Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Mwendokasi ni mpango wa kuifilisi nchi. Kwa nini wasingejenga city tram zikatumia umeme?
 
Hee huu ndo ujinga, kama hawana hali ya kutoa huduma nzuri si wawatoe?
Wasipokua na hio ari baada ya mkopo nani atalipa?

Au na wewe ni mnufaika ndo mana?
 
Huyu jamaa anapenda kukopa balaa
 
Serikali imejenge miundombinu, ikope hela kununulia mabasi kisha imkabidhi mwarabu kuyaendesha, akili matope hizi zinapatikana Tanganyika tu.
 
Tanzania wakubali tu mfumo wa SOEs (State Owned Enterprises) hawauwezi ni hasara tupu kila mahali

Serikali ya Tanzania haina ubunifu kwenye biashara ina speed ya trekta

Nikiangalia jinsi akina Abood, Shabiby, B.M n.k wanavyoweza kumanage biashara ya usafiri huwa nashindwa kuelewa kwa nini serikali huwa haitaki kuwashirikisha hawa wadau kwenye kutoa huduma

DART na UDART ni vitengo vya upigaji tu
 
kwenye kukopa tuko vizuri

kuendesha na kusimamia mradi
Ndiyo sifuri.....

Ova
 
Tuseme tu ukweli mali za serikali hamtunzi kabisa mnaingiza walipa kodi hasara kama nimadaladala yenu yanafanya kazi hata miaka 10 barabarani na hela manaingiza lakinj inakua vipi likija mali ya umma linahujumiwa na hakuna anaechukuliwa hatua wala kuwajibishwa hata mkikopa kwa utaratibu huu wakutotunza ni hasara kwa walipa kodi maskini
 
Serikali iache kufanya biashara, serikali ijenge miundombinu iwaite private sector tendering operators hata wa tatu na serikali irudishe gharama kwa kucharge hizi kampuni huku ikiboresha na ku maintain miundombinu. Hata SGR nilitoa ushauri serikali ikusanye tu fees isiingie kwenye issue ya kuendesha haya mashirika yalishakufa unawapa tena mtaji watauwa tena. Itafute njia ya kurudisha gharama sio tena kutoa mitaji na gharama za uendeshaji.

TRC na SGR mpaka leo sijui nini kipya wanacho ili isitokee yaliyotokea kwa Railway ya kati ya zamani. Ila nimesikia kuwa watakaribisha serikali hata private sector kutumia SGR kwa malipo na hili ni sawa na huduma za usafiri waachie private.
 
Mmmmmmmmmh 🤔 mabasi 100 wanataka mkopo sasa fedha zote zinazo kusanywa kwenye mradi tangu umeanzishwa zinakwenda wapi 🤔 wana gawana zote hakuna za kuendeshea mradi zinazobaki🤔 sasa ni kipi hii serikali inafanya kwa fedha zake unazo kusanya 🤔
 
Halafu baadaye kidogo watauziwa Waarab!
Tuliambiwa Kuna mwarabu mdubai amepatikana kuwa mbia.
Tukaambiwa Kuna mabasi yanashuka bandarini Mara gear imebadilishwa angani, tunakopa NMB.
Uganda wanatengeneza mabasi yasiyo tumia dizeli. Kwanini tusiagize kwa jirani? Au m7 amegoma kutoa Cha juu ?
Mimi naona atafutwe MTU mwenye daladala zaidi ya kumi apewe aendeshe huu mradi. Mtakuja kunishukuru.
Lakini kwa hizi PhD za kina Mhede & co. Hatufiki mbali.
 
Tungekuwa na mkuu wa isanga mwenye uchungu na nchi yake asingekubali huu upumbavu, bahati mbaya ni mwendelezo wa "mkayatizame"
 
Tukishanunua ndio tutamkodisha
 
Huyu ameiba sana pesa za umma na kuanzisha kampuni yake inajenga nyumba binafsi kama NHC inaitwa Venny company, huyu ni FISADI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…