 500,Hawa ndio walimnyima Mama Samia Suluhu Hassan usingizi na tayari amelimaliza hili, nakufanya kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuripoti kwa tarehe moja nchi nzima ambayo ni tarehe 06|01|2022
Hata hivyo watoto hawa hawatalipa ada hata mia kwani tayari Rais Samia ameshapeleka jumla ya Tshs 62.4bl kwa halmashauri zote 184 yaani mambo ni bam bam,
.........Kazi iendelee .........
==================================
![]()
Kidato cha kwanza 2022 wote kuanza shule siku moja
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.www.mwananchi.co.tz
Kidato cha kwanza 2022 wote kuanza shule siku moja
MONDAY SEPTEMBER 27 2021
Summary
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wanafunzi watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja.
Ummy amesema hayo leo Jumatatu Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma.
Amesema amepata maagizo kutoka kwa kiongozi huyo kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa asingependa kuona mwakani wanafunzi wanapishana kuanza shule kwa kisingizio cha uhaba wa madarasa.
“Ujumbe wako Rais nimeupata, hakuna cha kusubiri, madarasa lazima tuyajenge na nikuhakikishie tayari tumeshaanza kuyafanyia kazi, na wanafunzi wote itakapofika siku ya kufungua shule Januari 6, wote wataanza kwa pamoja, hakuna cha wa kwenda baada ya kusubiri miezi miwili au mitatu ili tumalize madarasa,” amesema Waziri huyo.
Alimshukuru Rais Samia kwa kuendeleza sera ya elimu bila ada, kwani katika miezi yake miwili ya bajeti yake ya kwanza ya mwaka 2021/22 wameshapeleka kwenye halmashauri zote 184 Sh62.4 bilioni.
“Tunakushukuru Rais, kwani kulikuwa na uzushi kwamba elimu bila malipo itafutwa chini ya uongozi wako lakini wote ni mashahidi fedha zimeshakwenda katika halamshauri zetu katika shule zetu za msingi na sekondari.
“Katika hili tunakushukurum, umesaidia watoto wa maskini kupata elimu,”amesema Ummy.
Kutokana na sera hiyo ya elimu bila malipo, Waziri huyo amesema wanafunzi wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza ni takribani milioni moja wakati wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni 460 elfu kwa hiyo kuna ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza zaidi ya 500 elfu
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA
View attachment 1960234
Sasa ukitaka tuseme wewe ndio unajenga au wananchi wanajenga? Acha ujinga.Pesa tulipe sisi ktk Kodi halafu useme Samia anajenga hizo Akili matope.
Samia hana pesa yeyote ni maskini tuu ndio maana tunamlipa mshahara sisi wananchi kwa Kodi zetu.
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Kwani we unaona vipi? Kunayo iliyosimama?Kwahio Hayo madarasa Manne una uhakika yatabeba wanafunzi wote kila kata Mkuu??...
Halaf Mkuu tukitoa hayo madarasa Mindombinu mingine Vip??Au unataka tu watoto waende shule halaf wamalize hawajui chochote??
Hao ni wale wenye fitina,hiyana na chuki tuu wala hakuna hoja ndio maana unaona wanahangaika kutaka akwame kitu ambacho hakitaa kitokee.Miondombinu gani hakuna mkuu wangu,
Hebu tuweni na shukrani wazee,
Mbona Mama anamaliza kila kitu kwa wakati yani,
#KAZI IENDELEE
Wakati mna praise yule mnyapara wenu haikuwa rubbish?BIG RUBBISH PRAISE AND WORSHIP
Kwani akisifiwa wewe unateseka nini? Amepitiliza wapi?Nahisi wewe ndiye Samia mwenyewe maana kila siku ni kusifia kulikopitiliza kama wale waliokuwa wakumsifia dikteta Magufuli
Nani kakwambia hakuna pesa iliyoingia? Darasa hata wiki 3 linakamilika.Yaan kama had tarehe ya leo hakuna pesa iliyo ingia hii ina maanisha ujenzi utaenda hadi mwezi machi 2022
Achana na wapuuzi hao Wana chuki tuu ila Mama atawafunika vibaya Sana.Mbona asipofanya hamjilalamikii mnamlalamikia?
RAIS AKIPATIA NONGWA AKIKOSEA NONGWA SISI WATU WA NAMNA?
#KAZI IENDELEE KWA KASI & NGUVU ZAIDI
Kwa akili zako fupi Kwani unadhani pesa huwa inatoka wapi kama sio kwa mwananchi?Hivi hiyo hela ni yake mfukoni? Hivi kwenye hiyo hela yeye na wale vigogo ambao kodi haiwahusu wanachangia nini?
Je kodi hiyo ni hii ambayo kakamuliwa huyu?
View attachment 1960308
Kisha sasa wanaitumia kama kampeni ya kujisimika mwanamke 2025?
Tunamsubiri:
Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao
Huyu habari na imfikie, kuna komando wetu mzalendo mikononi mwa serikali yake kinyume cha sheria. Wamrejeshe akiwa hai:
View attachment 1960308
Wewe umefanya lipi Kati ya ha hayo unayosema? Au unabwabwaja bila kuonesha mfano? Unataka nani akufanyie?Huu muda wa kusifia tungewekeza kwenye kutenda na fikra za kuboresha huenda wakulima wasingekosa wateja wa mahindi yao.., wala Wananchi wasingeminywa kwa Tozo wakati kuna vyanzo kede kede kuliko nchi zote zilizotunguka
Kumbe ulitaka usubirie baada ya mda gani? Hoji mwisho wa mwaka wa serikali Juni 2022..Update ya mwisho ya tozo za miamala ilikuwa inasoma 48B na viponit kadhaa walisema zinaenda kutengeneza vituo vya afya vip vituo vimefikia wapi au tusubiri baada ya mwaka ndio tuulize halafu mwezi huu wa tisa zimekusanywa ngapi maana nadhani ndio zinenda kujenga madarasa kabla ya januari inamaana kuna miezi mitatu kukamilisha madarasa elfu 15 kama vituo vya afya 160 havijafikia hatua ya ukamilishaji vipi tuamini tutaona madarasa elfu 15 kabla ya januari!?
Wazinguzi huwa hwakosekani kwani shule zote zimejengwa hivi?
Kwa akili zako fupi Kwani unadhani pesa huwa inatoka wapi kama sio kwa mwananchi?